Kaniambia ana HIV

monta

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2014
Posts
1,271
Reaction score
1,803
Hapa nilipo nimechanganyikiwa baada ya kuambiwa na mtu ambaye nlitokea kumpenda kupita kiasi kuwa ni muathirika wa VVU.Nilikutana nae sku chache zlizopita,ni msichana mrembo kupita kiasi nilimtongoza akasema anawachukia wanaume sikujua kwa nini.

Leo kaniambia kama kweli nampenda tukapime,nikamwambia poa,basi yeye akaamua kuniambia kuwa ana HIV na aliambukizwa na mvulana ambaye ndiye wa kwanza kwake.Nimelia sana kaniambia tuwe marafiki tu ila na yeye ananipenda ila hataki kuniua.

Hapa nilipo nimechanganyikiwa naona kama ndoto.
 
pengine alikua anakupima reaction yako,kwanini usngeenda?
 
Sasa Nini kimekuchanganya hapo.
 
Du pole mkuu shukuru huyo kawa muwaz kwel atakuwa anakupenda ndio maana kafunguka mwngn angechuna tu muwe wengi
 
Inaumiza sana ila kuwa HIV+ haimanishi mwisho wa maisha, maisha yataendele km kawaida, huyo dada anahitaji faraja yako kwa hiyo usije ukamtenga.
 
Huyo msichana Mungu ambariki sana, hatma ya maisha yako ilikuwa mikononi mwake
 
Wew mbona unamchulia mwenzio, sasa unalia nini??
kwani kafa??? na aliekwambia kuwa kuwa HIV+ ndio kufa nani.
we kama huja do nae unachanganyikiwa nini.
Kama kwel ameathirika usimtenge wala kumtangaza kama ulivyomtangaza hapa.


NOTE: Inawezekana ulikuwa unamsumbua sana, alafu yeye hakupendi kaamua kukutulizisha boli. Maana kunawanaume ving'ang'anizi hadi mtu anakereka.
 
Sioni kitu kilichokuchanganya hapo. Je angekuambukiza ungefanyeje si ungekuwa chizi. Mambo mengine ni kumshukuru Mungu na sio kuchanganyikiwa.
 
Acha kuchanganyikiwa wee vp potea ufie mbali umshukuru sana kwa kukuweka wazi tungekuwa tunajadili mengine saa hii ila usiache kuwa naye karibu kwani huyo ni muungwana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…