Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhashamu Maimbo Mndolwa amewahimiza Watanzania kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu, na kusema nchi inaweza kuingia katika mgogoro mbaya wa kikatiba kama watasikiliza watu wanaotaka kuahirisha uchaguzi huo.
Askofu Mndolwa amesema hayo leo Mei 11, 2025 Jijini Mbeya katika ibada ya kuwekwa wakfu Canon Jacob Kahemele kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya, ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Kwa kuwa Naibu Waziri Mkuu uko hapa na tuliombee Taifa zima kutoahirisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 kwa kuwa tutaingia katika mtanziko mkubwa na mgogoro wa kikatiba. Kama kuna changamoto zitafutiwe suluhu ziishe", ameshauri Askofu Mndolwa
Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema milango ya Serikali iko wazi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwasihi wenye hoja kujongea kwa mazungumzo.
"Ninachoweza kusema kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu utakuwa uhuru na wa haki huku nchi ikiendelea kuwa na amani",
"Uchaguzi utafanyika kwa uhuru na haki kama katiba inavyotaka, waliposikika waliotaka marekebisho ya sheria Serikali ilipitia na kufanya marekebisho ya sheria zinazosimamia uchaguzi na leo milango ya Rais Mhe. Dkt. Samia ipo wazi kwa yeyote mwenye kutoa malalamiko yake ili nchi iende mbele".amesema Dkt. Biteko