Kanisa katoliki lamsamehe aliyekamatwa akiondoka na Ekaristi Takatifu

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Kanisa Katoliki jimbo la Ifakara limemsamehe Enock Masala mwenye umri wa miaka 19 aliyetaka kutoroka na Ekaristi Takatifu kanisani.

kijana huyu alikamatwa julai 28, 2024 wakati wa misa ya kwanza Walinzi wa Kanisa hilo walimkamata na alipohojiwa na kamati ya ulinzi ya kanisa hilo alikiri kuwa yeye siyo Mkatoliki hajabatizwa wala hajapata mafundisho yoyote hivyo hajui utaratibu wa ibada wala kanisa hilo kwa ujumla

Hata hivyo Paroko wa Kanisa hilo amesema linaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na matukio ya aina hiyo.


 
Mvinyo? Asamehewe tu. Kanisa ni Nyumba ya Mungu haifilisiki.
 
Wakati nasoma seminary... Nilikula kal kamkate(ni ngano)

Siku hiyo baba askofu alikuja, watu walikuwa wanapewa hiyo mikate, ilikuwa baada ya mapumziko ndio shughuli inaanza, mie nilipopata taarifa hizo nikaona bora nisepe niingie mtaani haya hayanihusu, ukizingatia njaa ilikuwa imenikamata, wakati nachochora, sister akaniita, akaniuliza na kiingereza chake cha kihindi(whea arr yu gowing) 😂 akaniamuru niingie class, sasa njaa inanisokota, nilivyosikia mkate wa bwana nikaona huu siuachi ngoja nijipoze, wakati nimeoanga foleni, wanafunzi hawana mbavu, wanajua mie muislam, ila kwa kuwa school nilikuwa mchakaramu, mcheshi, mtukutu, kipenzi cha wengi.. Wakanivungia, aisee nikawa naona watu wanapiga goti wanapewa kitu mkononi wanasogea pembeni wanakula, wengine wanaweka mikono tumboni kuonesha unynyekevu wanaoanua kinywa wanalishwa, ilivyofika zamu yangu nikafanya hivyo, aisee sijamaliza hata hatua mbili kile kingano kishamung'unyuka😂🤣🤣.. Nikaenda kukaa wanangu wakacheka nami nikacheka siku ikaisha.
 
Zaman kulikuwaga na mastory eti kuna mtu alikabanza mdomoni mwake alivyofika nyumban akakitema ,alivyotema ikatoka damu badala ya mkate
 
Walikosea waliokuona wakijua hustahili ila wakakuacha , wao ndio waliandikiwa kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…