Kanisa katoliki lijitafakari

Madhebu ya dini kama hayawezi kushiriki moja kwa moja kama wadau kwenye majadiliano ya kutafuta suluhu kuhusu mikanganyiko ya kisiasa kama haya maswala ya chaguzi, ni bora yakafunga mdomo kuliko kutoa maoni ambayo yatayafanya yaonekane yapo biased.
 
Kupitia historia ya nchi yetu, hili suala la Rais akiwa na imani ya dini ya Kikristo anakuwa pia ni wa dhehebu la Katoliki. Hii ni bahati tu ama kuna kitu "somewhere under the line"
 
Hebu jikumbushe unajua Niwemugizi askofu wa jimbo la Rulenge alipokuwa Rais wa TEC alipotoa waraka ule alinyang'anywa passport na hajarudishiwa hadi leo vile yule katibu mkuu TEC father Saba hajarudishiwa passport hadi leo.
Ruwaich siyo mtu wa kuwa kupromised kirejareja.
Tuseme tu wameamua kuzama kiroho!! tusubiri
 
Siyo kanisa ndilo liloshiriki bali mapadre wake walishirika. Kuna utofauti wa maana ya sentensi yako. Kanisa kushiriki kama lingetoa maagizo ya hayo mauaji. Lakini kuna baadhi ya mapadre walishiriki na wengine hawakushiriki. Ni kama kusema Waislamu wa Ki Sunni walishiriki mauaji ya watu yaliyofanywa na ISIS. Ni kuwaonea maana sasa hivi tunawakosea waislamu kwa kuwaweka katika kundi moja na wauaji wa ISIS ama kuwaita ISIS waislamu wakati wale siyo waislamu bali ni wahuni na wauaji wanaojiita waislamu.
 
......
......Naunga mkono 200%
 
Ninadhani kanisa hili lilikuwa linakemea maovu wakati wa awamu ya 4 mkuu kilicho baki sasa limefumba macho na Mungu atuepushe na majanga yanayoweza kutokea maana chuki nchini zinazidi kuongezeka. Watu wanachukiana kwa itikadi za vyama, sasa watu wanaanza kulichukia hata kanisa kutokana na matamshi yao!! Oh Tanzania tumekumbwa na balaa gani? Wako wapi watu wenye hekima Kama ya mwalimu Nyerere watakao simama na kuukemea uovu na dhuruma na kuutaja kwa jina lake bila kuogopa na kujali dhuruma hizo zimefanywa na mtu mwenye cheo kikubwa kiasi gani!!? Mungu tuepushe na majanga yanayoweza kutokea ijapo kuwa wasababishaji tunao hapahapa na wameamua yatokee
 
Kwali Musa na Filauni wapo maana leo taasisi ya Ufipa inaomba msaada kanisa katoriki si bora basi kama ni hivyo wangeomba kanisa la Mwenyekiti.
 
Nafikiri tunaandika mawazo mengine ovyo ovyo. Kanisa ni kitu Holy. Litajitafakari vipi? Nafikiri ulichotakiwa kusema ni viongozi (Hasa sema Kiongozi) maana hawa ndio sisi binadamu tunaokosea na kuomba msamaha kila siku. Hakuna sababu ya mtu yeyote kutumia kosa la mtu mmoja (hata kama ni kweli) na kuanza kulitukana na kuandika mambo ya ovyo ovyo juu ya Kanisa Katoliki.
 
Mambo ya ovyo ya Kanisa Katoriki ndiyo yalizaa makanisa ya kiprotestante.

Tusisahau enzi hizo Kanisa hilo lilibariki biashara ya utumwa.
Haishangazi leo kuona baadhi ya maaskofu wao na Kardinali Pengo wana mawazo ya ajabu sana.

Siku zote wana ajenda za siri kuitawala Dunia. Rais akiwa Mkristo, wanahakikisha anakuwa Mkatoriki - Nyrere, Mkapa na Magufuli.

Freemasons wengi ndiyo hao hao hadi maaskofu na makardinali
 
Wakati vyama mbadala vikihangaika kutoa maoni, kukosoa na kupinga mawazo yasiyokuwa na manufaa kisiasa na kiuchumi hayakusikilizwa. Hata wale baadhi yao waliojitokeza kukemea na kuonya walionekana kuwa na mtazamo binafsi kwamba utashi binafsi si maamuzi na kauli ya taasisi nzima kuanzia za dini,AZAKI, n.k.

Hata kuonyesha hisia kwamba maovu yakuuwawa watu,kushambuliwa na kuibuka kwa makundi yasiyojulikana yaliishia kutazamwa tu.

Katika kipindi cha wiki moja kumeibuka usifiaji wa kitakatifu bila kusahihisha tulikopita. Kuanzia bungeni, taasisi za dini na hii itaendelea. Tumesahau kwamba vyama mbadala vikipiga kelele na kulalama kwa ukandamizaji.

Makovu ni makubwa na kufutika ni vigumu. Kusifia kila siku hakutashaulisha makovu yaonekanayo pachoni na maumivu yaliyojaa mioyoni. Tusiishie kusafisha nyumba leo wakati wageni wanakuja. Chaguzi za wasiwasi hazina maana kama usawa haukuwepo na kutokuwepo sasa na hata baadaye.

Viongozi wetu wa dini wanaanza kutoka hadharani bila aibu kama wana maslahi ya kifedha kwenye siasa hizi chafu.
 
Kama katoliki haikuungi mkono ujue Mungu hayuko nawe.
Nawaona bavicha inavyowauma rc kutoa tamko lenye tija kwa taifa...
 

Hawa viongozi wa Kikatoliki kuishi bila kuoa kuna "impair" uwezo wao wa kikatoliki. Ndio maana kwenye mila za kabila letu ukiwa mtu mzima halafu huna mke hushirikishwi kwenye vikao vya vya familia vya kutoa maamuzi ya masuala muhimu ya kifamilia!
 
Umeshasema mapande wake ndio walishiriki sasa ina maana kanisa linakaa na mijitu yenye roho za kishetani kuua binadamu wenzao, kama kanisa lilishindwa kuwachuja na kuwaondoa mapadre wa aina hyo je linawezaje kujitenga na matendo yao

Halafu kwa logic ya kawaida tu mapadre na maaskofu ndio wanabeba taswira ya kanisa hatutegemei wafanye tofauti na falsafa ya kanisa halafu tuseme eti sio kanisa limefanya.

Aliyoyasema askofu Nyaisonga ndio msimamo wa kanisa maana aliyasema akiwa katika shuguli zake za kichungaji.
 
Sure.... lkn n lazima utofautishe kati ya maamuzi ya kitaasisi na maamuz ya watu binafsi waliopo kwenye taasisi husika

Sawa. Kwa hili suala la uchaguzi wa serikali za Mitaa tungekuwa basi tumeshapata kauli rasmi ya kanisa kuwa yale yalikuwa maoni binafsi ya Askofu Nyaisonga.
 
Hili jiwe limeuma sana ufipani. Yaani nyuzi kibao za katolìki leo. Hata yule anayewalaza na viatu yule GOVERNOR wa dar Mr. Makonda wamemsahau kwa muda.
 
Aibu kubwa! utadhani hotuba yake aliandikiwa na polepole.
 
Pengo anazidi kutia pilipili kwenye vidonda ndoa ya kanisa na serikali za kidictator hazitaishia kwa Benito !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…