Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawajielewi hao mkuu achana nao usiwape faida kanisa katoliki litabaki kuwa katoliki wasikuumize kichwaMkuu mleta uzi unaonekana una bifu binafsi na kanisa katoliki kwa sababu yoyote unayoijua ww. Karibu kila dhehebu ama dini viongozi wa kisiasa hupewa nafasi ya kuwasalimia waumin na huzungumza mambo mbalimbali yakiweyo yanayoleta uchochezi, chuki na ubaguzi. Kama ni mfuatiliaji mzur kabla ya uchaguz lowasa alinukuliwa ktk kanisa moja la KKKT akihimiza achaguliwe eti kwa sababu hakujawahi tokea rais mlutheri .mbona hukutokwa na povu kama leo?, Anyway kanisa katoliki lianzaje kukemea serikali eti haijapandisha wafanyakazi madaraja mara hawajalipwa posho are you serious? Ina maana kanisa ligeuke kuwa chama cha wafanyakazi? Kazi ya vyama vya wafanyakazi ni zipi?. Mkuu kwa povu hilo dhidi ya kanisa katoliki "kunywa maji ulale tu hamna jinsi"
Huyo ni mkuu wa nchi popote atakapokuwa anayomamlaka ya kuwasalimia wananchi wakekwanini wanampa nafasi?,au wanaogopa atawatumbua nini?
Roman Catholic Church HierarchyUmeshasema alikuwa Jimbo la Dar....Kama alikuwa jimbo la Dar basi alikuwa chini ya Metropolitan ya Dar yenye Askofu mkuu Pengo...
Ni vyema mambo msiyoyajua wuwe mnaomba ufafanuzi kutoka kwa wanaofahamu
Roman Catholic Church HierarchyThibitisha pasipo shaka kuwa bosi wa Kilaini ni Pengo la sivyo hujuujui uongozi wa kanisa Katoliki Mkuu.
Umethibitisha kitu gani..?Nadhani nimethibitisha.
Roman Catholic Church HierarchyUmethibitisha kitu gani..?
Unapotembelewa na Mgeni Lazima umpe nafasi ya kusema neno, na neno hilo Lazima limhusu yy maana yy ndie Muongeaji siwezi kumwambia atoe neno gani,Habari wanabodi..
Awali ya yote ninaomba niwapongeze wale wote ambao wamefanikiwa kuuona mwaka mpya wa 2017.
Pili nawapa pole wale wote ambao wameanza mwaka kwa matatizo mbalimbali. Ninaamini MUNGU atawapa Faraja.
NAOMBA NIJIKITE KWENYE MADA.
Labda nianze kueleza taratibu za Kanisa Katoliki katika ibada zake.
Kanisa Katoliki lina sehemu kuu mbili za katika Ibada;
1. Liturjia ya Neno
2. Liturjia ya Ekaristi
Sehemu hizo zote mbili hazimruhusu mtu kusema neno lolote lililo nje ya utaratibu wa Kikanisa. Hata wakati wa matangazo hutakiwi kutangaza jambo ambalo Kiongozi Mkuu (Paroko au Askofu) halifahamu.
Pia Kanisa halina utaratibu wa kuruhusu mambo ya SIASA ndani ya Kanisa bali hutoa msimamo usiofungamana na upande wowote ili kutoadhiri msimamo wa Waumini. Japo linaruhusu KUKOSOA na KUPONGEZA PIA.
WAPI KANISA LINATAKA KUTUHARIBIA NCHI?
1. Kuruhusu hotuba za Kisiasa ndani ya Kanisa. Hili nionavyo mimi litaharibu Nchi. Wanasiasa wanayo majukwaa yao ya kuzungumzia mambo yao ya siasa na siyo Kanisani. Siku za hivi karibuni Kanisa Katoliki limekuwa likiwaruhusu wanasiasa kusimama Madhabauni na kutoa hutoba zao za Kiserikali na Kisiasa ama kwa kujibu hoja fulani au kutoa matamko ama kusambaza Kauli Mbiu fulani, (tafsiri yangu ya haraka hapa ni kwamba wanasiasa wanahitaji "mass support" hata kama wanafanya jambo baya). Kwa hili Kanisa halitendi haki maana viongozi wa Nchi hii ni wetu sote. Kama viongozi wetu wanahitaji kujibu hoja, kutoa matamko au kusambaza kauli mbio wasitumie NYUMBA ZA IBADA.
KANISA KATOLIKI WAPENI WATU NAFASI KANISANI YA KUSALIMIA TU NA KUSISITIJA JUU YA AMANI, UPENDO, MSHIKAMANO NA UWAJIBIKAJI NA SIYO VINGINEVYO.
2. Matamko ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Hawa viongozi ni lazima wajikite kwenye ukweli na siyo kujipendekeza. Nyakati hizi viongozi wa Kanisa Katoliki wamekuwa ni watu wa kupongeza tu bila kukosoa ukilinganisha na nyakati za nyuma.
a. Mmepongeza yale mazuri = VEMA.
b. Kwa nini hamkosoi na kusema ukweli juu ya mambo ambayo Serikali inakosea au hata kuhoji tu?. Mfano sijasikia mkikosoa au kuhoji juu ya,
i. Ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi.
ii. Matumizi ya fedha za wahanga wa Kagera.
iii. Nyongeza ya mishahara ambayo ni haki ya mfanyakazi.
iv. nk
KANISA KATOLIKI MKIENDELEA HIVI MTATUHARIBIA NCHI YETU.
Nawasilisha.