Kanisa Katoliki tuondoleeni utata huu. Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ni Padri au siyo?

Kanisa Katoliki tuondoleeni utata huu. Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ni Padri au siyo?

Baba Paroko hana pakuchomokea,Polisi hawawezi kukurupuka,naona mmeanza kumkana mtu wenu,

Akikutwa na hatia ale kitanzi tu,hiyo ni murder case,alitumia dini kujificha kama kimvuli tu.
 
Huyo msemaji wa polisi anapaswa kuwajibishwa kwa kuleta taharuki kwa kanisa katoliki.hakupaswa kuongea kwenye public bila kufanya uchunguzi wa kina .katudhalilisha sana waumini wa kanisa katoliki.
Wewe ndio ukamatwe ka kutaka kuficha ukweli. Hilo jina ni la padri kabisa na ni msaidizi wa paroko pale parokiani. Mnadhani kuna pa kujificha?. Imani inawafanya muwe wajinga sana
 
Wanatuchanganya.

Tukubali tu hakuna Padre au Paroko wa kuweza kufanya huu ujinga.
Hakuna anayekuchanganya ila unajichanganya mwenyewe,Paroko kwani wao ni malaika au binadamu kama sisi tu? Unapataje ujasiri wa kuwakingia kifua kua hawawezi kufanya huo ujinga?

Baba Paroko yupo nyuma ya nondo tayari,wewe kuiongopea akili yako kua hawezi kufanya huo ujinga ,haiwezi kubadili kitu.
 
Huyo msemaji wa polisi anapaswa kuwajibishwa kwa kuleta taharuki kwa kanisa katoliki.hakupaswa kuongea kwenye public bila kufanya uchunguzi wa kina .katudhalilisha sana waumini wa kanisa katoliki.
Huyo ni Padre anaonekana kwenye Directory ya Bukobadiocese.co.tz yuko Parish ya Rutabo na ameandikwa kwa jina la Fr. Elpidius Rwegoshora. Hivyo ni hakika ni Padre, pia tuelewe kuwa ubinadamu upo pale pale hata kama ni padre anaweza tenda dhambi pia.
 
Pia ndugu zangu tuwe wapole.
Hata mbuzi anaweza kutuhumiwa kula sabuni japo hajala.
Ikithibitika basi litakuwa lake.

Dhambi tunafanya sote.kubwa ni kutubu dhambi zetu mara kwa mara na kujitahidi kujiweka mbali na mazingira ya dhambi

Dah. Mtoto mdogo sana kapoteza maisha yake. Nmevaa viatu vya mzazi anayempenda mtoto wake
 
Angekua muislamu ungesema hivyo? Baba Paroko tayari yupo kwenye mikono salama,nenda kamtetee Mahakamani,kuiongopea akili yako hapa eti huenda hawajafanya uchunguzi wa kutosha,hakuwezi kubadili kitu.
NDIO maana nimesema hii taarifa ina walakini sijawahi na sina shabaha ya kuleta udini. SIJAWAHII kusikia padre au sheikh kufanya mauaji ya namna hii tena kwa mtoto asiye na hatia
 
Wanatuchanganya.

Tukubali tu hakuna Padre au Paroko wa kuweza kufanya huu ujinga.
Wapo kibao! Na masister Pia wapo sio mapadre pekee! Hadi walimu wa dini wapo!

Kama mtu anaweza kujinyonga kwa kushindwa au kufeli kuendelea na mafunzo ya upadre basi unaona kuna tatizo

Wapo wanazaa na wake za watu, Wapo wana fanya uhuni mpaka kero, wana lawiti watoto na hizi kesi hazipo Tz pekee ni Duniani na ndipo shinikizo linapo anzia kuwa wapewe ruhusa waoe
 
Back
Top Bottom