Napenda kulipongeza Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wakiongozwa na Rais wao Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu wa Iringa kwa kujitoa kwa nia ya dhati kuleta mabadiliko katika elimu ya juu kwa kupeleka huduma ya elimu ya juu katika maeneeo yaliyokuwa yamesahaulika kama Mtwara, Ruvuma, na Kagera, nawatakia kila la heri katika ule mpango wa kufika Kigoma, Biharamulo, Arusha, Singida, Zanzibar na kwingineko hivi karibuni, mwendelee na moyo huo huo kama mlivoweza kumiliki theluthi tatu ya utoaji wa huduma zote za jamii hasa Mashule na Hospitali kabla ya utaifishaji miaka ya katikati ya 1960, na baadae kwa dhati kabisa Mwadhama Laurian Kadinali Rugambwa kukubali kuzitoa kwa Serikali ya Mwalimu Nyerere ili zihudumie Watanzania wote.
Kwa hatua hii tunashukuru mpaka sasa kwa vyuo hivi!
1.St Augustine University of Tanzania Main Campus-SAUT,-MWANZA
2.Catholic University of Health and Allied Sciences-CUHAS,-MWANZA
3.Mwenge University College of Education-MWUCE,-MOSHI
4.Ruaha University College-RUCO-IRINGA
5.St Francis University College of Health and Allied Sciences-SFUCHAS,-IFAKARA
6.Archbishop Mihayo University College of Tabora-AMUCTA,-TABORA
7.Stella Maris Mtwara University College-STEMMUCO,-MTWARA
8.Bishop James University College of Songea-BJUCO,-SONGEA
9.Cardinal Laurian Rugambwa University College of Bukoba,-BUKOBA
10.Jordan University College-JUCO,-MOROGO
11.St Augustine University of Tanzania Dar es salaam Centre-DAR ES SALAAM
HONGERENI SANAAAA!