Kanisa la Askafu Gwajima bado limezungukwa na Askari Polisi hadi leo Juni 6, 2025

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708


​
Askari waliovalia sare za Polisi bado wameendelea kulizingira Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ikiwa ni baada ya taarifa ya kufungiwa kwa kanisa hilo.

Ikiwa leo ni Juni 6, 2025 ni siku ya nne mfululizo tokea ilipotolewa taarifa ya kufungiwa, askari wameendelea kuzunguka Kanisa hilo lililopo Ubungo, Dar es Salaam.

Hata hivyo bado njia zinazoelekea kwenye Kanisa hilo zimezungushiwa uzio unazuia watu kukatiza njia za karibu na Kanisa hilo.

Pia soma
~
Askofu Gwajima asema Kanisa la Mungu halijafungwa, tupuuze uzushi wa mitandaoni!

~ Serikali yalifutia usajili Kanisa la Askofu Gwajima kwa kuingilia masuala ya siasa kwa nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi
 
watekaji walazimika kuvaz upolisi ??
 
Wanaogopa litaibwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…