Kanisa la Baptist IFB: Heko Rais John Magufuli kwa msimamo wako juu ya corona na chanjo zake

Kanisa la Baptist IFB: Heko Rais John Magufuli kwa msimamo wako juu ya corona na chanjo zake

Verily Verily

Senior Member
Joined
Jan 4, 2007
Posts
192
Reaction score
148
TAMKO LA KANISA KUUNGA MKONO MSIMAMO WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA SUALA LA UGONJWA WA COVID-19 NA CHANJO ZAKE

1. UTANGULIZI:

Tamko hii halina malengo ya kisiasa kwa maana sio jukumu la kanisa kuhubiri siasa (1 Kor. 5:12; 2 Tim. 4:2). Hii ni taarifa fupi ambayo haitaweza kugusia kwa undani maana ya kiroho na kiunabii ya ugonjwa wa Covid-19 ulioenea katika mataifa yote ya dunia katika muda mfupi. Lengo la taarifa hii ni kumpongeza na kumtia moyo Rais John Pombe Magufuli na serikali yake kwa kusimama imara na kupinga ama kuhoji mbinu, taratibu,na makusudi ya mamlaka za dunia na vyombo vyake katika kuenea na hata kudhibiti ugonjwa huu duniani na ndani ya Tanzania. Rais yuko sahihi na kanisa la Bapist IFB tunamuunga mkono kikamilifu na kusimama naye sambamba katika msimamo huu.

2. RAIS AMECHAGUA FUNGU LILILO BORA
Kuna namna mbili za kupambana na tatizo. Ya kwanza ni kumtanguliza Mungu na ya pili, ni kuzitegemea akili za mwanadamu halafu Mungu baadae (Mit. 3:3-5). Rais Magufuli ameamua kumtanguliza Mungu. Sio jambo la kawaida kuona kiongozi wa dola anamtanguliza Mungu huku makanisa (sio yote) yakitanguliza juhudi za wanadamu katika janga kubwa kama hili. Msimamo wa Rais Magufuli na serikali yake uko wazi: Mungu kwanza. Msimamo wa makanisa (sio yote) hauko wazi lakini ni dhahiri hawajamtanguliza Mungu. Kanisa la Baptist IFB linaungana na msimamo wa Rais John Magufuli kwa kumtanguliza Mungu. Tunashauri waumini wetu na wote wenye ufahamu mzuri wa maandiko kusita, kufikiria mara mbili mbili na kujiridhisha kabla ya kukubali maelekezo kutokea katika mamlaka za mataifa ya nje na vyombo vyao kama (WHO, Vyombo vya habari kama BBC, CNN, Mashirika kama Bill and Melinda nk). Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili? Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya BWANA na juu ya masihi wake (Zab. 2:1-2). Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande (Dan. 7:23). Ikumbukwe pia kuwa serikali ya Rais John Magufuli imekuwa ikisimamia upande wa Mungu katika mambo mengine mengi ya kiroho huku makanisa yakisimama kinyume na maandiko, mfano: Uzazi wa Mpango, Kuhalalisha ushoga, Mabinti kupata mimba na kuruhusiwa kurudi mashuleni baada ya kujifungua, Vita dhidi ya Madawa ya Kulevya nk. Hili si bure bali kuna makusudi ya Mungu wa Mbinguni

3. MAGONJWA KATIKA UNABII
Biblia iko wazi kuwa mpinga Kristo na mamlaka zake watatumia magonjwa, vita na njaa kuitesa dunia. Kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na magonjwa mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni (Luka 21:11). Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa magonjwa na kwa hayawani wa nchi (Ufu. 6:8). Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao (Ufu. 13:8,16). Ieleweke kuwa chanjo sio chapa ya mpinga Kristo bali ni majaribio/ maandalizi yake.

4. COVID-19 NI SUALA LA KIROHO

Makanisa (sio yote) yamesahau wajibu wao wa kuwa macho kiroho. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze (1 Pet 5:8). Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake (Mat. 13:24-25). Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Efe.6:12) Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia (Luka 21:28). Hivyo ni halali kwa makanisa kusimamia maandiko katika jambo hilo na wala sio siasa nk.

5. MUNGU HUWEKA MAKIMBILIO KWA WATU WAKE
Neno la Mungu liko wazi: kila yalipoinuka mateso basi Mungu aliandaa makimbilio kwa ajili ya watu wake. Ni dhahiri kuwa Mungu anamtumia Rais John Magufuli na taifa la Tanzania kama eneo la makimbilio. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini (Uf. 12:6).

6. BWANA NDIYE AOKOAYE
Biblia iko wazi: Juhudi za mwanadamu sawa ni muhimu na lazima nazo zichukuliwe lakini Bwana ndiye akoaye. Kwa mfano, hizo juhudi wanazopigia kelele Tanzania kuwa haijazichukua ndizo wanazotumia wao na bado wanakufa Zaidi katika idadi ya maelfu tena kwa muda wa Zaidi ya mwaka mzima sasa. Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure (Zab. 121:1). Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini Bwana ndiye aletaye wokovu (Mit. 21:31). Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako (Mit. 3:5-6)

7. MWISHO
Tunampongeza, kumtia moyo na kumwombea Rais John Magufuli na serikali yake kusimama thabiti. Tupo sambamba naye katika vita hivi vya kiroho ambavyo wengine huviita vita vya kiuchumi. Ni vita vya kufa na kupona. Tunamwomba Mungu ambariki na kumtetea Rais John Pombe Magufuli na serikali yake na Mungu aibariki Tanzania inaposimama katika njia ya unyoofu.

IMETOLEWA NA UONGOZI
 
Matapeli yanatafuta favour. Makanisa ya kihuni
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom