Kanisa la EAGT rudisheni makanisa yenu yote mlikotokea TAG. Mnaichosha Serikali na migogoro yenu isoyoisha

Katika kanisa linaloongoza sasa hivi kwa migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ni EAGT.

Inaonyesha kabisa hawawezi kujisimamia kutwa kusumbua Serikali na msajili.

Hilo kanisa la EAGT walitokea Kanisa la TAG .Kule TAG kuna utulivu mkubwa na hakuna migogoro

Kanisa la EAGT rudisheni makanisa yenu yote mlikotokea TAG ambako kuna utulivu na ukomavu wa kiuongozi mnaichosha serikali na migogoro yenu isoyoisha.

Nawasihi viongozi wote EAGT wanaogombana humo Kuanzia Askofu mkuu wa EAGT na makundi yake na ya akina Mwaisabila na makundi yake na makundi mengineyo yaliyomo EAGT wakae wakubaliane makanisa yote warudishe TAG waendeshe chini ya TAG ambako kuna uongozi mkomavu na uliotulia nchi nzima.

EAGT mnalitia aibu kanisa na kusumbua Serikali.
Hata KKKT nao wanagombana tu 🤣🤣🤣,juzi hapa wanagombana mpaka wanafungiana milango ya makanisa.
Ni fujo tupu
 
Kundi la mwaisabila si wameshasajili Kanisa jingine, au bado halijazinduliwa, likizinduliwa tu mgogolo umekwisha.
Kuna mgogoro wa Mali wanataka kuondoka na mali za EAGT ikiwemo.majengo ya kuabudia nk yale yale ya Askofu Mwaikali wa KKKT aliyetaka kuondoka na majengo na mali za KKKT Dayosisi ya Konde na kuzifanya kuwa za Kanisa lake jipya la KKAM..Serikali ikabidi kuingilia kati kuwa huwezi ondoka na mali za taasisi nyingine na kuzipora kienyeji na kuzihamishia kwingine

Wangeondoka tu bila kupora mali za EAGT hakuna mtu wa kuhangaika nao.Ni kuondoka kwa amani na kwenda huko uendako ukatafute zako kwa hilo dhehebu lako jipya

Ndio maana nasema wanasumbua Serikali na mahakama.Mali zilizopo kisheria ni za EAGT sio za mtu binafsi awe mchungaji Askofu au yeyote.

Huwezi jimilikisha kanisa au jengo ukasema ni langu hata kama ulijenga mwenyewe ni mali ya taasisi husika .Majengo yote ya EAGT ni mali ya EAGT hata kama kuna mchungaji au mzee wa kanisa au Askofu au yeyote alijenga kwa nguvu zake peke yake zinabaki kuwa mali ya taasisi ya EAGT yawe magari ,majengo vyombo ,nk
 
Warudi tu kwenye dini yao ya asili kabla hawajawa wapendekoste. Nadhani kwenye asili yao ya Imani hakuna migogoro
Ni kweli kabisa. Roman Catholic hakuna migogoro ya kugombania madaraka
 
Kutoruhusu padri kuoa na kutokuwa na familia na majukumu ya kifamilia kumechangia kanisa katoliki kutokuwa na migogoro mingi ikiwepo iko michache si kuwa haipo mfano

A Roman Catholic cardinal who was once a close ally of Pope Francis has gone on trial in the Vatican, accused of misusing Church funds in a ruinous London property venture.
Cardinal Angelo Becciu, 73, is the most senior cleric in modern times to face trial for alleged financial crimes.
He is charged with spending €350m (£299m; $412m) of church money on a botched deal to buy a property in Chelsea that incurred huge losses.
 
Pesa pesa pesa
Pesa zenyewe zipo basi ukorofi tu
Mchungaji akijinunulia kapikipiki used tu kelele kibao na majungu kibao utafikiri majungu ya Yuda Iskariote alipoona Yesu anapakwa mafuta ya gharama na maria Magdalena akaanza mijungu na miyowe ohh mafuta yote haya ya gharama Yesu unajipaka yalitakiwa yakauzwe yasaidie maskini!!!

Kuna ma Yuda kwenye humo wa kutosha yasione mwenzao kapata chochote cha gharama mijungu na mikelele lazima uisikie
 
Kuna mgogoro wa Mali wanataka kuondoka na mali za EAGT ikiwemo.majengo ya kuabudia nk yale yale ya Askofu Mwaikali wa KKKT aliyetaka kuondoka na majengo na mali za KKKT Dayosisi ya Konde na kuzifanya kuwa za Kanisa lake jipya la KKAM..Serikali ikabidi kuingilia kati kuwa huwezi ondoka na mali za taasisi nyingine na kuzipora kienyeji na kuzihamishia kwingine

Wangeondoka tu bila kupora mali za EAGT hakuna mtu wa kuhangaika nao.Ni kuondoka kwa amani na kwenda huko uendako ukatafute zako kwa hilo dhehebu lako jipya

Ndio maana nasema wanasumbua Serikali na mahakama.Mali zilizopo kisheria ni za EAGT sio za mtu binafsi awe mchungaji Askofu au yeyote.

Huwezi jimilikisha kanisa au jengo ukasema ni langu hata kama ulijenga mwenyewe ni mali ya taasisi husika .Majengo yote ya EAGT ni mali ya EAGT hata kama kuna mchungaji au mzee wa kanisa au Askofu au yeyote alijenga kwa nguvu zake peke yake zinabaki kuwa mali ya taasisi ya EAGT yawe magari ,majengo vyombo ,nk
Maamuzi Kama yaliyofanywa kwa Askofu Mwaikali ndio yatakayofanywa EAGT na kwa wengine wanaopenda kujitenga, Chamsingi tu ni kusajili Kanisa lao, mgogolo umekwisha.
 
Ni sawa Migogoro kwenye mali hadi kwenye uislamu ilimalizika hivyo wakati Answar Sunna wakitaka kupora misikiti ya Bakwata na kuifanyia yao Serikali ikasema kajengeneni yenu mali za Bakwata ziacheni

Majaji na Msajili wawe wakali kama pilipili kwenye hili mtu akitaka kuondoka aondoke ila mali za taasisi husika ziache intact asiguse kukomesha.Polisi pia watoe msaada ruksa mtu kuhama dini katiba inaruhusu ila asiondoke na mali za taasisi ingine
 
Mie nashauri serikali itunge sheria ya kuthibiti migogoro kwenye makanisa na chini ya sheria hii kanisa lolote likihusika na migogoro ya waowao zaidi ya mara mbili, livunjwe na lifutiliwe mbali!
 
Nakumbuka kipindi Kuna kesi kati ya TAG na EAGT, jaji aliyepelekewa kesi alipofungua kinywa kuanza kusikiliza kesi alisema"Kwa kuwa watu hawa wanahubiri amani lakini wao wameshindwa kuitunza hiyo amani hivyo basi wamekuja kwetu tuwaamue".

Hii migogoro ni aibu kwa watu wanojinasibisha ni wafuasi wa kristo huwa naunga mkono serikali kuingilia kati kuwaamua maana wakati mwingine kanisani kunakuwa na majuha.
 
Katika kanisa linaloongoza sasa hivi kwa migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ni EAGT.

Inaonyesha kabisa hawawezi kujisimamia kutwa kusumbua Serikali na msajili.

Hilo kanisa la EAGT walitokea Kanisa la TAG .Kule TAG kuna utulivu mkubwa na hakuna migogoro

Kanisa la EAGT rudisheni makanisa yenu yote mlikotokea TAG ambako kuna utulivu na ukomavu wa kiuongozi mnaichosha serikali na migogoro yenu isoyoisha.

Nawasihi viongozi wote EAGT wanaogombana humo Kuanzia Askofu mkuu wa EAGT na makundi yake na ya akina Mwaisabila na makundi yake na makundi mengineyo yaliyomo EAGT wakae wakubaliane makanisa yote warudishe TAG waendeshe chini ya TAG ambako kuna uongozi mkomavu na uliotulia nchi nzima.

EAGT mnalitia aibu kanisa na kusumbua Serikali.
EAGT ndio spair gani ya gari?
 
Hizi Pentecostal churches hakuna kanisa wala kuabudu. Wanachojuwa ni kelele na kukusanya sadaka baada ya kuwatapeli waumini wao wenye FRUSTRATION. Hakuna mtu mwenye maisha yaliyonyooka anaabudu huko.

Kila muumini akipata vijisenti anafungua kabisa lake. Kwa hiyo makanisa yao yako linked na individuals. Moses Kulola kwa mfano alikufa jaribu ufuatilie uangalie kama bado kanisa lake lipo
lipo hapa mwanza linaendelea yupo mjukuu wake ndo kiongozi anaitwa dokta nani sijui
 
Je lina nguvu gani ? Ukilinganisha na lile aliloasisi Kulola mwenyewe? Isitoshe huyo Mjukuu hakubaliki na Baba zake wakubwa wanaoabudu kwa Mchungaji Katunzi wa City Centre Church.

Bado kuna mgogoro wa mirathi kati ya watoto, mke na marafiki wa Kulola. Shida tupu
 
Kutoruhusu padri kuoa na kutokuwa na familia na majukumu ya kifamilia kumechangia kanisa katoliki kutokuwa na migogoro mingi ikiwepo iko michache si kuwa haipo mfano

A Roman Catholic cardinal who was once a close ally of Pope Francis has gone on trial in the Vatican, accused of misusing Church funds in a ruinous London property venture.
Cardinal Angelo Becciu, 73, is the most senior cleric in modern times to face trial for alleged financial crimes.
He is charged with spending €350m (£299m; $412m) of church money on a botched deal to buy a property in Chelsea that incurred huge losses.
Utofautishe kati ya ubadhirifu/matumizi mabaya ya madaraka NA mivutano na migogoro inayotokana na fedha. Huo mfano wa kwako ni ubadhirifu/matumizi mabaya ya madaraka, lakini amri inatoka juu na huyo aliyefanya ubadhirifu anawajibika nalo. Tatizo la hayo makanisa ya kipentekoste ni kukosa chain of command, na inapotokea kuna jambo linaleta sintofahamu, hakuna mtu wa kushusha rungu na hivyo kila upande mmoja unajiona unaweza au upo sahihi, ndipo mivutano inapoanza na hata unakuta dhehebu linagawanyika
 
Back
Top Bottom