PreGE2025 Kanisa la FPCT lawataka watia nia kufanya siasa safi

PreGE2025 Kanisa la FPCT lawataka watia nia kufanya siasa safi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Baada ya Serikali kutangaza kuvunja mabaraza ya madiwani kote nchini huku Juni 27 mwaka huu Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuvunja Bunge 12 ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu Kanisa la FPCT Tanzania limewataka viongozi watakaotia nia katika nafasi mbalimbali kufanya siasa kwa amani.

Askofu mkuu wa makanisa ya FPCT Tanzania Askofu Steven Robert Mlenga ametoa wito huo juni 22 2025 wakati wa ibada ya kusimikwa kwa Askofu wa makanisa ya FPCT Mkoa wa Geita Askofu Devid Nzumbi ambapo Maaskofu hao wamewataka Watanzania kwa imani zao wazidishe maombi ya kuliombea Taifa katika kipindi hiki.

Viongozi wa Kanisa hilo pamoja na Waumini wamezungumzia tukio la kusimikwa kwa Askofu wa kanisa hilo huku wakilipa kipaumbele swala la kufanya maombi kwaajili ya Taifa.

Afisa Tarafa ya Busanda Fred Muhagama akizungumza kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Geita amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuwahimiza waumini wao kuitunza amani ya nchi


Chanzo: stormnews
 
Back
Top Bottom