- Source #1
- View Source #1
Hii ni kweli, kanisa la katoliki lawasisitiza watanzania kushiriki uchaguzi mkuu 2025?
- Tunachokijua
- Madai
Kipo kipande cha video kinachomuonesha Katibu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) akieleza masuala mbalimbali kuhusu kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, huku ikiambatana na ujumbe kuwa kanisa katoliki lasisitiza Watanzania kushiriki uchaguzi.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa yanapotosha uhalisia.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao kwa kupitia marejeo ya mahojiano aliyoyafanya katibu mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima na kituo cha habari cha Jambo TV Julai 8, 2025 alizungumza mengi lakini hakusema kuwa kanisa katoliki linawasisitiza Watanzania kushiriki uchaguzi.
Kipande kinachosambazwa hivi karibuni kimehaririwa kutoka katika video halisi ya Julai 28, 2025 ambapo Padre Kitima alikuwa akisisitiza mabadiliko yafanyike katika dosari zilizobainishwa na watu mbalimbali kuhusu mfumo wa uchaguzi ili walau kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru kama ulivyokuwa zamani.
Kuhusu CCM kushinda kwa 75% Padre Kitima alieleza kuwa hili linatokea kwa sababu upinzani ulidhoofishwa kuanzia mwaka 2015 na hivyo kuwaondolea ile nguvu yao katika uchaguzi.
Kuhusu muda kutokutosha wa kufanya mabadiliko makubwa ikiwemo kubadili katiba, Padre alieleza kuwa kwa kuwa muda uliopo hautoshi hivyo basi zile dosari zinazobainishwa na zinaweza kufanyiwa mabadiliko basi ifanyike hivyo ili kuwa na uchaguzi huru.
Katika mazungumzo yake hakusema kuwa wanawasisitiza wananchi kushiriki uchaguzi mkuu