PostGE2025 Kanisa la Moravian: Serikali isikilize malalamiko ya wananchi na wachukue hatua za haki kama walinzi wa amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kanisa la Moravian Tanzania limetoa tamko kuhusu matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, likiungana na Watanzania kutafakari na kusisitiza umuhimu wa amani, haki na mshikamano wa kitaifa.

Katika waraka huo uliotolewa Novemba 23, 2025, kanisa limesema matukio hayo yameacha majeraha ya kijamii na kiroho, na kuathiri familia nyingi. Kanisa lilikemea vikali vitendo vyovyote vya ukatili na kuvuruga misingi ya kitaifa, likisisitiza kurudi kwenye maadili ya Injili ya Kristo yenye upendo na haki.

Kupitia tamko hilo, kanisa limezitaka makanisa yote ya Moravian kuandaa ibada maalumu za maombi na toba kuanzia Novemba 23 hadi Novemba 30, zikilenga kuwaombea familia zilizoathirika, majeruhi, viongozi wa kitaifa, vyombo vya usalama na taasisi za utoaji haki.
1763975368498.jpeg

1763975385867.jpeg
 
Walikuwa wapi siku zote hizo
 
Back
Top Bottom