mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,205
- 19,142
Bwana Yesu apewe sifa. Nalisihi Kanisa la Mungu lililopo Tanzania limkumbuke Mch. Mbarikiwa Mwakipesile. Ninaposema Kanisa la Mungu la Tanzania simaanishi dhehebu! namaanisha ni watanzania waliomwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao na wanamwishia yeye kama alivyoagiza. Hawa wanapatikana kwenye madhehebu mbalimbali. Silengi dhehebu lolote.
Mch Mbarikiwa amepita na anaendelea kupita katika misukosuko na dhoruba nyingi sana na wote mnafahamu.
Alitegemea kuona Kanisa la Mungu linapaza sauti yake kwa Mungu kwanza (kumwombea kwa dhati), na kwa wale wanaohusika kwa namna moja au nyingine kumletea misukosuko ikiwemo serikali (ndiyo yenye mgogoro naye hadi walimfunga).
Alipoona aliowategemea kumsaidia wako kimya, aliumia sana na kuingiwa na uchungu mwingi na huo ukawa mlango wa adui kuingia na kumharibu zaidi.
Matokeo yake halisemi vizuri kanisa la Mungu hasa walioko kwenye makanisa ya kipentekoste! Hilo ni kosa kubwa kwa upande wake, lakini badala ya kumlaumu naomba asaidiwe! Ukimlaumu ni sawa na kumlaumu mtu mgonjwa kwa sababu ametapikia kitandani!
Hatupendi matapishi lakini hali ya mgonjwa inampelekea kutapika. Hali kadhalika hali ya mch Mbarikiwa inampelekea aseme hayo anayosema kuhusu watumishi wengine wa Mungu hasa Wapentekoste.
Mch. Mbarikiwa hayuko sawa, wala hayuko sahihi namna anavyowasema wapentekoste, ila wapentekoste na watumishi wa Mungu kwa ujumla wasimkasirikie! waielewe hali yake!
Naamini Mch Mbarikiwa anaweza kusaidika na ni mpambanaji mzuri wa jeshi la Mungu hapa Tanzania Kwa kipekee niwaombe Askofu Dickson Kabigumila na Askofu Gwajima (watu ambao naamini wanaielewa vizuri hali na mapito ya mch Mbarikiwa, na wanakubalika vizuri kwa mch Mbarikiwa), wamshauri asipambane/asiwakashifu wapentekoste maana hao ni ndugu zake katika Bwana hata kama anaona hawajasimama naye vizuri katika vita yake, hata kama hakubaliani nao kwa baadhi ya mambo ila wote tuna Bwana na Mwokozi mmoja.
Mch Mbarikiwa asiposaidiwa atapotea hivi hivi na ni aibu kwetu sote!