Kanisa la wa Sabato Tanzania lakanusha taarifa za kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini, lasema halijapokea ripoti ya CAG

Kanisa la wa Sabato Tanzania lakanusha taarifa za kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini, lasema halijapokea ripoti ya CAG

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Uongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania unapenda kutoa ufafanuzi kufuatia taarifa iliyosambazwa na vyombo vya habari kuhusu Bodi ya Wadhamini wa Kanisa, yenye kichwa cha habari kisemacho, "Bodi ya wadhamini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato yavunjwa kwa tuhuma za ubadhilifu."

Bodi inayotajwa katika taarifa hiyo iliteuliwa rasmi tarehe 12 Oktoba 2023, na tangu uteuzi wake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi na taratibu za Kanisa, na kwa kipindi chote tangu ilipoanza kutekeleza majukumu yake imezingatia misingi ya Sheria na utawala bora.

Kuhusu maelezo yaliyotolewa na kiongozi wa Rita kuwa hatua zilizochukuliwa za kuvunja bodi hiyo zinatokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kanisa linapenda kuweka wazi kuwa bado halijapokea rasmi ripoti hiyo, na kwa hivyo ni mapema mno kwa yeyote kutoa hitimisho kwamba kuna ubadhilifu. Mara tu ripoti hiyo itakapopokelewa, itapitiwa kwa umakini na kufanyiwa kazi kwa mujibu wa taratibu za kanisa, mifumo ya kikanisa, na kwa kuzingatia Sheria za nchi.

Uongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania unasikitishwa na namna habari hiyo ilivyotolewa kwa kuegemea upande mmoja bila kuzingatia mizania ya taarifa kwa kusikiliza maelezo ya Kanisa. Kufanya hivyo kunapingana na kanuni za maadili ya waandishi wa habari toleo la 2020, Kanuni ya 6.0 - "Haki na Usawa". Utoaji wa taarifa zisizokamilika au zisizo na mizania unaweza kuleta taharuki na kupotosha umma.

Uongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Union zote mbili bado upo, na unaendelea kusimamia misingi ya uwazi, uwajibikaji na uaminifu, na unawahakikishia waumini wake kuwa taasisi yao iko imara na inaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zake. Kwa sasa, Uongozi unawaomba waumini wetu wote kuwa watulivu, waendelee na kazi ya Mungu kwa uaminifu, na kuendelea kuliombea Kanisa na Taifa.

Soma > Unakula mpaka Sadaka aisee? Bodi ya Wasabato Tanzania Yavunjwa kwa Ubadhirifu wa Mali za Kanisa

SnapInsta.to_640926938_18340455478242767_3211838616534948718_n.jpg
 
Kanisa linapenda kuweka wazi kuwa bado halijapokea rasmi ripoti hiyo, na kwa hivyo ni mapema mno kwa yeyote kutoa hitimisho kwamba kuna ubadhilifu.
 
Back
Top Bottom