Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Roho zinaishi kwenye miili.
Sasa mbona wanahitaji mambo ya mwili kama zaka na sadaka kama lengo ni kiroho?
Narudia tena sio jukumu la kiongozi wa dini kumpangia kiongozi wa kisiasa
aendesheje siasa zake.

Nashangaa viongozi wa dini wanapata wapi muda wa kurumbana na wana siasa hali ya kuwa waumini wao wanafanya mambo ya hovyo mitaani.


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Yesu alisulubiwa kwa sababu ya siasa upo sawa kweli wewe?
 

Heroes ni mtawala, mwanasiasa, atamuuaje mtu ambaye hajihusishi na Siasa?
Unafikiri kwa nini walikuwa wakimuita Mfalme wa Wayahudi?
 

Hiyo ni katiba,biblia au Quran?,

Nikupe mifano ya Manabii na mitume waliokosoa watawala?
 
Sidhani kama uko sahihi mkuu, SDA siyo chama cha kisiasa, kwanini iingilie mambo ya kisiasa? Pia kwa msabato wa kweli haruhusiwi kujiingiza kwenye siasa!

Kwahiyo msabato kumkosoa mroma ni sahihi maana wote wako kwenye taasisi za kidini.
Umeshindwa kumwelewa mleta mada? Basi wewe ni aidha slow learner au msabato masalia mwenyewe.
 
Kwa hiyo Yesu alisulubiwa kwa sababu ya siasa upo sawa kweli wewe?

Sasa Unafikiri nini kilichomfanya asulubiwe?

Hapa ndio tutajua kweli wewe ni Msabato kweli au jina.

Embu nipe sababu na hoja kuntu zilizomfanya yesu asulubiwe.

Alafu mimi nakupa moja tuu ambayo ni maslahi ya kisiasa ndio sababu kuu
 
Walewale? Kuelewa kazi sana.
 
Kwann inabidi wakosoe watu in first place?
Wasabato wadeal na imani yao na kueneza imani yao, wasiingilie serikali kama chama cha siasa au kukosoa RC mana wao hawawahusu

Kueneza dini bila kukemea maovu ya watawala ndio uchawa ninaouzungumzia hapa
 

Sawasawa!
Serikali ikikosea ukaikosoa na kuirekebisha ndio kufanya siasa?
 
Wasabato si ndiyo wana uwezo wa kwenda popote duniani bila pasport, nauli wala Visa? Usiwategemee siyo wenzetu
 
Sawa msubirieni mbowe awasemee
 
Sasa kazi ya dini ni nini ? Ikiwa viongozi wa serikali wanatenda unyama, wanaiba kura na nyinyi mnaona hilo msiseme eti sio kazi yenu [emoji849]

Mnamsubiri mbowe awasemee
 
Naomba mstari kwenye Biblia unaosema Katoliki ni kahaba mkuu na mama wa makahaba please!!!
 
Wapi biblia imewapa wasabato hiyo haki ya kukosoa wengine?

Punguzeni ujuaji.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Sawa msubirieni mbowe awasemee
Mimi sio msabato, ila sipend hii issue ya wanasiasa kugeuza viongozi wa dini ni wanasiasa,
Itafika kipind cha uchaguzi TEC waseme wao hawaridhishwi na CCM bali wamependa sera za ACT ndio nzuri, kisha wasabato wakasema za CHADEMA ndio nzuri, KKKT wakazipenda za CCM,

Utakuta tunaanza kuchaguana kwa misingi ya dini, hatuna uhaba wa wanasiasa Tz kiasi cha kuanza kulazimisha viongozi wa dini wawe wakosoaji/wasifiaji wa serikali, wabaki kuwa observers wa karibu,

Tukiwaingiza sana kwenye siasa kuna siku tutalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…