Mnyanyaswaji naomba ufafanue uliposema "wakatoliki always ni wabinafsi" maana as long as i know ukiacha serikali kanisa katoliki ndio taasisi binafsi inaloongoza kwa kwa kutoa huduma za jamii kama afya, maji, shule, mashirika ya misaada (caritas n.k), kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu n.k. Je unamaanisha huduma hizi zote zinatolewa kwa wakatoliki peke yao? Sina hakika na hilo ushahidi nilionao unaonesha kwamba huduma hizo zinatolewa kwa watu wote bila kujali dini zao. Mfano ni kijiji cha matumaini dodoma wanalea watoto wote wakiwemo waislamu. Suala la kupora ardhi ya wananchi hata mimi siliafiki hata kidogo hasa kama limefanywa na mtumishi wa mungu. Mamlaka husika zinapaswa kufuatilia na kama ni kweli hatua za kisheria zichukuliwe. Sheria ni msumeno haibagui.