Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddeus Ruwa’ichi ametangaza kwamba kutokana na changamoto zilizopo katika eneo la Gezaulole ikiwemo maji kutuwama, mchakato wa ujenzi wa Kanisa Kuu Mbadala (Theotokos) lililotakiwa kujengwa Gezaulole, sasa litajengwa Pugu jimboni humo.
Tangazo hilo amelitoa leo Mei 9, 2025 wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya Pugu Marathon iliyofanyika Msimbazi Center, jijini Dar es Salaam.
#tumainitv
#radiotumaini30years
#tumainiletugazeti20years