Kanisani si kila anaelia amejazwa na roho mtakatifu wengine wanalia na shida zao

"Maisha yamekuwa magumu hadi ukienda kanisani kipindi cha maombi unalia na kuomba kwa uchungu watu wanafikiri umezama kwenye maombi kumbe ni uchungu wa maisha magumu."
Kutoa ya moyoni na kulia ni tiba. Kulia mbele ya madhahabu bila shaka itakuwa na carthasis kubwa zaidi. Wanafanya jambo jema na watiwe moyo badala ya kusimangwa.
 
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€kumbe unalia Kwa uchungu wakudaiwa Kodi,ada,mangi,umeme,maji... alafu kazi uliyonayo kipato akikizi maitaji au una kazi kbs n unga unga mwanaaa aiseeeeee,lazimaa hapo kanisanii unene Kwa uchungu sanaaa
 
1 Samweli 1:10

[10]Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana.

And she was in bitterness of soul, and prayed unto the LORD, and wept sore.
 
Siku hizi waumini wameacha kuomba kwa kulia, wameingia wachungaji wapya vijana wanaona ni ushamba kulia. Roho mtakakatifu hapewi nafasi kubwa watu waombe kwa kububujika kama zamani kanisa zima linabubujika hakuna anayeshangaa japo walikuwepo wanaolia kutokana na shida zao au kuigiza kunena kwa lugha
 
"Maisha yamekuwa magumu hadi ukienda kanisani kipindi cha maombi unalia na kuomba kwa uchungu watu wanafikiri umezama kwenye maombi kumbe ni uchungu wa maisha magumu."
Ivi mtu mzima unaliaje mbele za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ