Kanizidi umri lakini ana sifa hizi. Je, nijilipue nimuoe?

Kanizidi umri lakini ana sifa hizi. Je, nijilipue nimuoe?

Habari zenu,

Niko kwenye mahusiano na mwanamke ambaye kwa sasa ana miaka 30 kanzidi mwaka mmoja. mahusiano yana zaid ya miaka 6. (haya mahusiano hayakua straight mana kuna muda nlikua nahama mkoa hata miaka mi2, tena narudi tunaendeleza mahusiano). Kimuonekano mm sio handsome. Nina sura ya kawaida tu.

mwanamke huyu ana sifa zifuatazo
Yeye ni multiskilled, ni mpish mzuri sana yan akipika utajiramba, afu ni msusi afu ana ujuzi wa kushona kiufupi yy ni asset sio liability.

Miaka yote hyo hajawahi kuniomba pesa.(kuna watu mtasema eti kuna mwanaume ananisaidia majukumu). NO, huyu mwanamke n mpambanaji anafanya vibarua na sasa anafanya kibarua anacholipwa laki na nusu lakn hajawahi niomba hata 500 ya vocha.

Ni mwanamke mtiifu&anaenijali sana, nkiwa sina hela ya kula naenda kwake nakula nalala na asbuhi ananiogesha na nikiondoka siachi hata 100 na hajawahi nidai

Ni mwanamke mpambanaji na mwenye focus ya maisha yaan analipwa lak na nusu lakn kajibana mpaka kanunua vitu vyote vya ndani mfano kabati la nguo, la vyombo, kitanda, na vngine kwa pesa zake. sometimes hua ananipigia kakosa hela ya mboga anakula ugali na asali[emoji3064]

Kazn kwao wanatoka saa11 jion, akitoka kazn anaingia barabaran kwny zile folen anauza mataulo, chaja n. k kwa wale madriver.

LAKINI SASA:
Sikua na mpango wa kuoa kwa sasa lakn leo kanipigia smu anaongea huku akitoa sauti ya uchungu huku analia, anambia yeye anaona umri wake unaenda kwa hyo kama sina mpango wa KUMUOA n bora tuachane tu (naogopa nikimkosa je ntapata wapi mwngne kama yeye?)

Sura yake sio nzuri sana (simaanishi ni mbaya NO) ana sura ya kawaida tu yaan haivutii wala haikeri. mm pia sura yangu sio handsome nawaza watoto wetu si watakua na sura ambazo sio nzuri

Mimi bado nabangaiza na shughuli za ujasiriamali wa bidhaa ndogo ndogo, nikiingia kwny ndoa saiz hayo majukumu ya ndoa ntayaweza kwl?

Kanizid mwaka mmoja.

Nawaza sku nikikutana na mwanamke mwenye sura na muonekano naoutaka afu akanikubali je si ndo chanzo cha kuona nlikosea kuoa?

NB:sijamzalisha wala kumpa mimba.
Najua humu kuna watu wenye ujuzi na uzoefu wa haya mambo naombeni mnishauri jaman nimuoe au niachane nae??
Wewe oa weka ndani mpambane wote maisha menyewe ndo hayahaya, yaan unataka upambane mwenyewe jua lako mvua yako then uoe kamwanamke kaje kula tu mwishowe kanajaa tamaa kanakuua ili ukaachie mali,

Mimi nimeoa 2022 nilikuwa sina kitu chochote, tukawa tunashinda shambani wote huko, tumelima sana pamoja uzuri mke wangu mpiga kazi sana, mpaka sahivi tuna mtoto mmoja na tumefanikiwa kujenga na tumefungua biashara japo haijakaa kwenye ramani..mapambano yanaendelea.. mwanamke anatakiwa ajue uchungu wa mafanikio ndo awe na nidhamu siyo ayakute ,, mkuu kama mwanamke unamuelewa weka ndani mpambane.
 
Muogope sana mwanamke anayelia lia au mbwa dume anayechechemea.

Sasa jichanganye, wanawake wakifikaga umri kama huo kuwa wanyenyekevu ni kawaida.

Usitumie hisia oa ukiwa tayari.
 
sawa mkuu, nimekuelewa
 
Muogope sana mwanamke anayelia lia au mbwa dume anayechechemea.

Sasa jichanganye, wanawake wakifikaga umri kama huo kuwa wanyenyekevu ni kawaida.

Usitumie hisia oa ukiwa tayari.
sawa mkuu
 
Mbona naona Kama wewe ndio unampenda Sana, Alafu usi waamini wanawake Kama hao huaga ni waongo sana.
wanakuaga waongo kvp? huyu tangu namfahamu ndo tabia zake hajui ku-fake
 
Wewe inaonesha kigezo chako ni sura na Bado huna mpango wa kuoa. Ila huyo nadhani atakufaa sana kwa maisha ya ndoa. Ni wewe ndio Bado Kuna tatizo una tamaa za fisi (samahani) yaani Bado mroho unafikiria siku ukikutana na mwenye sura nzuri.
haswaaa uko sahh kabisa yan ww kweli umeielewa post yangu
 
Back
Top Bottom