Kanizidi umri lakini ana sifa hizi. Je, nijilipue nimuoe?

Wewe oa weka ndani mpambane wote maisha menyewe ndo hayahaya, yaan unataka upambane mwenyewe jua lako mvua yako then uoe kamwanamke kaje kula tu mwishowe kanajaa tamaa kanakuua ili ukaachie mali,

Mimi nimeoa 2022 nilikuwa sina kitu chochote, tukawa tunashinda shambani wote huko, tumelima sana pamoja uzuri mke wangu mpiga kazi sana, mpaka sahivi tuna mtoto mmoja na tumefanikiwa kujenga na tumefungua biashara japo haijakaa kwenye ramani..mapambano yanaendelea.. mwanamke anatakiwa ajue uchungu wa mafanikio ndo awe na nidhamu siyo ayakute ,, mkuu kama mwanamke unamuelewa weka ndani mpambane.
 
Muogope sana mwanamke anayelia lia au mbwa dume anayechechemea.

Sasa jichanganye, wanawake wakifikaga umri kama huo kuwa wanyenyekevu ni kawaida.

Usitumie hisia oa ukiwa tayari.
 
sawa mkuu, nimekuelewa
 
Muogope sana mwanamke anayelia lia au mbwa dume anayechechemea.

Sasa jichanganye, wanawake wakifikaga umri kama huo kuwa wanyenyekevu ni kawaida.

Usitumie hisia oa ukiwa tayari.
sawa mkuu
 
Mbona naona Kama wewe ndio unampenda Sana, Alafu usi waamini wanawake Kama hao huaga ni waongo sana.
wanakuaga waongo kvp? huyu tangu namfahamu ndo tabia zake hajui ku-fake
 
Wewe inaonesha kigezo chako ni sura na Bado huna mpango wa kuoa. Ila huyo nadhani atakufaa sana kwa maisha ya ndoa. Ni wewe ndio Bado Kuna tatizo una tamaa za fisi (samahani) yaani Bado mroho unafikiria siku ukikutana na mwenye sura nzuri.
haswaaa uko sahh kabisa yan ww kweli umeielewa post yangu
 
Yaani una umri mkubwa ila akili bado haijakomaa....."ananiogesha halafu siachi hata mia"....unaona sifa?
hapana sio sifa, sa ntampa hela hani wakati sina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…