Kansa ya damu inasababishwa na nini?

Kansa ya damu inasababishwa na nini?

kingfish

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Posts
571
Reaction score
159
Naomba nijulishwe huu ugonjwa unasababishwa na nini,dalili zake na tiba yake ni ipi?
 
SARATANI YA DAMU (LEUKEMIA)





Petechia%20hemmorhage_(1).jpg


Leukemia ni saratani inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph (lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.
Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali.

Leukemia husababishwa na nini?

Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.
Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya DNA, ambavyo kwa kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya kiumbe hai iweze kuishi, kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa, vinapobadilika maumbile na muundo wake kutokana na sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa DNA hujulikana kama mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa kasi zaidi kuliko kawaida, na pindi inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake huendelea kujizaa zaidi hatimaye kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.

Je, kuna vihatarishi vya leukemia?

Ndiyo vipo! Pamoja na kwamba chanzo halisi cha saratani ya damu hakijulikani, lakini kuna mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya damu.
Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya damu ni pamoja na:




    • Historia ya matibabu ya saratani hapo kabla: Watu ambao wamekuwa kuwa na aina nyingine za saratani hapo awali, na wakati wa matibabu wakapewa tiba ya mionzi au madawa makali ya saratani, wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu kwa sababu baadhi ya dawa hizi pamoja na mionzi huwa na tabia ya kuathiri pia seli nyeupe za damu pamoja na tishu zinazotengeneza seli hizo.
    • Kuwa na magonjwa mengine ya vinasaba: Ingawa haieleweki sawasawa uhusiano wake ulivyo, kuwa na baadhi ya magonjwa ya kinasaba kama vile ugonjwa wa Down syndrome, yasemekana huongeza uwezekano wa muathirika kuugua pia ugonjwa wa saratani ya damu.
    • Baadhi ya magonjwa mengine ya damu: Watu wenye magonjwa mengine ya damu kama vile ugonjwa wa damu unaoshambulia tishu za supu ya mifupa na kuzifanya zizalishe seli nyingi za damu bila uwiano unaotakiwa yaanimyelodysplastic syndromes, huongeza pia uwezekano wa mtu kuugua saratani ya damu.
    • Kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi: Watu ambao wamewahi kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi kama vile mlipuko wa mabomu au kulipuka kwa vinu na mitambo ya nuklea (nuclear reactors), wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya damu pamoja na saratani nyingine.
    • Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi kukumbana na baadhi ya kemikali kama vile benzene au zile zinazotumika kwenye viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza magurudumu au mabomba ya plastic, nao pia wapo katika uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu.
    • Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata aina mojawapo ya saratani ya damu.
    • Kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia: Watu ambao, baadhi ya ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu, nao pia wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba leukemia inaambukizwa isipokuwa kuna uhusiano wa kifamilia tu katika kusababisha ugonjwa huu.
Jambo moja la kufahamu ni kuwa, wapo watu wengi ambao wamewahi kukumbana na vihatarishi nilivyovieleza hapo juu bila kupata leukemia, kadhalika wapo waliopata leukemia bila kukumbana na kihatarishi hata kimoja kati ya hivi. Kwahiyo. Uwepo wa vihatarishi hivi haimaanishi kuwa ni lazima mtu apate leukemia isipokuwa inaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.


Makundi ya leukemia

Wataalamu wa afya wanaiainisha leukemia katika makundi mbalimbali kulingana na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa pamoja na aina ya chembe damu zilizoathirika.
Kulingana na aina ya chembe damu zilizoathirika, leukemia inaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili, ambayo ni:




    • Leukemia inayoathiri zaidi chembe damu zinazounda mfumo wa lymph ambayo kwa kitaalamu huitwa Lymphocytic leukemia. Mfumo wa lymph au lymphatic system ndiyo unaolinda mwili wako dhidi ya maradhi na maambukizi mbalimbali kama vile VVU n.k. Chembe damu zinazohusika hapa huitwa lymphocytes.
    • Leukemia inayoathiri zaidi chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani kwa kitaalamu Myelogenous leukemia. Aina hii ya leukemia huathiri chembe zinazoitwa myeloid cells, ambazo ndizo huzaa chembe nyekundu za damu, chembe nyeupe za damu pamoja na chembe sahani. Chembe nyekundu husaidia kusafirisha hewa safi ya oksijeni mwilini na kutoa hewa chafu ya kabondioksaidi, chembe nyeupe hupambana na vimelea wa magonjwa mbalimbali kama vile uti wa mgongo, minyoo, kifua kikuu, nk., wakati chembe sahani husaidia kuganda kwa damu pindi mtu unapoumia au kujikata.
Njia ya pili ya kuainisha makundi ya leukemia ni kwa kuangalia kasi ya kusambaa kwa ugonjwa wa saratani ya damu mwilini mwa muathirika. Kwa njia

hii, kuna makundi makuu mawili ya leukemia, ambayo ni:




    • Leukemia inayosambaa kwa haraka au wataalamu wanaita acute leukemia. Katika aina hii, chembe damu huwa changa, zenye mambo mabaya yasiyo ya kawaida, na zisizoweza kufanya kazi zao vizuri. Lakini mbaya zaidi, hujigawa na kuzaliana kwa kasi kubwa kiasi cha kusambaa na kujazana katika damu kwa muda mfupi sana.
    • Leukemia inayosambaa taratibu au kwa kitabibu chronic leukemia. Katika aina hii, chembe damu huwa zimekomaa na zenye uwezo wa kujigawa na kuzaliana taratibu na hata kufanya kazi zake kama kawaida. Chembe damu huweza kuishi kwa muda mrefu bila hata mgonjwa kuonesha dalili yeyote ya kuugua leukemia.
Aina za Leukemia
Bila kujalisha kasi ya kusambaa kwa ugonjwa au aina ya chembe damu iliyoathirika, leukemia inaweza kugawanywa katika aina zifuatazo:




    • Leukemia inayosambaa kwa haraka huku ikishambulia chembe damu zinazounda mfumo wa lymph yaani Acute lymphocytic leukemia (ALL). Aina hii huwapata zaidi watoto wenye umri mkubwa kidogo ingawa pia inaweza kwa kiasi fulani kuwapata hata watu wazima.
    • Leukemia inayosambaa kwa haraka huku ikishambulia chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani Acute myelogenous leukemia (AML). Aina hii ya leukemia inaongoza kati aina nyingine zote na huwapata watoto pamoja na watu wazima.
    • Leukemia inayosambaa taratibu huku ikishambulia chembe damu zinazounda mfumo wa lymph yaani chronic lymphocytic leukemia (CLL). Aina hii huwapata zaidi watu wazima, na nadra sana kutokea kwa watoto. Wagonjwa wa aina hii ya leukemia huweza kuishi vizuri kabisa bila kuwa na dalili zozote zile.
    • Leukemia inayosambaa taratibu huku ikishambulia chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani chronic myelogenous leukemia (CML). Watu wazima ndiyo waathirika wakubwa zaidi wa aina hii ya saratani ya damu. Mtu mwenye aina hii ya leukemia anaweza akapata dalili chache au asiwe na dalili kabisa kwa miezi hata miaka kabla ya ugonjwa kufumuka ghafla na kuanza kumshambulia.
Dalili za leukemia ni zipi?
Dalili za leukemia hutofautiana kutoka aina moja mpaka nyingine. Hata hivyo, dalili za jumla za leukemia ni pamoja na;




    • Homa au kujihisi baridi
    • Uchovu na ulegevu wa mwili
    • Maambukizi ya mara kwa mara
    • Kupoteza uzito bila kukusudia
    • Kuvimba tezi za mitoki
    • Kuvimba wengu (splenomegaly)
    • Kuvimba ini (hepatomegaly)
    • Kutokwa damu kirahisi na kupata michubuko ya mara kwa mara
    • Kuvilia kwa damu chini ya ngozi
    • Kutokwa jasho kupita kiasi hasa nyakati za usiku
    • Kuhisi maumivu ya mifupa
    • Kupungukiwa damu mara kwa mara
Mara nyingi dalili za Leukemia hazipo wazi na ni rahisi sana kwa mgonjwa kuchanganya na dalili za magonjwa mengine, hivyo ni vema kuwahi hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina na vipimo, mara tu uonapo dalili zilizotajwa hapo juu.

Uchunguzi na vipimo

Ni rahisi kwa daktari kugundua leukemia inayosambaa kwa kasi (acute leukemia) kuliko ile inayosambaa taratibu (chronic leukemia). Mara nyingi leukemia inayosambaa taratibu hugunduliwa mgonjwa anapoenda hospitali kwa ajili ya matibabu ya kitu kingine tofauti.
Pamoja na kukuuliza historia yako kwa lengo la kufahamu dalili na vihatarishi vya ugonjwa huu, daktari pia atakufanyia uchunguzi wa kina wa mwili kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa viashiria vya saratani ya damu kama vile ngozi nyeupe (katika viganja, macho au ulimi), kuvimba kwa tezi za mitoki, kuvimba wengu na ini; kuvilia damu katika ngozi, michubuko, au kama una dalili zozote za upungufu wa damu mwilini.

Vipimo utakavyofanyiwa ni pamoja na
Kipimo cha damu almaarufu kama Full Blood Picture ambacho huonesha kiwango cha kila chembe damu iliyopo mwilini. FBP huonesha kama chembe damu nyeupe zimeongezeka ama la, sambamba na chembe damu nyingine. Pia huonesha kiasi cha wingi wa damu, na iwapo mgonjwa ana upungufu wa damu ama la. Kwa ujumla wagonjwa wa leukemia huwa na ongezeko kubwa la chembe damu nyeupe zilizo changa, wakati chembe damu nyekundu pamoja na chembe sahani huwa chini.
Kipimo cha supu ya mifupa (bone marrow biopsy) hufanyika kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa seli za saratani. Kipimo hiki hufanyika kwa kuchukua sehemu ya mfupa wa nyonga au paja, kisha kuepelekwa maabara kwa uchunguzi. Biopsy husaidia kutofautisha kati ya leukemia na magonjwa mengine ambayo husababisha kuwepo kwa ongezeko la chembe damu nyeupe. Kwa maneno mengine, hiki ni kipimo tosha cha uthibitisho wa kuwepo kwa leukemia.
Vipimo vingine ni pamoja na vile vinavyoonesha utendaji kazi wa figo (renal function tests) na ini (liver function tests).

Baadhi ya madaktari hupenda pia kufanya kipimo cha uti wa mgongo (lumbar puncture) ili kuchunguza uwepo wa chembe za leukemia katika maji ya uti wa mgongo (spinal fluid).

Matibabu
Matibabu ya leukemia hutegemea mambo mbalimbali kama vile hatua ugonjwa ulipofikia, umri wa mgonjwa, hali ya jumla ya kiafya ya mgonjwa, na aina ya leukemia.
Leukemia inaweza kutibiwa kwa kutumia:
Dawa za kuua seli za saratani (chemotherapy): Hii ni njia kuu ya matibabu ya leukemia, ambapo dawa hutumika kuua seli zenye saratani. Kutegemeana na aina na hatua iliyofikiwa na ugonjwa, mgonjwa anaweza kupewa dawa moja au mkusanyiko wa dawa kadhaa tofauti tofauti kwa muda fulani.

Tiba ya mionzi (radiotherapy): Njia hii hutumia mionzi yenye nguvu kubwa iliyoelekezwa kwa ajili ya kuua chembe za leukemia na kuzuia ukuaji wake. Mionzi inaweza kutolewa katika eneo fulani maalum la mwili ambapo kuna kusanyiko la chembe za leukemia au mwili mzima.

Dawa zinazoelekezwa mahsusi kuua viasili vya seli za saratani (targeted therapy): Dawa hizi hufanya kazi maalum ya kuzuia seli kuzaliana au kujigawa kwa kuingilia mfumo wake wa utendaji kazi.

Tiba ya upandikizaji (stem cell transplant): Tiba hii hufanyika kwa ajili ya kurejesha sehemu ya supu ya mfupa iliyoharibika kwa kuweka supu mpya. Kabla ya tiba hii, mgonjwa hupewa dawa za kuua seli za saratani au mionzi ili kuua kabisa eneo lililoathiriwa kisha supu mpya hupandikizwa. Mara nyingi supu hii hutoka kwa mtu mwingine (donor) au inaweza ikatoka kwa mgonjwa mwenyewe kwa kuchukua sehemu ambayo haijaathirika.
Na njia nyingine ni tiba ya kuchochea mfumo wa kinga ya mwili kuzitambua, kushambulia na hatimaye kuua seli za saratani (biological therapy).


Nini cha kufanya?

Saratani ya damu ni jambo la kutisha na kusikitisha hususani kwa familia ambayo inamuhudumia mgonjwa wa tatizo hilo. Aidha ni jambo la kuhuzunisha sana kwa wazazi wenye mtoto aliyegunduliwa kuwa na ugonjwa huu. Kwa familia iliyokumbana na tatizo hili ni vema kufahamu nini cha kutarajia na kufanya. Kwa mzazi, hana budi kutafuta taarifa zaidi ya ugonjwa wa mtoto wake, aina ya ugonjwa, hatua iliyofikia na aina za matibabu yanayomfaa mtoto wake. Kwa mgonjwa, ni vema kufuatilia ushauri wa wataalamu wa afya na kuwa makini katika kutoa taarifa ya mabadiliko yeyote unayoyaona kuhusu maendeleo ya afya yako.

Kwa jamii nzima, ni muhimu kujiepusha na vihatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano mtu kupata saratani ya damu.http://www.tanzmed.com/component/k2/item/180-saratani-ya-damu-leukemia.html

 
Herbal Treatments for Leukemia


Leukemia is a type of cancer that affects the white blood cells. These blood cells are responsible for fighting infection in the body. Symptoms of leukemia may include bruising easily, unexplained weight loss, fever and lack of energy. With treatments such as chemotherapy, stem-cell transplant and radiation, leukemia can be cured, according to the U.S. Library of Medicine. Using herbal treatments for leukemia may also help fight off cancer cells.

Licorice Root


  • Licorice root is grown in Europe, the Mediterranean and Asia, and is a traditional ingredient in Chinese medicine. This herb may also kill cancer cells and prevent mutations in the DNA, explains the American Cancer Society. Licrocoumarone, a compound found in licorice root, is believed to be responsible for these benefits.

Shark Cartilage


  • According to the Leukemia and Lymphoma Society, shark cartilage is an herbal supplement used by patients to boost the immune system. Giving the immune system more strength may allow the body to more efficiently fights cancer cells.

Ginseng


  • Ginseng contains a couple dozen compounds which are called "ginsenosides." These compounds have the same effect on the body as steroid hormones, which may strengthen the immune system and slow the growth of cancer cells.

Flaxseed Oil


  • Flaxseed oil has been promoted as an anti-cancer agent for several decades, according to the American Cancer Society. The oil extricated from flaxseed is believed to strengthen the immune system and fight cancer cells. Flaxseed can be taken in supplement form, and added to diet through consuming raw flaxseed in cereals or eating breads that contain this ingredient.

Herbal Supplements to Avoid


  • St. John's Wort may be effective in improving mood in patients, however, it can interfere with chemotherapy medications, explains the Leukemia and Lymphoma Society. Also, dietary antioxidant treatments may interact with radiation therapy. The supplement laetrile should also be avoided, which can cause cyanide poisoning. "Mega doses" of vitamins may cause liver disease, nerve issues and balancing problems for patients.





 


fotolia_6884407_XS.jpg


Photo Credit Herbs image by Tomasz Cebo from Fotolia.comLeukemia is a type of cancer that affects your blood vessels, such as the lymphatic system and bone marrow. Symptoms include fever or chills, weight loss, fatigue, easy bleeding, red spots on the skin, bone pain and sweating. Treatment can include chemotherapy, radiation therapy and stem cell transplant. Certain herbal remedies may also help treat leukemia. You should consult your doctor before starting any herbal remedies. In addition, you should not replace other forms of treatment with herbal remedies.

MILK THISTLE


Milk thistle is a herb that originates from the Mediterranean region. This herb is commonly used for ailments of the liver, and it may also help decrease growth of certain types of cancer. According to the National Center for Complementary and Alternative Medicine, this herb is also being studied for its benefit in patients with leukemia and chemotherapy-related damage to the liver. Studies are ongoing and no evidence is established at this time.




KOREAN RED GINSENG

Korean Red Ginseng is a herbal remedy that may be beneficial in treating and managing leukemia. A study published in the 2008 Journal of Ethnopharmacology examined how this herb can inhibit telomerase activity and cause apoptosis in human leukemia cells. These two actions can benefit the management and slowed progression of cancerous cells. According to their findings, this herb may be beneficial if you have leukemia.
TURMERIC

Myeloproliferative disorders are a group of conditions that lead blood cells to abnormally grow within blood vessels. One of these conditions is chronic myelogenous leukemia, a type of leukemia in which the bone marrow synthesizes abnormal white blood cells in your bone marrow. Some herbs may be used for these disorders in order to help strengthen your body's defense systems. One herb that has been used is turmeric. The University of Maryland Medical Center indicates that a dose of 300 mg, three times/day, may reduce pain and inflammation associated with leukemia symptoms.


OLIVE LEAF


Another herb that may be used in the treatment of leukemia is olive leaf, also called olea europaea. The UMMC says that a standardized extract of 250 to 500 mg, for one to three times a day, may offer you anti-cancer effects and increased immune support. By boosting your immune strength, you may be better able to fight infection and illness or other symptoms of leukemia.


Beets as A Leukemia Natural Treatment

Did You Know… that beet juice is an astonishingly effective treatment for leukemia and other cancers?
The beautiful crimson color of the beet comes from betacyanins, natural compounds that also happen to be extremely powerful cancer-fighting agents. Beets also contain an amino acid called betaine, packed with anti-cancer properties and unique phytochemicals called betalains.
beets-as-leukemia-treatment-300x199.jpg


All of these nutrients are key to the incredible health properties of the beet. Betanin, one of the most researched betalains found in beets, has significant anti-inflammatory, antioxidant, and detoxifying effects.

According to The World’s Healthiest Foods (a website run by the not-for-profit George Mateljan Foundation, devoted to fostering a healthier world), recent lab studies found that betanin pigments can impede tumor cell growth in tissues throughout the body, including the . . .

  • Stomach
  • Nerves
  • Lungs
  • Breasts
  • Prostate
  • Testicles
These findings provide a compelling case for further research into the value of betanins and other betalains in preventing and curing cancer.
Because beets contain antioxidant and anti-inflammatory molecules, it is statistically likely that they can reduce the risk of many kinds of cancers. With the high antioxidant content, beets are a great leukemia natural treatment. The World’s Healthiest Foods says, “Eventually, we expect to see large-scale human studies that show the [cancer] risk-reducing effect of dietary beet intake.”

So Powerful That 100% of Cancer Patients in one Study Responded Positively!


A solid scientific basis for that work already exists. In the 1950s, a Hungarian cancer therapist named Alexander Ferenczi began putting his patients on a regime of raw or juiced beetroots in addition to their normal diet. He worked exclusively with patients who had already undergone chemotherapy and radiation, and who were primarily in the final (cachexic) stage of cancer. 


All of Ferenczi’s patients responded positively to the addition of beets to their diets. There was a clear,

clinical improvement in each and every one of their cancers
. The beet treatment proved to be so powerful, in fact, that in some cases patients actually overdosed on beets!

In some cases, the mass injection of nutrients — especially vitamin C — contained in the beets overloaded the patients’ livers.


So, the takeaway lessons from Ferenczi’s work are that:
Beets are a more effective cancer treatment when begun early. In fact, the regular consumption of beets might be most effective as a preventative treatment.
To avoid overwhelming your body’s waste disposal system, start with small quantities of beetroot and gradually increase. If you start to feel unwell, reduce your consumption.

Beets Fight Leukemia, Tumors, and Advanced Inoperable Cancers


The results of a later study of “red beet therapy” — the consumption of approximately 2 lbs of raw, mashed beets daily — corroborate Ferenczi’s findings and suggest that beets can help your body fight against leukemia and tumors.
While eating mass quantities of mashed beets may not be the most appealing option, it may be possible to get similar results in a more digestible format. In one clinical trial, 22 patients with advanced inoperable cancers were given 10 oz. of beet juice daily for 3 to 4 months.
All but one of those patients showed marked improvements in health. Surely that’s enough to make anyone regard beets in a whole new light.
It seems clear that beets are indeed a mighty health resource. They are high in folate — a compound necessary for bone health — and not only have they been shown to be a potent anti-cancer treatment, but they also detoxify the liver, kidneys, gallbladder, blood and lymph. Beets are also helpful for relieving constipation.

How to Get the Best Benefit from Beets



Beet juice
is such a strong substance that it should not be consumed on its own. Rather, mix it into another milder juice such as carrot, cucumber or apple. Dana Herbert, a natural health blogger, offers this advice to those interested in making beet juice from scratch:

“When juicing beets, alternate between pieces of beets and pieces of carrots, otherwise the beet pulp tends to build up on the sides of the spinning extraction basket and causes the juicer to vibrate.”
Dana also recommends chilling the juice for 2-3 hours prior to consumption.


The health-promoting pigments in beets can stain your skin, so it might be best to wear gloves while preparing them. If your hands do get stained, try lemon juice as a quick and nicely scented way to clean them!

Heat diminishes the concentration of phytochemicals in beets, so if you choose to cook them, World’s Healthiest Foods recommends steaming them lightly for 15 minutes, which will maximize their nutrition and flavor.





 
Asante sana kwa ufafanuzi wako mzizimkavu.ugonjwa huu ulimuua mdogo wangu niliyemwachia ziwa miaka 31 iliyopita.alikufa akiwa na miaka kumi.niliambiwa na wazazi kuwa alikuwa na kansa ya damu.sikuelewa ulikuwa na ugonjwa wa namna gani.asante kwa ufafanuzi huu.
 
P
Asante sana kwa ufafanuzi wako mzizimkavu.ugonjwa huu ulimuua mdogo wangu niliyemwachia ziwa miaka 31 iliyopita.alikufa akiwa na miaka kumi.niliambiwa na wazazi kuwa alikuwa na kansa ya damu.sikuelewa ulikuwa na ugonjwa wa namna gani.asante kwa ufafanuzi huu.
Pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom