Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Pole sana ndugu yangu; niliuguza mama mkwe akiwa na saratani ya matiti mwishowe akatuacha. Ila kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike aliyeiwahi akapona na sasa hivi anaendelea na maisha kama kawaida. Inategemea sana saratani hiyo iligundulika ikiwa stage gani. Ninakuombea sana Mungu akupe faraja na itokee kuwa iligundulika katika stage za awali
 
Daah inasikitisha ila ndo hivyo inasaidia kujiandaa kisaikolojia
 
Kaka nimepambana sana kusoma message zako PM lakini nimeshindwa sijajua tatizo nini.... Naomba niandike apa hii no uwasiliane na uyu mtu 0657 163 409 mtafute whatsapp
 
Pole sana mkuu I can feel you.
 
Nashukuru kwa experince. Mimi katika kuhangaika nimewapata watu wawili walio shuhudia walikua na kansa na wamepona
Mmoja alikatwa na ziwa kabisa

Mwingine yeye hata hospital hakufika, alipatiwa tu miti shamba.
 
Shukrani mkuu, lakin tumehangaika sana na CHEMOTHERAPY ila imeonekana kusaidia kwa kiasi kidogo sana na inaumiza sana aisee
 
Haya mambo yanachanganya sana mkuu, kuna mdada nimemuona amenishuhudia alipona kabisa, hospital aliambiwa ana kansa ya titi aanze matibabu akawa hana pesa, ikabidi akimbilie miti shamba.
 
Dawa ipo ni wewe tuu hujaamua kuitafuta...

"We are only limited by our imagination"
Mpaka kuandika hapa ndo kuamua kuitafuta mkuu. Nimejua hapa nitapata watu wengi wenye experience mbali mbali na hata wenye dawa.
 
Apumzike kwa amani Mama, hata matibabu ya india hayakusaidia, au alipata ahueni kwa miaka kadhaa
 
Sio juzi Wala Jana mkuu alifarik 2002 ni story ndefu na alichoma mionzi ocean road baadae akakatwa Titi sikia tu unajua mpaka funza walikua wanatoka..

Usimpe moyo hawezi kupona Cancer na Ina stages zake
Duuh aisee poleni sana. Experience inayoumiza sana kwakweli
 
Ahsante sana mkuu, hope kwa sasa anaendelea vizuri
 
Pole sana kwa mama mkwe.
Huyo aliyepona alitibiwa hospital au mbadala.
 
Kaka nimepambana sana kusoma message zako PM lakini nimeshindwa sijajua tatizo nini.... Naomba niandike apa hii no uwasiliane na uyu mtu 0657 163 409 mtafute whatsapp
Ahsante mkuu, nijieleze nimepewa namba na nani?

Ama naomba unitext 0756901102
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…