Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Pole sana ndugu yangu; niliuguza mama mkwe akiwa na saratani ya matiti mwishowe akatuacha. Ila kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike aliyeiwahi akapona na sasa hivi anaendelea na maisha kama kawaida. Inategemea sana saratani hiyo iligundulika ikiwa stage gani. Ninakuombea sana Mungu akupe faraja na itokee kuwa iligundulika katika stage za awali
 
Chief pole sana,Breast cancer ni moja cancer ngumu sana kupina ikivuka stage 1,lakini pia kuna zingine hata ukiiwahi stage 1 mgonjwa ataishi nayo mpaka itamuondoa. Usipoteze hela zako kutafuta tiba mbadala,waulize madaktari wako wakwambie ukweli,kama haiwezekani kupona.

Mara nyingi nchi za wenzetu ikifika level mbaya huwa Wana manage mgonjwa kwa dawa za maumivu ,maombi ,sala na toba . Ikubali hali halisi kisha anzeni kufanya maandalizi pamoja. Kuna bro wangu alifiwa na mkewe kwa cancer ya ziwa 2021 akiwa kwa mganga wa asili. Baada ya kuona hospital wameshindwa alimhamishia huko japo kwa ushauri wa madokta ilitakiwa arudi tu nyumbani.
Daah inasikitisha ila ndo hivyo inasaidia kujiandaa kisaikolojia
 
Kaka nimepambana sana kusoma message zako PM lakini nimeshindwa sijajua tatizo nini.... Naomba niandike apa hii no uwasiliane na uyu mtu 0657 163 409 mtafute whatsapp
 
Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Pole sana mkuu I can feel you.
 
Naelewa Mkuu kuwa unapitia changamoto kubwa lakini kwa experience yangu ya watu wa karibu waliopata kansa hakuna aliyepona.

Ila kilichowasaidia kuwa at least vizuri na kuongeza urefu wa maisha kiasi ni diet tu haswa kuepuka sukari

Pia kutumia sana juice ya carrot plain lakini na ya stafeli ambapo unachemsha majani yake lakini pia anakula tunda lake

Yote kwa yote bado naamini katika Mungu, yawezekana kwangu sikuona aliyepona au kuishi muda mrefu baada ya kupata cancer lakini kwako ikawa ni story tofauti.

Mungu akutie nguvu pia maana si kitu rahisi [emoji1431][emoji1431]
Nashukuru kwa experince. Mimi katika kuhangaika nimewapata watu wawili walio shuhudia walikua na kansa na wamepona
Mmoja alikatwa na ziwa kabisa

Mwingine yeye hata hospital hakufika, alipatiwa tu miti shamba.
 
Mkuu naona unamdanganya mgonjwa

Yaani cancer itibiwe na mitishamba?

Like really?

Tusidanganyane bwana

Hakuna useless tiba kama hizi za mitishamba,siku hizi zimepewa jina eti tiba mbadala,sio tiba mbadala ni miti shamba!

Ukijua definition ya cancer utajua directly tiba za mitishamba ni uongo mtupu!

Muache aende hospitali waue hizo cancerous cells usituletee uongo wa mitishamba bwana
Shukrani mkuu, lakin tumehangaika sana na CHEMOTHERAPY ila imeonekana kusaidia kwa kiasi kidogo sana na inaumiza sana aisee
 
Unamkumbuka Steve Jobs boss wa Apple? Cancer ya kongosho ilimuondoa. First time wameigundua akashauriwa operation pamoja na chemotherapy na ilikua anapona kabisa kwa sababu waliiwahi. Mzee aligoma akaenda fanya tiba mbadala za kihindi,hali ilipokua mbaya akarudi hospitali.

Madokta walimpambania mpaka akafanyiwa liver transplant,waliweza tu kumuongezea miaka michache ya kuishi. Kama ni tiba mbadala mtu asichane na tiba za hospitali,cancer sio wadudu ni seli za mwili zimekua immortal (hazifi). Unaziuaje kwa miti shamba pekee?
Haya mambo yanachanganya sana mkuu, kuna mdada nimemuona amenishuhudia alipona kabisa, hospital aliambiwa ana kansa ya titi aanze matibabu akawa hana pesa, ikabidi akimbilie miti shamba.
 
mama yangu pia amefariki kwa uo ugonjwa.. tumeenda mpaka india apollo akafanyiwa surgery na kuchomwa mionzi.

wahindi walituambia ukweli cancer ina tabia ya kurudi rudi. watu wa tiba asili kuwa nao makini sana ni wapigaji wanawaza kupata pesa zako tu huku wanajua uhalisia hawawezi kutibu.

epuka sana waganga wa kienyeji na watu wa tiba asili wanapenda sana kuvuna pesa za watu wenye shida za ki afya
Apumzike kwa amani Mama, hata matibabu ya india hayakusaidia, au alipata ahueni kwa miaka kadhaa
 
Sio juzi Wala Jana mkuu alifarik 2002 ni story ndefu na alichoma mionzi ocean road baadae akakatwa Titi sikia tu unajua mpaka funza walikua wanatoka..

Usimpe moyo hawezi kupona Cancer na Ina stages zake
Duuh aisee poleni sana. Experience inayoumiza sana kwakweli
 
Kama bado haijafika stage 3 Kuna uwezekano mkubwa Sana wa kuokoa maisha ya mkeo. Achana na chemotherapy. Kuna huu mti unaoitwa mtopetope au mstafeli.
Chukua majani yake, chemsha mpe anywe, Yani iwe ndio maji yake. Anywe hata Mara nne mpaka sita kwa siku, utaona hata nywele zitarudi kichwani baada ya muda mfupi.
Hii niliishuhudia kwa aliyekua na Kanda ya jicho, japo alichelewa kuanza kutumia dawa mpaka jicho moja likaondolewa, lkn baada ya muda nywele zilianza kuota na afya kwa ujumla ilirudi.
Please please jaribu hii dawa.
Let her drink like crazy majani ya huo mti.
Ahsante sana mkuu, hope kwa sasa anaendelea vizuri
 
Pole sana ndugu yangu; niliuguza mama mkwe akiwa na saratani ya matiti mwishowe akatuacha. Ila kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike aliyeiwahi akapona na sasa hivi anaendelea na maisha kama kawaida. Inategemea sana saratani hiyo iligundulika ikiwa stage gani. Ninakuombea sana Mungu akupe faraja na itokee kuwa iligundulika katika stage za awali
Pole sana kwa mama mkwe.
Huyo aliyepona alitibiwa hospital au mbadala.
 
Kaka nimepambana sana kusoma message zako PM lakini nimeshindwa sijajua tatizo nini.... Naomba niandike apa hii no uwasiliane na uyu mtu 0657 163 409 mtafute whatsapp
Ahsante mkuu, nijieleze nimepewa namba na nani?

Ama naomba unitext 0756901102
 
Back
Top Bottom