Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Wewe ni muongo.

Ukipata saratani ya kizazi/uke hakuna matibabu. Huwezi kupona. Lazima ufe.
 
kama unatiba mbadala msaidie hayo maneno huwa yanasemwa baada ya mgonjwa kupona hapo unazidi kumchanganya mwenzio ukweli umekosea...ila nawewe huenda sio kosa lako labda upo tungi.
 
Mkuu BICHWA KOMWE - hujamtendea haki mleta mada. Inawezekana hujaelewa madhara ya kauli yako. Umesamehewa.

Jamaa ameshirikisha nzengo changamoto anazopitia kuhusu afya ya mke wake. Akaenda mbali Zaidi akasema Ushauri wowote anapokea. Umeshindwa nini kumpatia Ushauri kama alivyoomba?

Hakuna mkamilifu. Jifunze kuelewa hisia za wenzako.
 
Manjano mbichi
Komamanga
Kitunguu swaumu
Tangawizi
Visikosekane kwenye mlo wa kila siku.
. Tuachane na machai yenye sukari,maubwaubwa, machapati,machipsi,vitumbua,maandazi, bagia na masembe..
 
Pole sana brother na Mungu akutie nguvu, niliwahi kusikia sehemu kuwa tunda la stafeli lina msaada mkubwa sana kwa wagonjwa wa saratani.
Majani yake achemshe anywe pia kuna Yale majani ya :mhadalati' naruhusu kurekebishwa spelling atwange achuje anywe, mkuu mfa.maji haachi kutapatapa jaribu huenda Mungu anaweza kushusha Shani yake, poleni mgonjwa na wewe muuguzaji Mungu azidi kukupa nguvu
 
Yasemekana mitaani huko Dawa inayoponya donda ndugu yaweza ponya kansa. Ila sasa sio kwa kila stge ya kansa
 
Mkuu pole sana hebu kajiunge hili group kisha omba protocol ya tiba ipi itamfaa kisha tumia me nlijiunga kwenye group hili baada ya kupoteza mzazi kwa cancer ningelijua mapema ningempa hizi dawa wanazotumia jamaa usichelewe
 
 
Huyu jamaa yupo kwenye list ya watu niliowaignore michango yao siioni ila mkimquote naona fulani uliyemuignore. Mara nyingi nagundua niko sahihi kuwaignore baadhi wa wapuuzi ninapokuta watu mnajibizana nao kutokana na upuuzi wanaoandika.

Wapuuzi ni wengi sana na kila ninapofakiwa kuwatambua mapema huwa natembeza ignore.
 
Ila kuna watu wamepitia nyakati ngumu sana. Sote tunajua tutakufa siku moja ila kuna wenzetu ndio kama hivi anajua kabisa mke wangu atafariki miezi fulani. Imagine maumivu yake.

Kaka nimechelewa kuona huu uzi ila shukuru kwa kila jambo. Naamini shemeji alipata wakati mwingi zaidi wa kuongea na Mungu na ametangulia akiwa msafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…