Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Pole sana mkuu, aisee kansa sio poa. Tupende na tutunze afya zetu jamani.
 
CHEMOTHERAPY haiwezi kukuponya KANSA, inakuongezea KANSA. Ni kama unajibanika kwenye TANURU LA MOTO.

Achana na CHEMOTHERAPY, angalia chakula chake cha kila siku ni chakula gani?

Kama una akili timamu, ungelima hapo bustani upande mchicha mwingi ambao hauna MAKEMIKALI, pamoja na KAROTI, hiyo iwe FIRST AID yake.

MAUCHAFU kwenye damu yake pia, SUMUU, UTANDO, MUCUS, afanye namna ya kuondoa yote hayo. DAMU CHAFU.

PAMBANA SANA, ATAPONA KAMA UNA AKILI TIMAMU.

Ukiendelea na MAKEMIKALI na hizo CHEMOTHERAPY utamuangamiza.
Akitumia alkaline foods atapona maana saratani inapenda acidic environment.
 
Naelewa Mkuu kuwa unapitia changamoto kubwa lakini kwa experience yangu ya watu wa karibu waliopata kansa hakuna aliyepona.

Ila kilichowasaidia kuwa at least vizuri na kuongeza urefu wa maisha kiasi ni diet tu haswa kuepuka sukari

Pia kutumia sana juice ya carrot plain lakini na ya stafeli ambapo unachemsha majani yake lakini pia anakula tunda lake

Yote kwa yote bado naamini katika Mungu, yawezekana kwangu sikuona aliyepona au kuishi muda mrefu baada ya kupata cancer lakini kwako ikawa ni story tofauti.

Mungu akutie nguvu pia maana si kitu rahisi 🙏🏽🙏🏽
 
Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Pole sana

Ni maombi yetu kwa Mungu amponye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kihangaikia maisha,kila aina ya kinalowezekana,lazima. Nadhani hata walioleta hiyo mionzi,wanajua ina msaada japo kidogo.
Mtoa mada amesema(kama sikosei ni yeye),kwamba ni titi la karibu na moyo,kama alihofia hiyo mionzi itaathiri moyo. Nadhani wanaoitumia wanajua cha kufanya, kwa hiyo asiache kumpeleka.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Uchawi is real.

Kwamba asisite kumpeleka kwenye TANURU LA MIONZI licha ya kwamba AMESHAUNGUZWA VYA KUTOSHA!!

Asisite aende tena na tena 😂😂😂😂🙈🙈🙈
 
Ukitaka kujua uzito wa dunia basi vaa viatu vya huyu mleta mada,

Nikupongeze kwa kutomkimbia mkeo kwa dunia ya leo unahitaji tuzo ya kipekee, kuna wanaume humu huwa wanadhihaki nyonyo ndala sasa wako amekatwa na bado unamthamini hivi,

Niliwahi kuona mkaka jirani na nilipokuwa alikuwa na kansa ya koo😭 mwaka juzi, amefariki mwaka jana, yule kaka alikuwa anatoa machozi ya damu yani maji ya machoni ilikuwa ni damu, kwa macho yangu nilikuwa naogopa hata kumtizama, inatisha nyie, tujidao tu ila ukiona u mzima unatembea unaringa ni kwa neema tu, kiukweli sijawahi ku experience hii kitu kusema nina msaada ila majani ya mstafeli kama walivyoandika wadau wengine nasikia yanasaidia kuna kipindi nilikuwa namtengenezea mzee home (kumkinga na tezi dume)tena ngoja nimkumbushe,

Msalimie mgonjwa na pole kwa kuuguza Mungu awatie faraja na kuwafanyia wepesi katika nyakati hizi ngumu
Kila mtu kwa zamu yake na kila mtu atapatilizwa kwa namna yake. Kuna msemo siku hizi nimeanza kuuelewa, "tuombeane mwisho mwema"!
Pole sana kwa muuguzi na pole nyingi sana kwa mgonjwa, ni kipindi kigumu nadhani kuliko vyote katika maisha yetu.
 
Alkaline food ni zipi uizo ?

Acidic food ni zipi hizo na mifano ?

Asante

Alkaline Foods​

  • Most fruits
  • Non-starchy vegetables like dark, leafy greens
  • Sea vegetables (kelp, seaweed, dulse)
  • Soy
  • Beans/Legumes
  • Potatoes
  • Avocados
  • Sprouts (soy, alfalfa, bean)
  • Cucumber
  • Broccoli
  • Himalayan salt
  • Nuts
  • Quinoa
  • Millet
  • Parsley
  • Seeds
  • Olive oil
  • Coconut oil
  • Almond milk

Acidic Foods​

  • Cheese
  • Meat, especially processed meat
  • Seafood
  • Brown rice
  • Yeast
  • Mushrooms
  • Carbonated beverages such as soda and seltzer
  • Coffee and caffeinated drinks
  • Protein supplements
  • Refined sugars
  • Salty foods
  • Eggs
  • Alcohol
  • Processed foods
 
CHEMOTHERAPY haiwezi kukuponya KANSA, inakuongezea KANSA. Ni kama unajibanika kwenye TANURU LA MOTO.

Achana na CHEMOTHERAPY, angalia chakula chake cha kila siku ni chakula gani?

Kama una akili timamu, ungelima hapo bustani upande mchicha mwingi ambao hauna MAKEMIKALI, pamoja na KAROTI, hiyo iwe FIRST AID yake.

MAUCHAFU kwenye damu yake pia, SUMUU, UTANDO, MUCUS, afanye namna ya kuondoa yote hayo. DAMU CHAFU.

PAMBANA SANA, ATAPONA KAMA UNA AKILI TIMAMU.

Ukiendelea na MAKEMIKALI na hizo CHEMOTHERAPY utamuangamiza.
Mkuu naona unamdanganya mgonjwa

Yaani cancer itibiwe na mitishamba?

Like really?

Tusidanganyane bwana

Hakuna useless tiba kama hizi za mitishamba,siku hizi zimepewa jina eti tiba mbadala,sio tiba mbadala ni miti shamba!

Ukijua definition ya cancer utajua directly tiba za mitishamba ni uongo mtupu!

Muache aende hospitali waue hizo cancerous cells usituletee uongo wa mitishamba bwana
 
Mkuu naona unamdanganya mgonjwa

Yaani cancer itibiwe na mitishamba?

Like really?

Tusidanganyane bwana

Hakuna useless tiba kama hizi za mitishamba,siku hizi zimepewa jina eti tiba mbadala,sio tiba mbadala ni miti shamba!

Ukijua definition ya cancer utajua directly tiba za mitishamba ni uongo mtupu!

Muache aende hospitali waue hizo cancerous cells usituletee uongo wa mitishamba bwana
Jamaa unazingua Sana, binafsi nawafahamu wagonjwa wa cancer waliopona. Nina mtu alienda south Africa kutafta Tina alifeli ,saizi yupo mtAani kApona
 
Back
Top Bottom