Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kansela wa Austria Sebastian Kurz amesema anapanga kujiuzulu kutokana na shinikizo la tuhuma za ubadhirifu, na nafasi yake itajazwa na waziri wa mambo ya nje.
Kurz amekuwa akikabiliwa na tuhuma kwamba chama anachokiongoza kilitumia fedha za serikali kujiunufaisha na fadhila ya vyombo vya habari.
Baada ya kukaidi miito ya kumtaka ajiuzulu, hatimaye Jumamosi usiku alisalimu amri, na kutangaza kuwa anajiengua madarakani kutokana na shutuma hizo kwamba ofisi yake ilivuja fedha za umma.
Kurz amesema ataingia bungeni kama kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Austrian People's Party (ÖVP), na kwamba waziri wa mambo ya nje, Alexander Schallenberg atajaza nafasi yake kama kansela.
''Nchi yangu ni muhimu kwangu kuliko mimi,'' amesema Kurz katika hotuba yake kwa njia ya televisheni.