#Kanumba , umekufa bro na bongo muvi imekufa, siku hizi sio talent tena ni uzuri wa sura na umbo ndio unaamua nani aigize. umaarufu unaotokana na talent uliondoka nao wewe, umetuachia maceleb wa scandals za kujiuza, ushoga na kusagana.Kufa kufaana, badala ya kukuenzi watu wanapiga hela kwa matamasha na viingilio kwa hekaya za kukuenzi.
bro, wewe ulikuwa mwigizaji na mwanamuziki kwa kipaji na uwezo, ila siku hizi kila mwigizaji nae amekuwa mwanamziki wa kukata viuno na kuacha maungo wazi, wakifungiwa kazi zao na basata wanasema wanabaniwa! Sikumbuki kazi yako yoyote kufungiwa ila huku kuna utitiri wa kazi zilizopigwa kufuli.
Bro wakati wewe ulisimamia uhuru wa fikra na mawazo faafu, ukasoma hata falsafa za great thinkers wengine na kuzitumia katika kazi zako, huku sasa hivi kila mtu ni script writer, wanaandika ukasuku tu hakuna jipya zaidi ya uliyoyaacha ambayo yameendelea kuwa mapya kila siku kwa ubora wake kuliko haya mapya yasiyo mapya yanayoandikwa sasa.
umetuachia wanasiasa bongo muvi, unashanga?usishangae , wameweka rehani dhamana ya dhima ya usanii wao katika kukosoa wale wafuja jasho letu na hatimae wameungana nao kutufuja!!inasikitisha! tena kwa gharama ndogo ya ahadi hewa na pesa za kijungu jiko.
Wakati director ni fani na uwezo kikazi, siku hizi kuna madirector wengi kuliko waigizaji na kila mmoja ana kampuni tena nyingine zinaendeshwa kwa ruzuku ya kugawa vipochi manyonya.
Yako mengi sana huku ila kwa leo niishie hapa.Pumzika!