Kwa mtizamo wangu sioni tatizo kwani yeye ni mwanadamu huru na ana uhuru wa kuchagua apendacho..
Ila sasa akumbuke kuwa njia hiyo haipo kwenye orodha ya njia za kiasili za kupata
mtoto/kutunga mimba. Wengi wanaitumia kama njia ya mwisho baada ya juhudi za kawaida/asili kugonga mwamba. Kama yeye ni mzima na juhudi za kawaida hazijagonga mwamba basi yeye kufanya hivyo ni kama kumdhihaki Mungu. Vitabu vinatuambia "..miili yetu ni mahekalu.." kumaanisha kuwa miili yetu ina thamani yake na hatuna ruhusa "kuichezea" tupendavyo labda kama kuna shida ya kweli.
Nawasilisha.