Kanumba ndani ya Big Brother House 2009


Maane, tatizo ambalo baadhi yetu tumejaribu kujadili (mfuatilie FP) siyo lugha! Tujikite kwanza kwenye uelewa. Kama mtu anaelewa mada basi anaweza kujadili hata kama lugha yake haijanyooka. Kwa kiwango cha form 6, tunategemea aweze kuelewa angalau vitu vya kawaida kwenye maongezi/majadiliano! Kama hawezi kujua tofauti ya temptation na meditation basi tatizo ni kubwa. Lakini kama anajua basi atajaribu kujieleza hata kwa broken ili msikilizaji amwelewe. Mbona Maximo tunamwelewa?

Labda tuanze hivi; je, kiswahili chenyewe tunakijua?
 

Nimeelezea mpaka nimechoka. Nadhani watu wakikuta Thread katikati hawaanzi kusoma toka mwanzo, hivyo inaharibu mtiririko wa hoja.

Asante Darkcity
 
Huko kutokujua kwake kiingereza mi sioni ajabu,wapo watu kibao wana graduate still kinawapiga vyenga,mimi ninachotaka kuongea kuhusu huyu bwa mdogo ni kwamba he has to be confident na chochote anachofanya pale mjengoni,asiogope mjengo wala vilivyomo,kuhusu lugha anaunga unga tuu hamna mbaya,kama akiona mambo magumu afanye mpango vibweka vyovyote vile(positive)ambavyo vitainua status yake!!
 


Mwingine huyu kadandia treni kwa mbele!!!!

Kanumba kashatoka na alitakiwa kukaa humo masaa 24 tu.

Mzee unakera, kuingilia mjadala bila kujua kinachojadiliwa. Watu wa aina yako WANABOA sana.
 
Nakubali kuwa Kiingereza ni janga la Kitaifa, lakini Kiingereza kilichomo kwenye hiyo globu, hasa pale kwenye biograph, kinaweza kusababisha mtu upatwe na kizunguzungu ghafla

Hilo ndo nililokuambia toka siku ile. Ukiona mtu hata kingereza cha kuandika kinamsumbua basi kuongea ni tabu tupu. Ndo maana sikuwa kwenye upande wa kumlaumu, bali kum-encourage ili apate moyo wa kuongeza kitu. Jamaa anaweza ku-improve, lakini si yeye tu bali pia anawa-inspire vijana wengine. ninatumaini tutakuja kupata wasanii wazuri na wenye uwezo zaidi. Roma haikujengwa siku moja.
 
Nasikia jamaa atawasili leo saa 6:00PM, na ameandaliwa mapokezi makubwa.
 
Nakubali kuwa Kiingereza ni janga la Kitaifa, lakini Kiingereza kilichomo kwenye hiyo globu, hasa pale kwenye biograph, kinaweza kusababisha mtu upatwe na kizunguzungu ghafla

Ndiyo hatujui Kiingereza, kwani hilo ni tatizo kubwa? Kwani ni sisi peke yetu tusiojua kiingereza? Kwangu hilo siyo suala la kuumiza kichwa. Naumia pale ambapo natakiwa kuwa na nondo (uwezo) wa kujieleza na kuchangia mada lakini nashindwa. Kwa hiyo napwaya. Lakini baya zaidi ni upumbavu wa kubandika mambo (to the public) katika lugha ambayo hujui vizuri. Kwani anashindwa nini kumwomba mshikaji akamsaidia kusoma na kunyoosha lugha? Mbona wapo vijana wengi sasa hivi (toka shule zetu za St...) wanajua lugha vizuri? Kwangu mimi hicho ndicho kiini cha tatizo. Kujizungusha uchi mtaani wakati unao ndugu kibao wanaoweza kukuazima (hata kukupa bure) suti!
 
Kanumba alienda kama guest celebrity lakini si one of the participants ambao wataishi ndani ya big brother house. Kwa kweli amevunja mayai mengi alivyokua anaongea, lakini nilipenda alivyojitahidi kutoa ushauri kwa mates, kwamba hata kama wakisurvive kwa siku chache zinatosha kwa wao kutoka kwenye nchi zao, aliongea point ya maana sana pale hata kama lugha haikunyooka-alieleweka.

Hongera Mwana wa Tanzania Kanumba.
 


Huwezi kuwa na confidence kama huna nondo. Kwa wale waliopitia shule, neno confo (confidence) lilikuwa maarufu sana kumaanisha kuwa mambo yanapanda. Kama hayapandi hata siku moja hakuna confo. Ila ukiwa mjanja (ambapo wengi wetu ni wajinga) unaweza kuwatumia watu wenye nondo zao kujijenga. Dunia nzima inafanya hivyo na ndiyo maana kuwa wataalamu wenye fani zao; na wanapata pesa nzuri kwa kuwafanyia kazi watu wenye vipaji lakini ufahamu kiduchu au wanahitaji huduma ambayo hawawezi kujipatia wenyewe!
 

Huwezi kuona ajabu maana hata wewe mwenyewe hakipandi na hujaona umuhimu wake. Ukweli ni kwamba kiingereza kina nafasi yake sana ktk dunia ya sasa kwa hao wanaotaka kujihusisha na mambo hayo ya performance pamoja na wengine ambao wanahitaji kuingia ktk international settings. Acha kujiridhisha kwa hisia,tafuta facts,period!
 



the problem is that some people are dying with envy, mtakubali tu lugha kitu gani what matters is what you are doin in the building.kama pumba utamwagwa na kama mchele atachukua dola.
 
hii biography ya KANUMBA,mtu yoyote akiisoma anam dismiss on the spot,Kanumba ni star lakini kwa maelezo/lugha hiyo pulizzzzz god help us.Mimi naona INVISIBLE jitahidi kuwasaidia hawa vijana,hizi biography zao kupitia kwako tunaweza wachongea vitu vyenye uhakika after all tusiposaidiana watanzania nani atatusaidia.NAWAKILISHA
 
mwacheni kanumba wa watu jamani..atia huruma sana..maana clouds wanavyomsakama..duu..pole zake..na yeye akasoma kidogo sasa..maana ana pesa ya kujisomesha..
 
Lugha ni tatizo. Alifahamu toka hajaondoka kuwa kule ni kithungu tu, angewagomea kwa maelezo kuwa anakwenda British councel kujinoa. Afadhari angeenda Monalisa, si mlimwona kwenye SHE IS MY SISTER?

Pamoja hayo, angalau huyu amejaribu. Jamani mmeshawahi kusikia kiingereza cha Ray, Johari, Richie, Da kiboga a.k.a Asha ngedere, JB n.k? Hivi Ray ameshawahi kuigiza na Wanaijeria?
 

Kichuguu,
Nafikiri zote zinaweza kuwa sawa kutokana na wilaya uliyopo. Unafahamu neno hivyohivyo kwa Sikonge tunasema "Vyenivyo", Usoke wanasema "fyenifyo", Wasukuma wanasema "shenisho".
Hii nimeiona kibahati kwani nilishapoteza hamu ya kufuatilia hizi BB programs. Sijui kwa nini hata kusoma huwa ni mvivu sana.

Huyu kijana wetu Manumba (Majumba) kwa kweli inabidi akaze buti. Ningelimshauri aende shule intensive course kama miezi sita. Ajifungie na ajifue kwa nguvu hasa. Dada yangu aliyekuwa darasa la saba, alifanya hiyo course pale Dar na sasa ni "mwalimu International School". Celine Dion alikuwa hajui Kiingereza kabisa, alijichimbia kama miaka 2, alipotoka na kuimba "Beauty And The Beast" ambao kama hukumfahamu mapema, huwezi amini kuwa ni Francophone.
Kijana Kanumba, usikate tamaa, wewe ongeza mwendo. Kufahamu lugha ni muhimu sana kwa watu kama nyie. Forrest Whitaker alijifunza Kiswahili kwenye film ya Idd Amini. Jitahidi ujifunze Kiingereza na Kifaransa na ukiweza ongeza hadi Ki-Spain. Katika kazi yako ni muhimu sana na hasa kama unataka kupanua msuli wako hadi nje ya Tanzania (why not?)
 
Waliosema kiingereza ni janga la Taifa hawajakosea imefika wakati elimu kuanzia primari iwe kwa kiingereza mahausigeli na mama mboga wa Malawi,Zambia,Kenya na Uganda wanaongea kiingereza kizuri kushinda Kanumba.Wakina Kanumba ni wengi tukubali kiswahili 'will take us nowhere' na tutaishia kuogopa soko huru la ajira kwakuwa hatuko 'competetive'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…