Nyamwage
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 712
- 1,748
Gari ya kutoka T/chang'ombe kwenda Makumbusho iliingia Makumbusho stendi na abiria wakiwa level seat lakini hakuna abiria alieshuka ikimaanisha kuwa hao abiria wamegeuka na gari ili wasisimame wamelipa nauli ya go and return abiria tuliokuepo stendi tukapanda tukasimama chuma ikaamsha.
Tumefika Mwananyamala kuna dada kapanda na mtoto wake kama wa miaka miwili akitarajia kuwa atapishwa seat akae lakini wapi abiria wamegeuzia shingo pembeni wanaangalia nje.
Kaona kama vile abiria hawajamuona ili wampishe akae sijui alimfanya nini mtoto wake sijui alimfinya maana mtoto aliangua kilio cha ghafla tu lakini wapi abiria wamekaza hawakujali chochote.
Tumeendelea na safari chuma kimefika Buguruni abiria wakashuka wengi tu karibia wote gari lika baki na seat kibao mzee mmoja kamwambia binti kaa umbembeleze mwanao maana safari ya huyo dada bado ilikuwa inaendelea dada kugoma kukaa bwana kasema eti sina shida ya kukaa.