Kanuna eti kisa hajapishwa siti ya daladala akae na mwanae

Ifike mahali Waziri mwenye dhamana ya usafirishaji atangaze kuwepo na seat maalumu kwenye kila daladala ambayo siti hizo watakaa wanawake wajawazito, au walemavu, wazee na wenye watoto. mtu mwingine ataruhusiwa kukalia siti hizo ikiwa tu hakuna katika hao. Vinginevyo tunawatesa hawa akina mama wenye watoto kwa sababu wao hawajageuza na gari, ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kulipia nauli mara 2 kwa safari moja?

Watanzania tuache roho mbaya jamani, ni kweli umegeuza na gari na umelipia mara mbili lakini isiwe ndio sababu ya kuacha kusaidia wenye matatizo. Hawa watoto tutawafanya wakue na tabia za chuki na roho mbaya kwa sababu ya sisi tuliowafanyia roho mbaya wakati wakiwa wadogo. Mimi afya sio nzuri lakini nikiwa kwenye daladala akaingia mwenye mtoto, au mjamzito au mzee nampisha hata kama nimegeuza. Huwa nafurahi napomsaidia mtu barabarani
 
πŸ˜…πŸ˜…

I miss you twin
Mmekumiss pia twin. 😍

Ila Umenifanya nicheke mana mie mwenyewe nipo kwenye daladala hapa nimeshikilia bomba. Teh teh 😜

I hope uko mzima?
 
Huyo mzee aache unafiki.
Angekuwa mwema angempisha
 
Yan serikali inayotumia kichwa used cha SGR ianze kudeal na daladala,mpe kaisar yalo yake
 
vitu vinavyokosesha utulivu ukiwa ndani ya dala dala.

kukaa seat moja na wachuuzi wa vitunguu,nyama au samaki wabichi.

kuketi ktk seat wakati kuna mama kasimama akiwa kabeba mtoto amekugeukia anakutizama.

konda kubaki na chenji yako.

kukaa na muongeaji wa simu muda mrefu na ananuka mdomo.

dah jaman tuombeane kununua magari aisee,mji mgumu sana huu.
 
Story yako inafanana na nilichotaka kusimulia. Ilikuwa hivyo hivyo, dada kaacha gari kibao zinapakia akasimama kando yangu na mtoto, halafu gari ilipoondoka akaniambia ''Kakaa naomba unisaidie huyu mtoto''. Tofauti na wewe mimi nilimpa makavu na nikamwambia sitaki. Nikamwosha yale magari tuliyoacha nikamwambia kwa nini asipande?
 
Ni kweli vinakera wengi. Na pia mtu mwenye flu kali, au mtu mchafu kupitiliza ananuka majasho. Bila kusahau hawa vijana malimbukeni wanaobeba vibegi vya mgongoni kama gamba la kobe, huku wanageuka na kugonga navyo abiria wengine.
 
Hahahaha mkuu utaniua kwa kucheka
 
Mmekumiss pia twin. 😍

Ila Umenifanya nicheke mana mie mwenyewe nipo kwenye daladala hapa nimeshikilia bomba. Teh teh 😜

I hope uko mzima?
Mie niko poa,habari za uzima?
 
πŸ˜…πŸ˜‚ mimi sikuhiz sipishi ng'ombe yoyote seat, yaaan labda uwe na mguu mmoja... Mjamzito Mzee Mlemavu wa kawaida tu au Mama mwenye mtoto I don't care utasimama mbele yangu mwanzo wa kituo hadi mwsho wa safar na sipepesi macho pembeni
Kuwa na adabu hata kama hautaki kumpisha mtu lakini kitendo cha kumuita abiria mwenzako ng'ombe kinaonesha upumbavu wako na kukosa adabu, kuwa memba JF si ujanja.
 
sawa Elvis *****.... hata wew na mimba yako hiyo siwez kukuachia seat... Ng'ombe jike wew
Kuwa na adabu hata kama hautaki kumpisha mtu lakini kitendo cha kumuita abiria mwenzako ng'ombe kinaonesha upumbavu wako na kukosa adabu, kuwa memba JF si ujanja.
 
Kwanza haya mambo yakupishana seat kwa vigezo fulani fulani yanaanzaje kwani mtu si ameona gari imejaa na akapanda akijua atasimama tu,
 
siku hiyo gerezani pale tuligombania kibombadia mwendokasi aisee tumejazana wacha aingie mdada ana uja uzito eti anataka apishwee... πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ watu walimshambulia akashuka kwenda kupanda zile za kawaida
 
[emoji28][emoji23] mimi sikuhiz sipishi ng'ombe yoyote seat, yaaan labda uwe na mguu mmoja... Mjamzito Mzee Mlemavu wa kawaida tu au Mama mwenye mtoto I don't care utasimama mbele yangu mwanzo wa kituo hadi mwsho wa safar na sipepesi macho pembeni
Unapanda daladala na ng'ombe? Wapi huko ng'ombe mnapanda nao daladala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…