Kanuni kumi za ndoa

KakaNanii

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2008
Posts
325
Reaction score
52
1)KANUNI YA NENO LA KUPENDEZA
Usipitishe siku nzima bila kutamka neno la kupendeza na la kukumbukwa na mwenzio.
2)KANUNI YA NENO "NIMEFURAHI KUKUONA"
Usikutane na mwenzio bila kumkaribisha kwa kauli ya upendo
3)KANUNI YA KUTAWALA HASIRA
Usiwe mwepesi wa kukasirika
4)KANUNI YA KUDHIBITI ULIMI
Usiongee kwa sauti kubwa na mwenzio
5)KANUNI YA UWAJIBIKAJI
Usiruhusu swali lirudiwe
6)KANUNI YA UTII
Wapenzi wawili mko sawa. Ni mameneja wawili ambao kila mmoja ana majukumu yake.
7)KANUNI YA UKARIMU
Usifanye jambo kwa gharama za wengine
8)KANUNI YA KUZIKA MAKOSA
Usifufue makosa labda kama yanajirudia mara kwa mara.
9)KANUNI YA USAFI WA MAMBO
Siri ya furaha iko kwenye kusahau yaliyopita na kuanza kila siku na mambo safi
10)KANUNI YA MUUNGANO WA THAMANI
Muda wote ukiwa na nafasi kaa na mwezi wako.
 
Naomba nikuulize umeoa/umeolewa?? Maana hizi thread zako zina utata sana mkuu. Samahani kama nimekukwaza
 
Asante sana,mawazo mazuri........:clap2:
 
KakaNanii,
Uzikariri vizuri hizi kanuni, utazihitaji siku ukioa au ukiolewa.
Hizi ni za vitabuni, za katika maisha halisi unaweza kuzimia..ndio maana ninakusisitiza uzikariri vizuri zitakusaidia sana.
Siku hizi ndoa nyingi ni "vita", kama ni mtu wa dini, ndoa zinageuka"jehanamu". Nikisema nyingi maana yake sio zote. Pengine hizo chache wanatumia hizi kanuni ulizoziorodhesha hapa.

Ndoa...ndoana....wengine hupata vidonda vya tumbo kwa maudhi ndani ya ndoa...
Ndoa nyengine ni sawa na kuangalia kanda za video,filamu....raha tupu.
 
kuna kanuni mbili tu jamani, nazo zimeegemea kwenye upendo kwani upendo ndio utimilifu wa sheria. kanuni hizo ni hizi:

1. mpende Mungu wako kwa moyo wako wote kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote, na
2. wapende wote wa nyumbani mwako (akiwemo mumeo/mkeo/watoto nk.) kama unavyojipenda mwenyewe

hapo utakuwa umetimiza kila kanuni, zilizokwishatungwa na zitakazotungwa. glory to God
 

Miss umenena. hizi units 2 tu lakini zinatushinda. asante kwa kutukumbusha.
 
hii nzuri sana my dear..

lakini ukifuata amri kumi za Mungu ..
u will never go wrong ..lol
 
Dah!!! Mmesahau kanuni moja nayo ni Serengeti na Tusker ya baridi
 
Inawezekana unayosema ni kweli lakini application yake mmmh, mi naona hayo ni rahisi zaidi mkiwa wachumba au kwa ndoa ya mkataba kama ipo, lakini ile ya kudumu kabisa mpaka kifo kitutenganishe sidhani.....
 
Inawezekana unayosema ni kweli lakini application yake mmmh, mi naona hayo ni rahisi zaidi mkiwa wachumba au kwa ndoa ya mkataba kama ipo, lakini ile ya kudumu kabisa mpaka kifo kitutenganishe sidhani.....

Kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…