RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Kuna watu wakienda sokoni wanajikuta wananunua bidhaa nyingine (nyingi) ambazo hawakupanga kununua, hayo ni matumizi mabaya ya pesa. Zifuatazo ni kanuni kuu mbili za kwenda kununua bidhaa sokoni.
(1). IFAHAMU VIZURI BIDHAA UNAYOKWENDA KUNUNUA SOKONI:
Usiende sokoni kichwa kichwa, utapigwa. Kwanza ifahamu vizuri bidhaa unayotaka kununua, pia ubora wake, gharama yake, na eneo maalum inapopatikana (kwa ujumla hakikisha una taarifa kadhaa kuhusu bidhaa). Kama unahitaji kununua bidhaa nyingi andaa orodha. Itakusaidia kuzingatia lengo lako la ununuzi.
(2). EPUKA KWENDA SOKONI NA HELA NYINGI:
Usiende sokoni na hela nyingi kupita gharama ya bidhaa unayokwenda kununua. Kwa mfano, kama ulipanga kununua simu ya shilingi laki tano (TZS 500,000) kamwe usibebe shilingi milioni mbili (TZS 2,000,000) kwenda nazo sokoni. Kwasababu utanunua bidhaa nyingine ambazo hukupanga kununua. Baadae utagundua kuwa bidhaa nyingine ulizonunua hazina umuhimu wowote kwako.
RIGHT MARKER
Dar es salaam.