Kanuni ya masaa 72 timu kucheza mechi haiswihi kwa Tanzania

Kanuni ya masaa 72 timu kucheza mechi haiswihi kwa Tanzania

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nchi yetu ni kubwa sana na timu zimetawanyika sana kwenye mikoa, wilaya, tarafa, kata hata kwenye vijiji. Viwanja vyetu vingi havina dimba nzuri la kuchezea hivyo linazalisha ajali nyingi zisizozuilika kwa wachezaji.

Wachezaji wetu wengi hawakutokea kwenye sports academies hivyo wanarukiana tu bila kujali afya za wenzao na kuzalisha majeraha mengi kwa wachezaji.

Baadhi ya barabara za kwenda na kutoka kwenye mikoa, mechi zitakakochezwa ni ndefu na zina mashimo na matuta mengi, baadhi ya viwanja viko kwenye maeneo ambayo hakuna usafiri wa ndege, timu nyingi hazina fedha za kusafirisha timu kwa ndege.

Timu zetu na hospitali zetu hazina matibabu mazuri kwa wachezaji. na wachezaji wetu hawapati vyakula vizuri vya kuponyesha mwili haraka. Hivyo ndani ya masaa 72 mchezaji atakuwa hayuko fit 100% kumudu kucheza mechi nyingine.

Kanuzi ya TFF/Bodi ya Ligi, CAF na FIFA kupangia timu kucheza mechi kuazia masaa 72 baada ya mechi iliyopita inaziathiri timu nyingi kwenye ligi zetu Tanzania, hasa timu ndogo ambazo hazina vikosi vipana kutokana na hali ya uchumi wao.

Timu kucheza baada ya masaa 72 tu kunalazimisha wachezaji kucheza wakiwa na uchovu mwingi, majeraha, kukosa baadhi ya wachezaji muhimu na timu kufanya vibaya.

Mazingira yetu (jeografia, ubora wa viwanja, aina ya wachezaji na makuzi yao, huduma za afya, usafiri, uchumi na vyakula vya wachezaji) hayaruhusu utekelezwaji wa kanuni hii ya masaa 72, hivyo tusiwe kama dodoki au kasuku wa kutekeleza kila kanuni bila kuangalia hali yetu.

Yaani we have to think globally and act locally kwa kuzingatia hali yetu sisi Tanzania.
 
Wakati kanuni hii inatungwa walioitunga na kuipitisha bila shaka ni wazungu kutoka Ulaya ambako Wana vinchi vidogo, viwanja vizuri, uchumi mkubwa, matibabu safi, usafiri mzuri na miundombinu yote ya sporting iliyokamilika. Kama walikuwemo waafrika pia basi ama waliotoka Afrika kaskazini TU au wlikuwa mazuzu wa kutoka kusini mwa jangwa la Sahara, waoga, wenye njaa na wasioifahamu vyema lugha iliyokuwa inatumika kwenye majadiliano. Pamoja na hayo viongozi wetu wa mpira walnatakiwa kulingana na mazingira yetu watende kwa kuzingatia hali yetu badala ya kuzingatia kanuni TU inasemaje,

Kutekeleza kanuni kama hizi kunasaidia ligi kutoa washindi ambo hawezi kushindana kwenye mashindano ambayo sio ya TFF. Yaani tunapata false winners. Kwakutumia uchovu wa wachezaji prisons wataifunga Simba sio kwa ubora wao bali uchovu wa wachezaji wa Simba na tabia ya prisons ya kucheza kwa nguvu bila kujali afya za wachezaji wenye kwenye kiwanja kibovu ambacho mchezaji hawezi ku slide Wala kufanya tackling bila kujiumiza kwanza.
 
Back
Top Bottom