Kanuni ya Nguvu ya Umakini/Focus (Kanuni za Ulimwengu na Akili)

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,920
Reaction score
3,240

Huu ni muendelezo wa Taratibu na Sheria za akili na ufahamu.

Akili ya mwanadamu ni sehemu ambayo watafiti wengi wamekuwa wakihamasika kuielewa. Akili ni sehemu pana sana kwa mwanadamu. Ni sehemu ambayo haionekani wala haishikiki lakini ina matokeo makubwa sana kwa mwanadamu. Akili imezaa vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu, mawazo, imani, misimamo n.k. Kama unapenda sana kujifunza na kufahamu mengi lazima utakuwa unatamani kufahamu siri kuu za akili. Kuelewa siri kuu za akili ni kufahamu Sheria ambazo zinaiongoza akili. Katika mada hii utapata kuona mwanga kuhusiana na akili na kuweza kujifahamu vyema.

SHERIA/KANUNI HIZO NI:

  1. Sheria ya Chanzo na Matokeo
  2. Sheria ya Uhuru wa Kufikiria
  3. Sheria ya Umakini/focus
  4. Sheria ya Mawazo
  5. Sheria ya Ubinafsi
  6. Sheria ya Uumbaji
  7. Sheria ya Hisia
  8. Sheria ya Ubadili
  9. Sheria ya Usawa wa Akili
  10. Sheria ya Kutokea.Nini maana ya Sheria za Akili?

Bado tupo katika sheria kuu kumi ambazo zina uwezo mkubwa kwa mwanadamu katika kujitambua na kufahamu zaidi maajabu ya ulimwengu.

Sheria ya kwanza ilikuwa inasema kuwa ili kitu kuwepo au hali kuwepo lazima kuwepo kuwa sababu yake. Kwa maana kuwa hakuna tokeo lisilo na chanzo. Kila hali ina chanzo chake kinachopelekea hali hiyo kuwepo, kila kitu kuwepo lazima kuwe kuna chanzo chake kupelekea kuwepo. La si hivyo kisingekwepo.

Katika ulimwengu wa akili, ufahamu na ulimwengu tukaona kuwa chanzo kikuu cha ufahamu ni akili. Mawazo huweza kufanyiwa kazi na kupelekea kuumbwa kwa kilichokuwa kinawazwa. Tukachukulia mfano computer, simu, madirisha, mavazi n.k vyote hivi vilianza kama wazo, idea halafu vikafanyiwa nguvu kazi na vikatokea katika ulimwengu wa kifizikia.

Sheria ya pili ilikuwa inasema kuwa tuna uwezo wa kuelekeza mtazamo wetu popote tutakapo. Unaweza kuamua kuwaza unachotaka kuwaza, unaweza kuamini unachotaka kuamini, unaweza kuamua uelewe nini na ukatae nini. Ni uhuru wa Free Will katika kufikiria. Una uhuru wa kufikiria unachotaka na hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako bali wewe mwenyewe.

KANUNI/SHERIA YA TATU - NGUVU YA UMAKINI.
Katika mojawapo ya hatua za mwanadamu kujitambua, kufahamu sheria hii ni mojawapo kati ya hatua za muhimu sana kwenye kufahamu maajabu ya ulimwengu. Uelewa wa sheria hii ni faida kubwa sana hasa kwa wanadamu wanaopenda kujifunza mengi na kuboresha maisha yao katika njia sahihi.

UMAKINI: Ni nguvu kani. Ni kama vile energy. Umakini unapelekea kukusanya ufahamu wako katika sehemu moja na kupelekea nguvu zako kukusanyika na kuweka nguvu kubwa kwa pamoja.

Mwalimu mmoja wa ki-Asia aliwahi kusema kuwa:
Umakini ni kama mwanga wa jua, unauona ni wa kawaida lakini ukiweka lensi mbinuko unaukusanya mwanga ule na kuwasha moto.

Ni sawa na umakini. Unaweza ukawa umeshawahi kuona tamaduni za kiAsia mtu akiwa anajifunza wanasisitiza mtu kujifunza kwanza kuuongoza umakini. Mfano Kung-Fu mtu ili aweze kutumia nguvu ya Chi anatakiwa aweke umakini wake katika nguvu hiyo na attention yake yote iwe hapo ndipo nguvu hiyo huamka.

Umakini una nguvu kubwa sana katika ulimwengu, ukijifunza chochote kwa umakini unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana. Mfano mzuri ni mimi pale nilipokuwa najifunza Piano na Guitar, ukiweka akili yako hapo kwenye Piano utajikuta unaweza kupiga mzunguko ambao hata hukutegemea kama ungeweza kutengeneza.

Hapo bado hatujaingia katika sheria hii kwa undani. Hapo nilikuwa najaribu kukuelekeza umakini ulivyo. Sheria hii kiini chake kipo hivi.

POPOTE UNAPOELEKEZA UMAKINI WAKO AU FOCUS YAKO PANAKUA. Unapoelekeza ufahamu wako katika hali fulani, mawazo fulani, ufahamu fulani n.k utaona ufahamu uo unakua. Buddha aliwahi kusema hivi,

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Chochote unachoweka umakini hukua.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mfano ukiwa unanyanyua vyuma misuli itatumika sana, halafu baada ya kutumika kunyanyua vyuma hukua na kujaa. Chochote unachokitumia sana kinakua au kinaboreka ili ukitumia vizuri. Hii sio sheria ya ufahamu tu bali hii ni sheria ya ulimwengu, ni sheria ambayo Uasili au Nature imekua ikitumia kufanya kazi yake. Mnyama akitumia kiungo fulani sana kiungo kile kinakua na kuboreka kumsaidia akitumie vyema na kwa zaidi. Kisichowekewa mtazamo au matumizi kunapotea. Hii nisheria ya Nature, na hata akili ni nature hivyo ipo mpaka kwenye fikra, mawazo, misimamo n.k

Mfamo unaweza kukuta mtu anaamini kitu fulani, ameweka ufahamu wake wote hapo na anaamini hivyo na huwezi kumbadili hivyo. Naye anaona anachoamini ni uhalisia kabisa. Kumbe reality yake imetokana na kujizoesha kuamini hivyo na kuelekeza ufahamu wake huko mwishowe anajikuta anaamini hivyo na yeye mwenyewe hajui hilo kwani hafahamu kuwa kuna sheria kama hii duniani.

Kufahamu ufahamu huu itakusaidia kuuliza unachokiamini. Je ni kweli reality yako imetokana na umejizoesha kuamini hivyo au kufahamu hivyo na kupelekea wewe leo hii kuona hivyo au ni reality?

Wewe ni ufahamu wako, wewe unajitambua kupitia ufahamu wako, Hakuna kitu kingekwepo bila ufahamu. Ufahamu ni kinachouona ulimwengu. Kwa sasa ufahamu wako unategemea milango yako ya ufahamu (macho, pua, ulimi, ngozi, masikio) kuutazama ulimwengu. Ulimwengu huu ni ulimwengu wa milango ya ufahamu. Shida unazoziona, raha unazoziona zote unazihukumu kwa kusema hiki ni shida na hiki ni raha kwa kutumia milango yako ya ufahamu na sio ufahamu wenyewe. Ungezaliwa katika ulimwengu unaoamini maumivu ni raha ungeona ni raha kwani ufahamu wako hauna uhusiano na kitu au hali yenyewe. Ufahamu unaweza kubadilika na kupelekea hali kuonekana tofauti kwani ni ufahamu unaohukumu hali na sio hali yenyewe.

Kuelewa sheria hii utajifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa makini na unachokiamini, kuwa makini na kinachoendelea katika akili yako, kuwa makini na matumizi ya hisia zako, kuwa makini na kutazama mawazo yako, kuwa makini kwa kutazama imani na maamuzi yako halafu linganisha na maisha yako ya nje. Kuelewa sheria hii ni kuelewa kuwa ulimwengu wa ndani yetu inaumba ulimwengu wa nje.

Watu walioweza kujitambua na kufahamu sheria hii waliweza kujitahidi kuongoza fikra zao kwa kuumba uhalisia wao. Mtu makini ni mwenye ufahamu kuwa yeye na mchango mkubwa katika kubadili maisha yake na sio kingine. Haijalishi unaishi katika hali gani, ni kubadili mtazamo wako na KUUTAZAMA MTAZAMO WAKO.

MIFANO:
Una maumivu kwenye bega. Unaweza ukaamua kuweka fikra yako katika kuwaza jinsi ulivyo na maumivu katika bega na kukosa raha au unaweza kuweka umakini wako kwa sehemu nyingine za mwili ambazo ni nzima na kushukuru kwa kila jambo. Lakini kuna ambao wataelekeza akili yao kwenye maumivu na wengine wanakata taamaa kabisa na kuona hatapona.

Unaweza ukahisi unaumwa ugonjwa fulani na kuona unaanza kuumwa ugonjwa huo. Upo ushahidi wa kisayansi kuwa kuna magonjwa yanachangiwa na akili. KUna dalili nyingine zimetokana na mtu kuwaza ugonjwa sana na anaanza kuona dalili.

mkuu Apollo mm nashukuru sana kwa hii elimu muhimu sana kwa afya ya ubongo
kiukweli ww ni mmoja wa watu ambao wanaifanya JamiiForums kuwa chuo bora kuliko vyuo vikuu tuvijuavyo

kila ulichokiandika ni kweli kabisa
mm nilipokuwa secondary nilikuwa na uwezo wa ku-concentrate katika jambo moja na matokeo yake yakawa ni makubwa sana yenye kustahajabisha, lakini sasahiv nashindwa kabisa mkuu
hivi naweza kuirudia hali ya zamani ?

Cc: Monstgala
Cc: Pasco
Cc: Rakims

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
nimekuelewa vyema kaka....nasubir mWendelezo
 
Nashukuru sana ndugu yangu, JamiiForums ni sehemu ya muhimu sana kwani hapa tunakutana watu mbalimbali wenye elimu mbalimbali na ujuzi tofauti tofauti. Kwa wanaopenda kufahamu mengi tunatumia nafasi hii kujifunza zaidi.

Unaweza kurudisha uwezo wako kwani bado unao. Kila mwanadamu ana ability ndani mwake, uwezo huo haupungui. Ni sababu ndogo ndogo sana ambazo zinaukinga kama vile matendo yasiyo sahihi, cravings, mazoea mabaya, tamaa, hatred, selfish desires, anger, sexual misconducts, na ignorance. But ukiwa makini katika nidhamu, busara na concentration ability yako inajionyesha.

Ni vyema kuendelea kujifunza mengi, kujichunguza katika matendo yako, kinachoendelea kwenye akili yako, kuboresha sifa nzuri, na kupunguza mazoea mabaya.
 
Mwanadamu ni sehemu ya uumbaji sababu anachokiwaza ndicho kinachoumbika kwenye maisha yake ya kawaida.
Hivyo kama hajajitambua unakuta anajidhuru mwenyewe. Na kama ukijitambua unaweza kuendesha maisha yako kama utakavyo.
 
mkuu aretaskimario wengi wetu tunafaham neno kujitambua lakini huwa hatufaham maana yake na inakuaje-kuaje mpaka mtu anajitambua, na kuna hatua gani mtu anaweza kufuata ili kuanza kujitambua
tafadharini wakuu aretaskimario na Apollo naomba mnidadavulie hii kitu inaitwa kujitambua

Cc: Apollo

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
mkuu aretaskimario wengi wetu tunafaham neno kujitambua lakini huwa hatufaham maana yake na inakuaje-kuaje mpaka mtu anajitambua, na kuna hatua gani mtu anaweza kufuata ili kuanza kujitambua
tafadharini wakuu aretaskimario na Apollo naomba mnidadavulie hii kitu inaitwa kujitambua

Cc: Apollo

.made in mby city.

Hii nimeicopy kutoka kwenye uzi wa Apollo.

Umeshawahi kujiuliza wewe ni nani?
Wewe ni nani?

Wewe sio kazi yako unayofanya, wewe sio kundi la watu unalojihusisha nalo.

Wewe sio mawazo yako,

Wewe sio Akili yako,

Wewe sio mwili wako,

Wewe sio mtu mwenye furaha, huzuni, hasira wala shida kama unavyojifahamu,

Wewe sio tafsiri uliyozoea kuifahamu.

Wewe ni nani?

Wewe sio ambaye wazazi wamekuambia,

Wewe sio ambaye marafiki wamekuwa wakikuambia,
Wewe sio ambaye viongozi wa dini wamekuwa wakikuambia,
Wewe sio ambaye serikali imekuwa ikikuambia,

Wewe sio maelezo unayotumia kujielezea kuhusu wewe.

Achia mbali majina unayoitwa, maelezo unayojielezea kwenye mitandao kama Facebook au mitandao mingine ya kijamii.

Achia mbali jina lako, aina ya mtu unayejijua wewe ndiye, sifa ulizonazo, muonekano, asili, tamaduni yako au sifa ulizoandikiwa kwenye kitambulisho chako cha kazi au masomo,

Je unajisikiaje hivyo vyote ukiviachia mbali na kujiuliza wewe ni nani.

Nini kinabakia ukitoa mali zako, mwili, akili, shida, mawazo yako, imani yako, mazoea yako, tamaa zako, jina unalopewa na watu au unalojipa wewe, na sifa unazopewa na watu na sifa unazopewa wewe?

Wewe ni nani?

Kama wewe sio unachofanya,

Kama wewe sio unachofikiria,

Kama wewe sio unachopenda,

Kama wewe sio maelezo unayotumia kujitambulishia,

Je Wewe ni nani?

Tambua kwa kina...

Hauzuiliwi na mipaka ya mwili,

Wala wewe sio mapigo ya moyo wako,

Wewe sio Akili yako, mawazo yako na hisia zako,

Je kama wewe sio hivyo vyote je wewe ni nani?

Vuta pumzi taaratibu, hewa hiyo inaingia kwenye mapafu halafu inaingia kwenye kila seli ya mwili wako.

Funga macho, acha kuwaza, acha kuweka mawazo nje yako, hisi nafasi inayobakia iliyo kimya, na isiyo fikiria, waza, wala isiyokuwa na hisia yoyote kutoka kwenye milango ya ufahamu.

Kumbuka wewe ni nani, kumbuka hauna mipaka, mwili utakufa utauacha, jinsia yako nayo unaiacha, mali utakuwa nazo bali nazo utaziacha, hisia ulizonazo ambazo chanzo chake ni mwili wako nazo utaziacha mwilini, hasira na mawazo nayo yote utayaacha, sifa ulizopewa kama vile ulikuwa mchoraji bora au mwimbaji bora n.k nazo utaziacha kwani nazo zinategemea mwili mfano unaimba kwa kutumia mdomo lakini ukifa unauacha na huo mdomo na sifa zake ulizozizoea.

Je kama maisha yako ya hapa duniani yatakapoisha vyote hivi unaviacha...

Je wewe ni nani???

Wewe ni ufahamu unaofahamu vyote hivyo,

Jiangalie ndani yako kwa kina,

Wewe ni empty,hauna kitu

Wewe ni sehemu ya muumbaji,

Kila ukionacho, unachokiwaza, unachokitenda, na unachokizungumza kinawakilisha ulimwengu wa ndani yako.

Wewe na mimi ni kitu kimoja, wewe upo kama mimi na mimi nipo kama wewe.

Tunachopaswa kufanya katika safari ya maisha ni kujijua na kujitambua. . .
 
Last edited by a moderator:

Huu ni muendelezo wa Taratibu na Sheria za akili na ufahamu.

Akili ya mwanadamu ni sehemu ambayo watafiti wengi wamekuwa wakihamasika kuielewa. Akili ni sehemu pana sana kwa mwanadamu. Ni sehemu ambayo haionekani wala haishikiki lakini ina matokeo makubwa sana kwa mwanadamu. Akili imezaa vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu, mawazo, imani, misimamo n.k. Kama unapenda sana kujifunza na kufahamu mengi lazima utakuwa unatamani kufahamu siri kuu za akili. Kuelewa siri kuu za akili ni kufahamu Sheria ambazo zinaiongoza akili. Katika mada hii utapata kuona mwanga kuhusiana na akili na kuweza kujifahamu vyema.

SHERIA/KANUNI HIZO NI:

  1. Sheria ya Chanzo na Matokeo
  2. Sheria ya Uhuru wa Kufikiria
  3. Sheria ya Umakini/focus
  4. Sheria ya Mawazo
  5. Sheria ya Ubinafsi
  6. Sheria ya Uumbaji
  7. Sheria ya Hisia
  8. Sheria ya Ubadili
  9. Sheria ya Usawa wa Akili
  10. Sheria ya Kutokea.Nini maana ya Sheria za Akili?

Bado tupo katika sheria kuu kumi ambazo zina uwezo mkubwa kwa mwanadamu katika kujitambua na kufahamu zaidi maajabu ya ulimwengu.

Sheria ya kwanza ilikuwa inasema kuwa ili kitu kuwepo au hali kuwepo lazima kuwepo kuwa sababu yake. Kwa maana kuwa hakuna tokeo lisilo na chanzo. Kila hali ina chanzo chake kinachopelekea hali hiyo kuwepo, kila kitu kuwepo lazima kuwe kuna chanzo chake kupelekea kuwepo. La si hivyo kisingekwepo.

Katika ulimwengu wa akili, ufahamu na ulimwengu tukaona kuwa chanzo kikuu cha ufahamu ni akili. Mawazo huweza kufanyiwa kazi na kupelekea kuumbwa kwa kilichokuwa kinawazwa. Tukachukulia mfano computer, simu, madirisha, mavazi n.k vyote hivi vilianza kama wazo, idea halafu vikafanyiwa nguvu kazi na vikatokea katika ulimwengu wa kifizikia.

Sheria ya pili ilikuwa inasema kuwa tuna uwezo wa kuelekeza mtazamo wetu popote tutakapo. Unaweza kuamua kuwaza unachotaka kuwaza, unaweza kuamini unachotaka kuamini, unaweza kuamua uelewe nini na ukatae nini. Ni uhuru wa Free Will katika kufikiria. Una uhuru wa kufikiria unachotaka na hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako bali wewe mwenyewe.

KANUNI/SHERIA YA TATU - NGUVU YA UMAKINI.
Katika mojawapo ya hatua za mwanadamu kujitambua, kufahamu sheria hii ni mojawapo kati ya hatua za muhimu sana kwenye kufahamu maajabu ya ulimwengu. Uelewa wa sheria hii ni faida kubwa sana hasa kwa wanadamu wanaopenda kujifunza mengi na kuboresha maisha yao katika njia sahihi.

UMAKINI: Ni nguvu kani. Ni kama vile energy. Umakini unapelekea kukusanya ufahamu wako katika sehemu moja na kupelekea nguvu zako kukusanyika na kuweka nguvu kubwa kwa pamoja.

Mwalimu mmoja wa ki-Asia aliwahi kusema kuwa:
Ni sawa na umakini. Unaweza ukawa umeshawahi kuona tamaduni za kiAsia mtu akiwa anajifunza wanasisitiza mtu kujifunza kwanza kuuongoza umakini. Mfano Kung-Fu mtu ili aweze kutumia nguvu ya Chi anatakiwa aweke umakini wake katika nguvu hiyo na attention yake yote iwe hapo ndipo nguvu hiyo huamka.

Umakini una nguvu kubwa sana katika ulimwengu, ukijifunza chochote kwa umakini unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana. Mfano mzuri ni mimi pale nilipokuwa najifunza Piano na Guitar, ukiweka akili yako hapo kwenye Piano utajikuta unaweza kupiga mzunguko ambao hata hukutegemea kama ungeweza kutengeneza.

Hapo bado hatujaingia katika sheria hii kwa undani. Hapo nilikuwa najaribu kukuelekeza umakini ulivyo. Sheria hii kiini chake kipo hivi.

POPOTE UNAPOELEKEZA UMAKINI WAKO AU FOCUS YAKO PANAKUA. Unapoelekeza ufahamu wako katika hali fulani, mawazo fulani, ufahamu fulani n.k utaona ufahamu uo unakua. Buddha aliwahi kusema hivi,

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Chochote unachoweka umakini hukua.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mfano ukiwa unanyanyua vyuma misuli itatumika sana, halafu baada ya kutumika kunyanyua vyuma hukua na kujaa. Chochote unachokitumia sana kinakua au kinaboreka ili ukitumia vizuri. Hii sio sheria ya ufahamu tu bali hii ni sheria ya ulimwengu, ni sheria ambayo Uasili au Nature imekua ikitumia kufanya kazi yake. Mnyama akitumia kiungo fulani sana kiungo kile kinakua na kuboreka kumsaidia akitumie vyema na kwa zaidi. Kisichowekewa mtazamo au matumizi kunapotea. Hii nisheria ya Nature, na hata akili ni nature hivyo ipo mpaka kwenye fikra, mawazo, misimamo n.k

Mfamo unaweza kukuta mtu anaamini kitu fulani, ameweka ufahamu wake wote hapo na anaamini hivyo na huwezi kumbadili hivyo. Naye anaona anachoamini ni uhalisia kabisa. Kumbe reality yake imetokana na kujizoesha kuamini hivyo na kuelekeza ufahamu wake huko mwishowe anajikuta anaamini hivyo na yeye mwenyewe hajui hilo kwani hafahamu kuwa kuna sheria kama hii duniani.

Kufahamu ufahamu huu itakusaidia kuuliza unachokiamini. Je ni kweli reality yako imetokana na umejizoesha kuamini hivyo au kufahamu hivyo na kupelekea wewe leo hii kuona hivyo au ni reality?

Wewe ni ufahamu wako, wewe unajitambua kupitia ufahamu wako, Hakuna kitu kingekwepo bila ufahamu. Ufahamu ni kinachouona ulimwengu. Kwa sasa ufahamu wako unategemea milango yako ya ufahamu (macho, pua, ulimi, ngozi, masikio) kuutazama ulimwengu. Ulimwengu huu ni ulimwengu wa milango ya ufahamu. Shida unazoziona, raha unazoziona zote unazihukumu kwa kusema hiki ni shida na hiki ni raha kwa kutumia milango yako ya ufahamu na sio ufahamu wenyewe. Ungezaliwa katika ulimwengu unaoamini maumivu ni raha ungeona ni raha kwani ufahamu wako hauna uhusiano na kitu au hali yenyewe. Ufahamu unaweza kubadilika na kupelekea hali kuonekana tofauti kwani ni ufahamu unaohukumu hali na sio hali yenyewe.

Kuelewa sheria hii utajifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa makini na unachokiamini, kuwa makini na kinachoendelea katika akili yako, kuwa makini na matumizi ya hisia zako, kuwa makini na kutazama mawazo yako, kuwa makini kwa kutazama imani na maamuzi yako halafu linganisha na maisha yako ya nje. Kuelewa sheria hii ni kuelewa kuwa ulimwengu wa ndani yetu inaumba ulimwengu wa nje.

Watu walioweza kujitambua na kufahamu sheria hii waliweza kujitahidi kuongoza fikra zao kwa kuumba uhalisia wao. Mtu makini ni mwenye ufahamu kuwa yeye na mchango mkubwa katika kubadili maisha yake na sio kingine. Haijalishi unaishi katika hali gani, ni kubadili mtazamo wako na KUUTAZAMA MTAZAMO WAKO.

MIFANO:
Una maumivu kwenye bega. Unaweza ukaamua kuweka fikra yako katika kuwaza jinsi ulivyo na maumivu katika bega na kukosa raha au unaweza kuweka umakini wako kwa sehemu nyingine za mwili ambazo ni nzima na kushukuru kwa kila jambo. Lakini kuna ambao wataelekeza akili yao kwenye maumivu na wengine wanakata taamaa kabisa na kuona hatapona.

Unaweza ukahisi unaumwa ugonjwa fulani na kuona unaanza kuumwa ugonjwa huo. Upo ushahidi wa kisayansi kuwa kuna magonjwa yanachangiwa na akili. KUna dalili nyingine zimetokana na mtu kuwaza ugonjwa sana na anaanza kuona dalili.

Nimejifunza kitu.
Umetumia maneno mepesi na yanayoeleweka.
Naomba uwe unanitag katika madarasa yako.
 
We have a long journey to understand ourselves. For us to understand ourselves we must think beyond our formal education which limit us to a certain laws of life. Nimejifunza mengi hapa na naendelea kujifunza mengi kutoka kwako Apollo. My question is kwanini dini zimefumba juu ya mambo haya? na pia kwanini formal education haitoi elimu juu ya mambo haya?
 
Habari ndugu yangu. Nashukuru sana kwa kunipa moyo, ninaamini wapo watafutaji mbalimbali ambao wanapenda kufahamu zaidi kwani ni muhimu kufahamu kwani knowledge ni mwanga na ujinga ni giza.

Kuhusu Dini kupotosha, kama tunavyosema kuwa kila mtu anaishi katika ufahamu wake na ufahamu huo unaumbwa na uelewa wako, akili yako, milango yako ya fahamu na imani yako, hivyo na walio katika dini nao ulimwengu wao nao hujitokeza. Dini sio mbaya kwani zinatupa uelewa wa kuwa kuna uhalisia zaidi ya huu tunaouelewa, lakini mwanadamu hatakiwi kufikiri kuwa kwa dini anayoamini basi ameokoka bali anatakiwa afahamu kuwa kwa matendo yake na uelewa. Miaka ya zamani mtu kuongea ukweli huu alikuwa anachomwa, ni kama kanisa linajitahidi kuzuia watu kujitambua lakini sio kwa malengo mabaya kwani ukija kufahamu nguvu ya mwanadamu unaweza ukaitumia vibaya, kanisa na dini nyingi zimesaidia kuweka uelewa wa utiifu kwa watu na imesaidia. Lakini mwanadamu mwenyewe anatakiwa aelekeze jitihada zake kufahamu zaidi na kuwa mchunguzi zaidi bila kuhukumu.

Wanasema, UKISHAAMKA KATIKA ULLUSION HAUTAPOTEZA MUDA KUHUKUMU WALIO LALA BALI UTATAFUTA NAMNA YA KUWAAMSHA NA WAO.
 
na mimi uwe unani tag kila unapoweka post za namna hii hakika zinanijenga
 
MMmmm mimi sijaelewa chochote nimetoa macho tu naona hili linawafaa wasomi zaidi
 
Usiwe na shaka. Elimu hii ni kwa kila mtu. Ni kuchunguza kwa umakini maisha kwa ujumla.
 
Asante sana kwa som mkuu, nimejifunza mengi na bado nna kiu ya kujifunza zaidi
 
bro umeniongezea ufaham..mda mwngne nafikiria kuwa elimu tunayopewa madarasani ina uhalisia mdogo sana na maisha tunayoishi.. naamin zaidi katika sheria ya pili na tatu(kufkiria na umakini) kwan hapa ndio penye kujenga na kubomoa..mm naamini hv "Unayeamini kuwa kakuzidi kwa mengi, basi kafikiria zaidi na kwa umakini kukuzidi wewe"..kwa mfn unaweza usiwe na kipaj cha kufanya jambo flan lakin kwa kutumia uhuru wa kufikiria na umakini jambo lile ukalifanya vizur kuliko mwenye kipaji na ww ukaonekana bora na mwenye kipaji..
Asante bro wa mimi
 
Back
Top Bottom