JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Muongozo uliotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuhusu kanuni za maadili kwa wanataaluma wa habari zinaeleza kanuni za maadili kwa Mpiga picha za magazeti kama ifuatavyo:-
Wapiga picha wa magazeti wanatakiwa kutoa picha zinazoonesha usahihi wa hali ya tukio husika.
Wawe makini wakati wanapochukua na kutumia picha za walioathirika na majanga au watu wenye huzuni. Picha za aina hiyo zitatumika inapokuwa lazima kuelezea habari iwapo njia nyingine zote zikiwa zimeshindikana.
Wanatakiwa kuchukulia habari kama mali ya jamii na sio bidhaa ya kuudha ili waweze kuzingitia utu.
Uchukuaji wa bila kibali picha kuhusu maisha ya faragha ya watu au maslahi yao hairuhusiwi.
Upvote
2