PreGE2025 Kanuni za maadili za Tume Ya Uchaguzi: Marufuku kutumia simu kwenye kituo cha kupigia kura

PreGE2025 Kanuni za maadili za Tume Ya Uchaguzi: Marufuku kutumia simu kwenye kituo cha kupigia kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Hizi ni baadhi ya kanuni ambazo ACT Na vile vyama vingine 14 walienda kusaini last week.

Kwa kweli No Reforms No Election. This is too much!

===============

Mtu yeyote hatoruhusiwa kutumia simu ya kiganjani au kifaa kingine cha mawasiliano ndani ya kituo cha kupigia kura, kuhesabia au kujumlishia kura isipokuwa kwa msimamizi wa uchaguzi, msimamizi msaidizi wa uchaguzi, msimamizi wa kituo, wasaidizi wake na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao wataruhusiwa kutumia simu zao au kifaa kingine cha mawasiliano pale itakapobidi kwa shughuli za uchaguzi tu.

Taarifa hii ni kulingana na kanuni za maadili ya uchaguzi wa mwaka 2025 zilizokwisha sainiwa na Vyama vya siasa na kuchapishwa kwenye Gazeti la serikali ambapo mbali ya Maafisa wa uchaguzi kuruhusiwa kuwa na simu

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Simu na vifaa hivyo kwa wakati wote vimetakiwa kuwa vimeondolewa mlio na viwe kwenye mtetemo".

IMG_0984.jpeg


Katika utangulizi wa kanuni hizo, Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Uchaguzi wa haki, huru, amani na wa kuaminika hutegemea ushirikiano na uadilifu wa wadau muhimu wa uchaguzi katika kutekeleza wajibu wao wakati wa kuendesha kampeni na zoezi la uchaguzi ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushauriana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyama vyote vya siasa imeandaa Kanuni hizo za Maadili ya Uchaguzi ili kuweka msingi utakaozingatiwa na washiriki wa uchaguzi pamoja na hatua za kinidhamu zinazoweza kuchukuliwa kwa atakayekiuka Kanuni hizi.

Pia soma: Hizi hapa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za Mwaka 2025
 
Ni kweli.
Uchaguzi ni SIRI.
LAKINI lengo la SIRI hii ni la maslahi kwa Taifa?.
 
kwahiyo uchaguzi wetu unafanyika gizani na matokeo tusubiri kutangaziwa kwenye TV na radio..wakati nchi za wenzetu mfano kenya au zambia hapo wanaruhusu waandishi wa habari wenye kamera na wapiga picha kuanzia kwenye kupiga kura,kuhesabu na kutangaza matokeo..waandishi na makamera yapo live..lakini sie eti tunaimba uchaguzi utakuwa huru,haki na uwazi..ila ajabu sasa hizo njia za kuonyesha hio haki na huo uwazi zimezuiwa.!
 
Simu zikiruhusiwa zinaeweza kutumika kurusha matukio ya kihalifu yatakayotokea kituoni.

Yaani wakati watu wa nchi zingine wapo kwenye 6G, sisi huku wenye viswaswadu tunazuiana kutumia simu kwenye vituo vya kupigia (kuibia kura?) kura.
 
Back
Top Bottom