Kanye West alimshobokea Diamond

kedrick

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
5,080
Reaction score
4,914

Baada ya picha ya staa wa bongo fleva Diamond Platnumz akiwa na Hip Hop staa kutoka Marekani, Kanye West kusamba pamekuwa na maswali mengi ya Ilikuaje mpaka picha hii ikapigwa? .

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema, “Nilipokuwa airport pale Los Angeles tunasubiri kuchukua mabegi yetu, nilisikia mtu akisema ninaweza kupiga picha viatu vyako?

Kwakuwa alikuwa ameinama sikuweza kumtambua lakini alipoinuka nikashangaa kumuona ni brother Kanye West. Nilimuomba tupige picha kwanza halafu vingine vitaendelea. ”
Kuhusu collabo D alisema

“Tumuombe Mungu mambo yaendelee vizuri kama tulivyopanga, kuna kitu kizuri kinaweza kikatokea kati yetu ”.
 
Unamsemea kanye west yupi??? Maana hapa mtaani kuna jamaa tunamwita kanye west...nadhan utakua unasemea huyo!!!
 
Basi watu wenyewe roho mbaya huu uzi utawatoa povu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…