Ye anasema kuwa alikuwa mtumwa wa Wayahudi wanaotawala dunia hii lakini sasa ni mtu huru. Je, unadhani Ye haujui ukweli wa dunia hii?
Kama Ye anaujua ukweli wa dunia hii, kwa nini mtu kama yeye anaposema jambo tunalodhani ni siri ya dunia hii tusimwamini?
Ye anapolitaja jina la Yesu kama kimbilio lake wakati wa dhiki kuu, kwa nini tusiamini kuwa angalau anaujua ukweli fulani kuhusiana na jina hilo (kuliko wengi wetu tunaodhani tunajua ilhali tuko gizani)?
Mheshimiwa Mchungaji Louis Farrakhan, adui nambari moja wa Wazungu na Wayahudi duniani, ambaye Wayahudi wameshindwa kumuua kutokana na nguvu kubwa aliyonayo, anamwamini Yesu na Mtume Muhammad kwa pamoja. Ni Mwislamu kindakindaki lakini si Mkristo! Mbona analitumia jina la Yesu kama kinga na kimbilio lake?
Ye ametoboa siri kuwa kwenye mikataba ambayo wasanii kama yeye huwa wanasaini na hao Wayahudi wenye nguvu, kuna kipengele kinachowakataza wasanii hao kulitaja jina la Yesu. Kama jina la Yesu halina nguvu kwa nini wanalikataza kwenye mikataba?
Kama kweli Wayahudi wanaendesha dunia hii, kama anavyosema Ye, unadhani hawaijui siri ya dunia wanayoiendesha?
Katika kitabu kiitwacho "Malleus Maleficarum" kwa Kilatini (au "Nyundo ya Wachawi" kwa Kiswahili), kilichoandikwa na Heinrich Kramer na Jacob Sprenger na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1486, nyundo hiyo inayozungumzwa hapo ni Jina la Yesu.
Jina la Yesu au msalaba wa Yesu ndivyo vilivyookoa watu dhidi ya uchawi katika kipindi hicho cha karne ya 15. Hivyo ndivyo inavyoelezewa katika kitabu cha "Nyundo ya Wachawi", nilichokisoma chote, kinachoelezea matukio halisi yaliyotokea huko Ulaya zaidi ya miaka 600 iliyopita.
Jina la Yesu lina nguvu kubwa zaidi kuliko kitu kingine chochote kile ulimwenguni. Hiyo ni mojawapo ya siri za ulimwengu huu.
Amka, fumbua macho, na uujue ukweli.
—Enock Maregesi, mwandishi wa vitabu