Kapombe na Tshabalala nuksi Taifa Stars

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Mechi ya kwanza tuliicheza kibabe sana... hadi tukapata matokeo mazuri...

Sijui ni nani akaona wivu na mwenendo mzuri wa Stars hadi akashauri tuwarudishe kikosini wachezaji wenye mikosi na Nuksi.

Kuna wachezaji tukubali muda wao umewatupa mkono. Hao wachezaji wengi wao wako na mikosi ya timu ya stars ya nyakati za nyuma.

Ni nani anamshauri vibaya kocha? Kocha alianza vizuri tu kwenye selection zake ingawa kulikuwa na makosa mawili matatu.

Tutaiona AFCON tutakapo achana na ujinga huu.
 
We kweli ndo kiazi akili zote kwenye mawazo mgando. Mpira uliosababisha tufungwe goli umeshindwa kudhibitiwa na Dickson Job hadi tukafungwa hapo kapombe na Tshabalala wanahusikaje?

Tshabalala kapiga mpira mkubwa na Taifa Stars imeanza kuzidiwa katikati baada ya kutoka Mzamiru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…