mugah di matheo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 6,307
- 12,410
Licha ya ushindi bado mapengo yao yalionekana Sasa aibu imewatoka wamewarudisha kundini fullbacks bora afrika nzima.
======
Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam alitoa taarifa iliyokuwa ikinahusu kuogezwa kwa wachezaji hao wa wili wanaochezea klabu ya Simba.,
"Maneno yalikuwa mengi sana baada ya uteuzi uliofanyika mwanzoni lakini tumeona matunda yake, kuongezwa kwa Kapombe na 'Tshabalala' ni pendekezo la Kocha Mkuu, Adel Amroache na tayari wamejiunga kambini na wenzao," amesema Karia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , Wallace Karia amesema kuitwa kwa nyota hao ni pendekezo la Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Adel Amrouche na sio matakwa ya TFF.
Aidha Karia amesema wao kama TFF hawajakaa wala kumshauri Amrouche kuhusu uteuzi wa kikosi isipokuwa walimpa uhuru wakiamini ni kocha mzuri na anayetambua vyema wachezaji kwani alishaanza kuwafuatilia kwa muda mrefu hapo nyuma.
"Sisi hatuwezi kuingilia majukumu yake kwa sababu tunaamini katika weledi aliokuwa nao, jukumu kubwa kwetu ni kuendelea kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tufikie malengo yetu kama taifa," amesema Karia Rais wa TFF.
Stars itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumanne hii ya Machi 28 ikiwa na morali kubwa baada ya mchezo uliopita kushinda bao 1-0 lililofungwa na, Simon Msuva katika mechi iliyopigwa nchini Misri katika jiji la Ismailia.
Katika kundi F Stars iko nafasi ya pili ikiwa na pointi nne nyuma ya vinara Algeria yenye pointi tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu.
Niger ni ya tatu na pointi mbili huku Uganda ikiburuza mkiani baada ya kukusanya pointi moja.