Kapombe, Zimbwe JR waitwa Stars haraka kuiwahi Uganda

Ni jambo zuri. Wakati mwingine tutapiga kelele kuitwa kwenye timu ya Taifa, wachezaji wanaoishi mafichoni! Badala ya kwenye klabu zao zilizo wasajili.
 
Wakianza ktk me hi ya keshokutwa alafu tukafungwa SI wanawatafutia maneno tu, nashauri kikosi kilikile kianze then wao wataingia sub kipindi Cha pili
 
Licha ya ushindi bado mapengo yao yalionekana Sasa aibu imewatoka wamewarudisha kundini fullbacks bora afrika nzima.

saw.jpeg

======

Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam alitoa taarifa iliyokuwa ikinahusu kuogezwa kwa wachezaji hao wa wili wanaochezea klabu ya Simba.,

"Maneno yalikuwa mengi sana baada ya uteuzi uliofanyika mwanzoni lakini tumeona matunda yake, kuongezwa kwa Kapombe na 'Tshabalala' ni pendekezo la Kocha Mkuu, Adel Amroache na tayari wamejiunga kambini na wenzao," amesema Karia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , Wallace Karia amesema kuitwa kwa nyota hao ni pendekezo la Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Adel Amrouche na sio matakwa ya TFF.

Aidha Karia amesema wao kama TFF hawajakaa wala kumshauri Amrouche kuhusu uteuzi wa kikosi isipokuwa walimpa uhuru wakiamini ni kocha mzuri na anayetambua vyema wachezaji kwani alishaanza kuwafuatilia kwa muda mrefu hapo nyuma.

"Sisi hatuwezi kuingilia majukumu yake kwa sababu tunaamini katika weledi aliokuwa nao, jukumu kubwa kwetu ni kuendelea kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tufikie malengo yetu kama taifa," amesema Karia Rais wa TFF.

Stars itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumanne hii ya Machi 28 ikiwa na morali kubwa baada ya mchezo uliopita kushinda bao 1-0 lililofungwa na, Simon Msuva katika mechi iliyopigwa nchini Misri katika jiji la Ismailia.

Katika kundi F Stars iko nafasi ya pili ikiwa na pointi nne nyuma ya vinara Algeria yenye pointi tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu.

Niger ni ya tatu na pointi mbili huku Uganda ikiburuza mkiani baada ya kukusanya pointi moja.
kwahiyo kocha kashinikizwa?
 
nasema tena tunaenda kufungwa na Uganda jumanne hizi shamra shamra inanikumbusha mechi ya Tanzania dhidi ya Msumbiji mwaka 2007 wakati huo uwanja wa Taifa bado mpya zilitungwa hadi nyimbo dk ya 7 tukala kimoja shoka moja mbuyu chini
Tiko tiko mtu mbadi akaingia kambani, nilikuwa taifa siku ile
 
Jibu ni hakuna. Bora hata wangemuita Sure Boy.
Na mimi ndio nawaza hivyo. Huko mbele anakuwepo Samata na Msuva ila mipira kufika ni kazi kweli kweli mpaka Samata anarudia mipira nyuma.

Pale katikati kuna wanaume wanapiga kazi kweli kweli lakini ni ya kukaba zaidi, kina Mzamiru, Hidim Mao. Mudathiri kidogo anajaribu kupeleka mashambulizi lakini hawezi kumfikia Sure Boy mana Sure boy, akitoa pasi anaifuata, huwezi kumuona anajificha asipewe pasi!
 
Nchi ngumu Sana hii niamini Mimi..!

Kuna mjuba Kaweka Uzi Kbs, Eti Kapombe ana mengi Ya Kujfunza Kwa Job..!

Hata huku Vibaruani Na Makazini Wale Wapya huwa Wanachukua nondo na Kujifunza Kazi Kwa Waliowatangulia.!
 
Licha ya ushindi bado mapengo yao yalionekana Sasa aibu imewatoka wamewarudisha kundini fullbacks bora afrika nzima.

saw.jpeg

======

Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam alitoa taarifa iliyokuwa ikinahusu kuogezwa kwa wachezaji hao wa wili wanaochezea klabu ya Simba.,

"Maneno yalikuwa mengi sana baada ya uteuzi uliofanyika mwanzoni lakini tumeona matunda yake, kuongezwa kwa Kapombe na 'Tshabalala' ni pendekezo la Kocha Mkuu, Adel Amroache na tayari wamejiunga kambini na wenzao," amesema Karia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , Wallace Karia amesema kuitwa kwa nyota hao ni pendekezo la Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Adel Amrouche na sio matakwa ya TFF.

Aidha Karia amesema wao kama TFF hawajakaa wala kumshauri Amrouche kuhusu uteuzi wa kikosi isipokuwa walimpa uhuru wakiamini ni kocha mzuri na anayetambua vyema wachezaji kwani alishaanza kuwafuatilia kwa muda mrefu hapo nyuma.

"Sisi hatuwezi kuingilia majukumu yake kwa sababu tunaamini katika weledi aliokuwa nao, jukumu kubwa kwetu ni kuendelea kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tufikie malengo yetu kama taifa," amesema Karia Rais wa TFF.

Stars itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumanne hii ya Machi 28 ikiwa na morali kubwa baada ya mchezo uliopita kushinda bao 1-0 lililofungwa na, Simon Msuva katika mechi iliyopigwa nchini Misri katika jiji la Ismailia.

Katika kundi F Stars iko nafasi ya pili ikiwa na pointi nne nyuma ya vinara Algeria yenye pointi tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu.

Niger ni ya tatu na pointi mbili huku Uganda ikiburuza mkiani baada ya kukusanya pointi moja.
Aaaaaah
 
Back
Top Bottom