Kapten John Komba ana nini na Anne Kilango?

Kapten John Komba ana nini na Anne Kilango?

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
7,375
Reaction score
6,958
Gazeti la Taifa letu la jana tarehe 22/05/2009 lilikuwa na kipande kifuatacho cha habari..

....Pia katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mjumbe Halmashauri Kuu, John Komba aliwaambia waandishi kwamba Mjumbe mwenzake Anne Kilango Malechela si lolote kwenye kampeni za Busanda.

Komba alisema waandishi wa habari wanafanya makosa kumfanya aonekane kwamba Kilango amekuja kuikoa CCM.

''Kama kuzomewa kwenye mkutano wa Katoro hata yeye Kilango alizomewa, lakini mkaficha nasisitiza Kilango alizomewa kama wenzake'', alisema.


Jamani hii imekaaje? ni wivu, au yeye Komba kujiona yuka juu sana, kuongozwa na utashi wa kifisadi, au kitu gani??
 
lazima uelewe profession ya Komba ni mwanakwaya aka msanii,hio post kapata hauri ya kuimba saaaana.shule=00000
habari ndio hio......
 
Ulidhani wanasisiemu wote wanapendana?

Akina Komba wapo Busanda tangu mwanzo wa kampeni, so

ni wazi wasingefurahi kwa mtu aliyepelekwa baadaye

(Anne Kilango) awapige bao kwa kuwashawishi wana

Busanda waipe kura sisiemu! So ndo kama hivyo!

Kimsingi wanajua kwamba kwa sasa hakuna anayeweza

kukiokoa chama hicho, ndo maana wanapondana wao kwa

wao!...Mzee, ndo umefika mwisho wa genge hilo sasa,

hujastukia tu?
 
Jamani hii imekaaje? ni wivu, au yeye Komba kujiona yuka juu sana, kuongozwa na utashi wa kifisadi, au kitu gani??

Ninachoweza kuchukua kutoka maneno ya Komba ni kukiri hadharani kwamba wamezomewa, japo ukweli ulifahamika, lakini walikuwa bize kupinga kuwa walizomewa, tofauti na Mkuchika ambaye anaweza hata kukataa kwa ujasiri kuwa haitwi George Mkuchika.
 
Naona mmemuelewa vibaya Captain J. Komba. Nilvyoelewa mimi alitaka kuweka wazi side B ya huko Busanda ambayo wapasha habari walinaficha,siyo wivu hata kidogo.
Wait baada ya uchaguzi hata brother G.Mkuchika ATAKIRI.
NATAMANI UPINZANI USHINDE WASUKUMA TUNANYANYASWA SANA NA CCM kila kitu nanhenee.
eeeeeh Mungu tunusuru wasukuma na adui yetu namba 1 CCM.
 
Well, mpasuko ndani ya CCM haujanza leo kwa akina Komba na Kilango. Mpasuko uko tangu enzi za Mwalimu na akina Sokoine. Imekuja mpaka zama za akina Lowassa, Kolimba na wengineo wengi. Tofauti na zamani, sasa tumefikia kwenye climax. Watu wameshindwa kuvumiliana anymore. The likes of Mwakyembe, Selelii, Kimaro na wengineo wameamua kujitoa hadharani kuwapinga wenzao. Huyo Kilango anayesifiwa kwa ujasiri, I reserve my comments. Waache wauwane wenyewe kwa wenyewe. Vita ya panzi, sisi kunguru tutafaidi. Tatizo ni nani wa kutuongoza baada ya panzi wote kufariki.
 
Wasukuma ni CCM dam dam!

Angalieni Usukumani: je kuna Mbunge yoyote wa Upinzania licha ya Cheyo??
 
Tatizo ni nani wa kutuongoza baada ya panzi wote kufariki.

Ukituambia nani atatuongoza baada ya hawa mafisadi, hapo naona si sahihi sana Mkuu. Kwani USA waliamini in the first place kuwa Obama anaweza kuwa Rais wao?

In short kuna Watanzania wazuri tu wenye uwezo wa kuiongoza nchi. Nchi haiongozwi na mtu mmoja bali tunahitaji mtu mmoja mwenye busara, hekima na utashi wa Kizalendo aweze kuunda serikali itakayo itoa Tanzania hapa ilipo. Naamini kuwa viongozi wazuri wapo, bali mfumo uliopo na tabaka tawala sasa hivi havitoi nafasi kwa viongozi wenye sifa kuchaguliwa.

Hapa hakuna kuogopa kuwa eti nani atatuongoza, ni fikra kama hizi ndizo zinazotumika kuwadanganya Wananchi kuwa eti wakichagua upinzani basi kutakuwa na vita. Huu ni upotoshaji wa mambo! Hakuna kuogopa, hakuna kulala, tunahitaji CHANGEZ. So wacha waachie ngazi, kwa namna yeyote ile na nchi yetu itaendelea.

I pray to submit
 
Kapten John Komba ana nini na Anne Kilango? Eti kuna hofu kwamba ni nani atatuongoza hawa panzi wakitoweka!
Hakuna uongozi thabiti sasa, ndio sababu Tz tunadidimia katika lindi la umaskini wakati mafisadi ktk ccm wakitamba na viongozi waandamizi wakiendelea kukwapua mamilioni ya fedha toka hazina za umma. Busanda wana fursa ya kuonyesha njia kwa kuwa-ditch CCM na kuchagua Chadema. Chadema, labda wakishirikiana na CUF ktk serikali ya mseto waongoze. Hapo ndipo umuhimu wa Katiba kubadilishwa.
Licha ya kwamba wengi wa Chadema hawajapata uzoefu kuendesha Serikali, ni dhahiri kuwa misimamo yao inatoa matumaini. Huko Karatu, Kigoma na Tarime Chadema kinaongoza Halmashauri za Wilaya, na uzoefu umeonyesha performance huko ni transparent na uadilifu unaonekana.
Jambo muhimu ni wana-Busanda kesho kuonyesha njia kwa kushiriki kuanza kubomoa ccm.
 
..John Komba ndiyo amekuwa mtumbuizaji na mhamasishaji mkuu wa CCM kwa muda mrefu sana.

..sasa nadhani anaogopa kwamba ikionekana Anne Kilango naye ni mpiga kampeni mzuri, basi umuhimu wake[john komba] ktk chama, pamoja na ulaji wake, utakuwa mashakani.
 
Wasukuma ni CCM dam dam!

Angalieni Usukumani: je kuna Mbunge yoyote wa Upinzania licha ya Cheyo??

Mzalendohalisi, unajua ni kwa nini wabunge wa usukumani karibu wote ni CCM? Wasukuma ni watu waoga sana. Wamekuwa wakitishiwa kuwa mkichagua wapinzani wataleta vurugu na kukosa amani. Ukiachilia mbali angalau Bariadi na Magu ambako kulishawahi kuwa na wabunge wa upinzani. Lakini sasa naona wameanza kufunguka macho na kuona kuwa walichokuwa wanaambiwa si kweli na adui yao namba 1 ni CCM. Na kama wataamua kikwelikweli basi CCM ina hali mbaya kwani ndo wengi katika taifa hili. Aluta continua
 
Well, mpasuko ndani ya CCM haujanza leo kwa akina Komba na Kilango. Mpasuko uko tangu enzi za Mwalimu na akina Sokoine. Imekuja mpaka zama za akina Lowassa, Kolimba na wengineo wengi. Tofauti na zamani, sasa tumefikia kwenye climax. Watu wameshindwa kuvumiliana anymore. The likes of Mwakyembe, Selelii, Kimaro na wengineo wameamua kujitoa hadharani kuwapinga wenzao. Huyo Kilango anayesifiwa kwa ujasiri, I reserve my comments. Waache wauwane wenyewe kwa wenyewe. Vita ya panzi, sisi kunguru tutafaidi. Tatizo ni nani wa kutuongoza baada ya panzi wote kufariki.[/QUOTE]


Mzee hii haikuwa nzuri, au ulipitiwa tu, ni kweli una maanisha hawa viongozi wote wanao tuongoza wakifa nchi yetu pia ita kufa??!!
 
lazima uelewe profession ya Komba ni mwanakwaya aka msanii,hio post kapata hauri ya kuimba saaaana.shule=00000
habari ndio hio......


Hii hunishawishi kuwaona watu wa MBINGA kuwa ni -0 (yaani chini ya zero) kwani kwa kumchagua Komba wanalifikiri nini, Bungeni si mahali pa kuimba kwaya.

Huyu jamaa ni Mj**ga sana, nilisikia wakati wa Kampeni Busanda akiwaambia Mkutano wapinzani wana kiherere kama nywele zinaota kila sehemu akaanza kuzitaja.

Anyway CCM ndio wanayataka ma Rubber stamp kama hili gunia ili kupitisha mambo yao ya kifisadi
 
Walimwita aokoe jahazi ....ingawa wana beef naeee....ila alieokoa jahazi kabisa bila ubishi ni magufuli peke yake...huyo muimba kwaya atulie enzi zake zimeshapita......hana jipya hana shule....hana vision.....hii sio karne yake na wenzake .......wanaobebwa kwa ajili ni mwenzetu sio uwezooo..........
 
Kina Komba walikua wanavuna mijiposho tu kwa saaaaaaaaaaaana yeye na Tambwe Hizza
 
Watu kama John Komba ni wale ambo hawajui ni kwanini wapo CCM,wana mawazo ya kijinga sana na kauli za namna hiyo ni za mtu asiyejua jukumu lake.shame on You!
 
Nafikiri ni jambo jema sana NDANI ya ccm kuona frictions kama hizo.

Tunahitaji msuguano huo kuwa kwa kiwango kikubwa zaidi ... !Vinginevyo maedeleo halisi yatatoka wapi?

Tunahitaji Kundi la vipofui kama Komba kuwa kubwa ndani ya chama lijiuge liwe genge la vipofu.....vile vile kundi la Mama Kilango liwe kubwa...

Ni Dynamics nzuri ambayo sioni kama inapingika ili kuliletea taifa letu UHURU HALISI!!!
 
Du. Wamegundua sasa kuwa pesa za kifisadi pekee toka kwa wanamtandao hazitoshi kubadili mwelekeo wa uchaguzi na matokeo ya kura, mpaka kuwapeleka wapiganaji waliopo ndani ya CCM kama mama Kilango kuokoa jahazi.

Haya mama umefanya kazi yako, sasa rudi benchi, mafisadi waendelee kula.

Kuhusu huyo muimba kwaya, ni wivu tu unamsumbua. Anaona umuhimu wake unapotea hivihivi.....
 
Huyu Komba asiwasumbue vichwa yeye anajua kwaya huko kwao Ubunge aliupata kwa kuwa ccm ilisema hata ikiweka jiwe watu watalichagua tu.

Hna vigeoz thats why analopoka tu. Yeye angesema kuwa CCM WALIZOEWA BASI ISYO KUPOINT OUT SASA YEYE ANAPLAY A HERO AU? Kuna sehemu nyingine huwa najiuliza watu wake wakoje kwani kuchagua mtu kama KOMBA!!!!!Mhhhhh
 
Back
Top Bottom