Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amedai nchi haiwezi kupata maendeleo ikiwa katika mfumo wa demokrasia.
Kapteni Traore alitoa kauli hiyo mnamo Jumatatu ya tarehe 1 April 2025 wakati wa salamu za kuanza robo ya pili ya mwaka 2025.
Kapteni Traore alidai hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo huku ikiwa katika mfumo wa kidemokrasia bali maendeleo hupatikana kupitia "Mapinduzi ya kijamii" ambayo yatahusisha wananchi wote wa nchi husika.
Kapteni Traore pia alisema kuwa nchi ya Burkina Faso kwa sasa haipo katika mfumo wa kidemokrasia bali ipo katika "mapinduzi " na akadai kushangazwa na wasomi wanaopotosha umma kwa kutumia neno "demokrasia"
Je, wewe una maoni gani kuhusu madai haya ya Kapteni Traore?
CHANZO: YouTube Channel ya Shirika la Habari la Burkina Faso( RTB)