Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Japo mimi si wa makamo sana ila husoma sana Vitabu vya hawa nguli wa fasihi.

E. Kezilahabi nimesoma vitabu vyake kadhaa. Nilipenda zaidi Rosa mistika. Aisee hicho hakiishi utamu. Kinaendana na mazingira ya kila namna. Ama kwa hakika kila nikikisoma hugundua jambo jipya katika mtoririko wa aya zake.

Vile vile Dunia uwanja wa fujo nakumbuka harakati za Tumaini na jinsi alivoishia hukumu ya kunyongwa.

Kiufupi, mimi hupendelea riwaya zenye Kunga na uficho fulani kifasihi ambao hauhitaji mtu uelewe moja kwa moja kinachozungumzwa.
Ndio maana Hussen Tuwa nae huwa ananikamata sana na mfululizo wa vitabu vyake.
Ben R. Mtobwa nae huwa sishibi bubujiko la lugha yake ya kifasihi.

Nina soft copy ya Rosa mistika na Nagona. Ila nashindwa kuviattach hapa. Nielekezeni
 
Waandiahi wa zamani walipewa uwezo wa kuchambua na kidadisi Mambo.
 
Asante G Ni ngumu sana hata watu kuelewa why now...... ila nikupongeze sana kwa kutubrash sisi ambao hatukukisoma. Namkubali sana Masoud Kipanya
 
N


Naomba ukielekezwa tafadhali unitag
 
Walikuwa wanamanisha nini? Ila Mambo mazuri ndo huwa yanakatazwa na kuacha mamvo ya hovyo hovyo.
 
GuDume kwa niaba ya wote nakushukuru kwa kukichambua Kaputula la Marx nakuomba ufanye kama hivi katika fasihi ya Seithy Chachage ya Makuwadi wa soko huria. Japo E. Kezilahabi yupo hai huko Botswana huyu Chachage yalimkuta ya kumkuta sasa tunaomba ili tufahamu naye aliandika nini tuamke sie wasionacho.
 
Kitabu hiki nilikinunua mwaka 2007 kama sikosei kikapotea katika mazingira ya kutatanisha bila kuanza kukisoma naahidi nikikipata tena nitakisoma nikilete jamvini tukae kitako tukojadili.

 
sasa hivi hatuna waandishi wa sanaa kama wapo ni wachache wengi wanaandika vitu vya kufikirika ambavyo havina nafasi katika jamii yetu zaidi ya kuegemea umagharibi, ngono na vitu vingine vyenye mchango mdogo wa kuchochea fikra zetu
 
Da mkuu vitabu vizuri sana hivyo. Hizo softcopy ziko kwenye mfumo gani? eg: PDF.... Ukipewa email unaweza ku-share?
 
Mkuu tutumie.
 
Kama ni pdf na unatumia jf app, tazama chini ya hapo unapo type utaona maneno photos, Files na alama ya kujumlisha kama kwenye kiboksi. Hiyo ndio sehemu ya kuattach
 
watanzania hawasomagi vitabu mkuu
 
Pole
 

Inachekesha sana hii kauli ya huyo dingi! Hivi huyu Profesa Kezi yuko wapi siku hizi?
 
Nimecheka sana eti kaptula la Max na shati la Mao alafu vyote havimtoshi ha ha ha ha a literature tamu sana
 
Natafuta sana cha rosa mistika niliuliziaga maktaba ya mkoa wa moshi na moro bila mafanikio yeyote
Mkuu nenda mitaa ya samora pale kuna wadau unawapa title wanaenda kukutafutia pia kuna ma guru wengine wako nyuma ya new africa hotel pale
 
Mkuu nenda mitaa ya samora pale kuna wadau unawapa title wanaenda kukutafutia pia kuna ma guru wengine wako nyuma ya new africa hotel pale
Ntakitafuta nijisomee niongeze mbolea kwenye ubongo wangu make dilution imezidi kutokana na viongozi wa hii awam.
 
Hiki kitabu nilikua natamani sana kukisoma , kama kuna mtu anaweza kunambia nawezaje kukipata hata online nitafurahi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…