Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Hahahahha mkuu literature ulipata mswaki au?
Jamaa anamaanisha kuwa yule mzee amekengeuka yale alokuwa anayapondea ndo anayatenda yani kiufupi anakula matapishi yake.
Nimeuliza tu kama kukengeuka na kushindwa kuongea huko ni habari za kweli; na kama kumetokana na stroke ama la. Sasa mambo ya kupata mswaki wa Fasihi sijui yanatoka wapi. Walangira bwana !!!

Kutokana na ubora na upana wa kazi zake, kwangu mimi Kezilahabi ndiye mwanafasihi bora kabisa katika fasihi ya Kiswahili ukimwondoa nguli Shaaban Robert. Hawa ni watu wa muhimu sema tu hatuna tabia ya kuenzi "mashujaa" wetu.
 
Gamba la Nyoka na Dunia Uwanja wa Fujo. Hizo ni fasihi andishi ambazo zina ubora wa hali ya juu sana. Hadithi zake zinaishi mpaka leo.
Lakini cha kusikitisha kizazi hicho kimeondoka na HAZINA YAKE, HAKIJARITHISHA KWA KIZAZI KIPYA.
Nina kitabu cha Njama, nakisoma mara kadhaa, utafikiri kimetungwa jana kilivyo na mvuto na unogo katika kukisoma.
Kina Elvis Musiba hawakuacha kipawa kwa kizazi kipya.
 
Ule msemo wa kiswahili "UKITAKA KUMUUA NJAA MTANZANIA MPE KITABU" una nafasi sana kwa jamii.

Ukitaka kukusanya shilingi kwa wabongo elezea kitu kwa undani alafu waache njia panda waambie 'story zaidi ipo kwenye kitabu fulani" na hakikisha una copy za kutosha.

Kwa ufupi watanunua kama si vyote, but utapata faida,
 
If we all know the power if educating our minds! Kusoma vitabu ndio mpango mzima
 
Bado una hivyo vitabu?
Babu alikua navyo vingi mno hadi vya watunzi Wengine kama Kuli,tumgidie Bwege,Mtu ni utu,muhi huwa mwema, unyama wa mafia nk.
Sema mda umepita tokea afariki 1994 ngoja nikafukue makaburi kama bado kuna masalia
 
Kwa maelezo haya huyu KB ni kweli bado yupo na anasumbua na maelezo yake sumbufu kwa njia tuitayo kupitisha maadili na ustawi wetu....! Ila kwa sasa hatutafuata maelezo yake sumbufu...tutatafuta 'shoti kati'...! Ingawa njia tutakayopita itakuwa na vikwazo kadhaa na vinavyovumilika...lakini itakuwa fupi na tutafika haraka. Tukifika huko huyo KB tutam'tag' kwenye mtandao wetu ajionee mapicha na mavideo kedekede ya ustawi wa nchi yetu. Asubiri aone.

Hah hah hah....

Nimekuelewa Sana Mkuu.
 
2010129000154.jpg

nyongeza katika hayo
"Korchnoi" ni jina la Kirusi, "Brown" ya Kiingereza; hii inarejea njia ya Tanzania ya Nyerere kati ya "mashariki" ya kikomunisti na "magharibi" ya kibeberu
Svoboda: neno la Kirusi la kumaanisha "uhuru"; jina la nchi larejea wito wa mapinduzi ya Kifaransa -taz. chini-
Fraternite: neno la Kifaransa la kumaanisha "undugu" - ni moja ya wito 3 za mapinduzi ya Kifaransa "liberte, egalite, fraternite" (uhuru, usawa, undugu)
 
Gudume hujawahi kuniangusha, shukrani sana umenikumbusha mbali sana, Dunia inaenda kasi Sana vitabu kama KIVULI KINAISHI, KAPTULA LA MAX nk sasa hivi vimewekwa kapuni japo ni vitabu vinavyo fikirisha sana.
 
Hahaaaaa ukisoma vizuri kazi za kifasihi kwa jicho la kifasihi unafaidi mmbo mengi matamu sana yasio fahamika kwa wanaosoma kazi hizi kama magaazeti na kupita, kazi kama vile Kufikirika, Kusadikika, unaposoma kazi kadha wa kadha na kukutana na wahusika kama Bi Kirembwe, Mtolewa, Bawabu 1&2 unaweza chukulia poa but kuna mambo mazito sana yanayozungumziwa, Umewahijiuliza mhusika Bi Kirembwe ana fananishwa na nanani? Ahsate muheshimiwa
 
kwenye vitabu kuna maarifa zaidi ya bahari,tatizo jamii yetu si wasomaji wa vitabu.
 
Babu alikua navyo vingi mno hadi vya watunzi Wengine kama Kuli,tumgidie Bwege,Mtu ni utu,muhi huwa mwema, unyama wa mafia nk.
Sema mda umepita tokea afariki 1994 ngoja nikafukue makaburi kama bado kuna masalia
Pamoja
 
Mkuu zamani wabongo walikuwa wanaandika Fasihi bora sana. Sikuhizi ukikuta riwaya zinazouzwa hazivutii hata kusoma na macover yao ya marangirangi.
Nilibahatika kusoma Dunia uwanja wa fujo.Hicho Kaptula la Marx sijawahi soma. Ni wakati wa serikali na Baraza linalohusika wafungulie vitabu walivyofungia. Kuna kile shamba la wanyama/ Animal farm na kile the dark side of Nyerere. Hakuna haja ya kuendelea kuvifungia. Kuna kitabu kimoja cha zamani kinaitwa Bosi, umewahi kisoma?
Na wasomaji bora wa hizo fasihi na maandiko mbalimbali walikuwepo pia maana mtu yupo primary anasoma andiko ambalo halina hata picha
 
View attachment 863547
nyongeza katika hayo
"Korchnoi" ni jina la Kirusi, "Brown" ya Kiingereza; hii inarejea njia ya Tanzania ya Nyerere kati ya "mashariki" ya kikomunisti na "magharibi" ya kibeberu
Svoboda: neno la Kirusi la kumaanisha "uhuru"; jina la nchi larejea wito wa mapinduzi ya Kifaransa -taz. chini-
Fraternite: neno la Kifaransa la kumaanisha "undugu" - ni moja ya wito 3 za mapinduzi ya Kifaransa "liberte, egalite, fraternite" (uhuru, usawa, undugu)

Shukrani kwa ufafanuzi!
 
Nadhan wameviweka kapuni baada ya kuona vijana wengi wa sasa siyo critical. Na pia wahusika hawapend vijana wasome waelimike...wawe great thinker.so wanahusika kuwaharibu halafu watoto wao wanasomeshwa nzuri za kuwasidia kujenga hoja. Vijana wengi kwa sasa ukiwachenga kidogo kwenye andiko la kiswahili tu wanaibuka na matusi. Hawawezi jenga hoja.. wamejifunza sana matusi kuliko kufikiri.

Elimu ya sasa ya ubabaishi mwingi. Wengine tulisoma when education was education. Siyo kizazi hiki cha copy and paste. Siyo kizazi hili cha kuforward.ukimuuliza aliyeforward hiyo meseji inahusu nini atakwambia "aaah.... Kuna jamaa yangu kanitumia nikaona nishirikiane nanyi"

Back
Top Bottom