Unajua. Kulikuwa na sababu zake kwamba hata katika baadhi ya akademia za kale za Wagriki Sarufi, Mantiki (Logic) na Fasihi kuu yalikuwa masomo ya lazima. Fasihi inasaidia sana katika kukomaza uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa njia mbadala mbalimbali. Pia ni njia nzuri ya kutolea povu hasa kwa tabaka gandamizwa.
Sisi leo kila mtoto tunataka awe mwanasayansi pamoja na ukweli kwamba kuna baadhi ya tasnia (mf. Siasa na uongozi) wanasayansi wengi hawaziwezi kutokana na mfumo wao wa kufikiri (kisayansi).