..ni CHANGAMOTO kubwa kwelikweli.
..waandishi wa vitabu [hadithi, mashairi..]hawawezi kupatikana ktk mazingira hayo ya shule zetu kuwa na uhaba mkubwa wa vitabu, haswa vitabu vya watoto.
..jambo lingine watoto wetu hawafundishwi SANAA, MUZIKI, na TAMTHILIA. Kwa hiyo itakuwa vigumu kuwa na wachoraji, wanamuziki, au waigizaji filamu, waliopikwa na wenye uwezo wa kufanya kazi na zikatambulika kimataifa.
..Na kama hatufanyi mambo yote hayo, lugha yetu adhimu ya KISWAHILI nayo tutashindwa kuihifadhi, kuikuza, na kuieneza.