Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu

Ila huyu Kezilahabi alikuwa na lugha kalikali. Kwenye Dunia uwanja wa fujo kuna kabinti kalibalehe na kakaanza ishu za wavulana vichakani. Basi dingi yake akakakamata na kuanza kukapa stiki huku akisema " vimatako vyenyewe vikavu halafu unataka kutuletea nyege"
 
Mkuu zamani wabongo walikuwa wanaandika Fasihi bora sana. Sikuhizi ukikuta riwaya zinazouzwa hazivutii hata kusoma na macover yao ya marangirangi.
Nilibahatika kusoma Dunia uwanja wa fujo.Hicho Kaptula la Marx sijawahi soma. Ni wakati wa serikali na Baraza linalohusika wafungulie vitabu walivyofungia. Kuna kile shamba la wanyama/ Animal farm na kile the dark side of Nyerere. Hakuna haja ya kuendelea kuvifungia. Kuna kitabu kimoja cha zamani kinaitwa Bosi, umewahi kisoma?
Hapana mkuu sijasoma hata kimoja hapo. Nitumie ulivyonavyo!..
 
Mkuu zamani wabongo walikuwa wanaandika Fasihi bora sana. Sikuhizi ukikuta riwaya zinazouzwa hazivutii hata kusoma na macover yao ya marangirangi.
Nilibahatika kusoma Dunia uwanja wa fujo.Hicho Kaptula la Marx sijawahi soma. Ni wakati wa serikali na Baraza linalohusika wafungulie vitabu walivyofungia. Kuna kile shamba la wanyama/ Animal farm na kile the dark side of Nyerere. Hakuna haja ya kuendelea kuvifungia. Kuna kitabu kimoja cha zamani kinaitwa Bosi, umewahi kisoma?
Hicho cha the dark side of nyerere tupe udodonozi
 
SHIMBA YA BUYENZE,
Fasihi yetu imegeuka mipasho, magazeti ya jamaa mmoja anayeweka kidokezo "IN GOD WE TRUST" lakini ndani yamejaa ugoro mtupu pamoja na vipindi vyepesi vya redio viitwavyo shila wada ndio imekuwa fasihi yetu kwa sasa , hakuna mwandishi anayeumiza kichwa kuandika mambo magumu wala hakuna msomaji anayeumiza kichwa kusoma mambo magumu. Ni udaku kwenda mbele , magazeti ya udaku saa mbili asubuhi tuu yote yameisha.
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]mim nikijana mdogo wakati huo skuwepo na shule nimesoma lakin si hadi kwa levo za juu je sokoni kipo au kukipata unaweza tumia njia gani
 
Tatizo umagharibi umetuharibu sana. Kwa asili yetu waafrika sanaa ni mali ya jamii nzima, hivyo msanii aliona fahari kuona kazi yake ikielimisha au kuburudisha jamii yake tofauti na sasa ambapo wasanii wanawaza pesa tu.

Naamini wasanii kama watafanya kazi nzuri, jamii itahamasika kupenda kusoma/kusikiliza au kutazama kazi za sanaa kuliko kuacha kabisa kutumia vipaji vyao.

Hivi kwa zana hizi ambazo kumkosoa mh.rais ni kosa la jinai akiibuka mwanafasihi akaweza kutumia kalamu yake vizuri kama walivyokuwa wakifanya akina Kezilahabhi, Chinua Achebe, Ngugi wa Thiongo n.k atakosa wateja?

..utamaduni wa kusoma na kufurahia vitabu ni jambo ambalo linapaswa kujengwa kwa watoto eanaoanza shule za vidudu au shule ya msingi.

..bahati mbaya sana waTz wengi tunasoma shule zenye upungufu mkubwa wa vitabu na zisizokuwa na maktaba.

..wengi tuliopitia mfumo wa elimu wa Tz tumekutana na maktaba tulipojiunga chuo kikuu.

..mazingira hayo hayawezi kujenga jamii yenye utamaduni wa kupenda kusoma vitabu.
 
Kweli hii ni changamoto kubwa inayolikabili taifa letu!
 
Tatizo umagharibi umetuharibu sana. Kwa asili yetu waafrika sanaa ni mali ya jamii nzima, hivyo msanii aliona fahari kuona kazi yake ikielimisha au kuburudisha jamii yake tofauti na sasa ambapo wasanii wanawaza pesa tu.

Naamini wasanii kama watafanya kazi nzuri, jamii itahamasika kupenda kusoma/kusikiliza au kutazama kazi za sanaa kuliko kuacha kabisa kutumia vipaji vyao.

Hivi kwa zama hizi ambazo kumkosoa mh.rais ni kosa la jinai akiibuka mwanafasihi akaweza kutumia kalamu yake vizuri kama walivyokuwa wakifanya akina Kezilahabhi, Chinua Achebe, Ngugi wa Thiongo n.k atakosa wateja?
Hili inabidi litazamwe katika mfumo mpana wa kijamii. Jamii yetu inaionaje dhima ya elimu na maarifa katika maendeleo yake? Kuna faida gani ambazo Mtanzania atazipata kwa kujisomea vitabu? Kwa vile tafiti zimeonyesha kwamba usomaji wa vitabu umeporomoka sana, ni lazima tujiulize: Kwa nini watu wetu hawapendi kusoma vitabu? Je, vitabu ni ghali sana? Hakuna waandishi wazuri? Makampuni ya uchapishaji yanaendeshaje biashara zake? Ni nani anayefaidika na kazi za wanafasihi wetu? Tutafute kiini. Tuihamasishe jamii. Kufanya vinginevyo haitasaidia sana.
 
Fasihi yetu imegeuka mipasho, magazeti ya jamaa mmoja anayeweka kidokezo "IN GOD WE TRUST" lakini ndani yamejaa ugoro mtupu pamoja na vipindi vyepesi vya redio viitwavyo shila wada ndio imekuwa fasihi yetu kwa sasa , hakuna mwandishi anayeumiza kichwa kuandika mambo magumu wala hakuna msomaji anayeumiza kichwa kusoma mambo magumu. Ni udaku kwenda mbele , magazeti ya udaku saa mbili asubuhi tuu yote yameisha.
Kweli mkuu. Nilishawahi sema mahali kuwa huyo jamaa mwenye magazeti yenye kauli mbiu za kilokole single handedly ameweza "kuangamiza' kizazi kizima. Ametajirika ndiyo lakini gharama yake ni kubwa sana. Tumekuwa taifa la umbea na ushilawadu. Wenye mawazo mapya na fikra chokonozi wanaonekana maadui. Jamii isiyojali. Sad !!!
 
Rosa Mistika, Kwanini umejiua? Rosa anajibu, ni kutokana na maudhi ya Baba yangu... Hiki kitabu ni kitamu saana
Riwaya ya kwanza ya Kezilahabi wakati akiwa bado kijana. Wakati huo akiwa bado hajakomaa kifalsafa na katika Rosa Mistika falsafa yake ya maisha kama ua waridi linalopita ndiyo ilikuwa inajengwa. Ukitaka kumwelewa sawasawa na kuona ukomavu wake wa kifalsafa jaribu kusoma vinovela vyake viwili viitwavyo Nagona na Mzingile; na hata baadhi ya mashairi yake katika Kichomi na Karibu Ndani.
 
Back
Top Bottom